Nimewaza Ujinga: Kwanini magari yasigome kuwaka mpaka dereva atakapochomeka leseni yake na funguo kwa pamoja?

Nimewaza Ujinga: Kwanini magari yasigome kuwaka mpaka dereva atakapochomeka leseni yake na funguo kwa pamoja?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini kusiwe na mfumo ambao utawezesha, licha ya kwamba engine imewashwa kwa funguo, lakini bado gari itagoma kuwaka mpaka utakapochomeka pia leseni yako ya udereva?

Yaaani kunakuwa na direct contact baina ya servers za TRA, Police Traffic pamoja na ignition system ya gari.

(1) Faida yake ya kwanza ni kwamba, hakuna mtu atakayeweza kuendesha gari kama hana leseni (Leseni inakuwa na smartchip kama ya ATM Card)

(2) Faida ya pili ni kwamba, ata ikitokea kuwa gari imeibwa ni rahisi kujua ni leseni ya dereva yupi inatumika kuendesha gari hiyo. Pia Mamlaka husika wanaweza kulizima hilo gari mara moja.

WATAALAM WA ICT, COMPUTER NETWORKING PAMOJA NA MECHANICAL/AUTOMOBILE ENGINEERING msipite bila kusema chochote please.

I STAND TO BE CORRECTED.....!!!!!

Nimelisajili hili wazo langu la kijinga kijinga...!!!!!

NB: TTCL nitawapa wazo kubwa sana la biashara ambalo halipo katika mitandao mingine ya simu za mikononi/kiganjani.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Binafsi nafikiri "itakuja kuwezwkana" ingawa kwa sasa inawezekana ila si kwa mtindo huo uliouainisha hapa. Ulaya madereva wa mabasi na malori wanaendesha kwa kutumia kadi janja, kadi zenye chip, ambapo ufanyaji kazi wake ni kuwa taarifa za dereva akiwa kwenye usukani zinarekodiwa kwenye gari na kadi kwa hiyo mkaguzi akipata kadi hiyo basi atafahamu speed gari lilivoendeshwa, muda dereva amekaa kwenye usukani, na taarifa hizo zipo kwa siku 30 nyuma. Hilo la gari kuwasha lipo kwenye mabasi, ila dereva anatakiwa kupuliza kipimo cha pombe, kikisoma sifuri ndio basi litafanya kazi.
 
Back
Top Bottom