Nimewaza Ujinga: Kwanini magari yasigome kuwaka mpaka dereva atakapochomeka leseni yake na funguo kwa pamoja?

Binafsi nafikiri "itakuja kuwezwkana" ingawa kwa sasa inawezekana ila si kwa mtindo huo uliouainisha hapa. Ulaya madereva wa mabasi na malori wanaendesha kwa kutumia kadi janja, kadi zenye chip, ambapo ufanyaji kazi wake ni kuwa taarifa za dereva akiwa kwenye usukani zinarekodiwa kwenye gari na kadi kwa hiyo mkaguzi akipata kadi hiyo basi atafahamu speed gari lilivoendeshwa, muda dereva amekaa kwenye usukani, na taarifa hizo zipo kwa siku 30 nyuma. Hilo la gari kuwasha lipo kwenye mabasi, ila dereva anatakiwa kupuliza kipimo cha pombe, kikisoma sifuri ndio basi litafanya kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…