Ukweli kuhusu engines. Engine yoyote kwanza matumizi yake yanahesabiwa kwa masaa engine ilipofanya kazi na siyo km kama wauza/ watengeneza magari magari walivyojiwekea, na kuwajaza watu huo uongo. Fikiria tu Meli,Matrekta, Ndege na mitambo mingi inatumia engines ma hakuna kati ya hizo zinahesabiwa km zilizotembea!
Na kwa mantiki hiyo, kama kila engine inafanyiwa service kama aliyeitengeneza alivyosema, engine itadumu maisha yote. Engine zinakufa kwa kukosea service tu.
Maana yake ni hii.
1. Fikiria kuwa una gari unaamua hutembezi unalipaki lakini kila ukiamka asubuhi unalipiga start na unalizima jioni baada ya saa kumi. Gari hilo kwa mwezi, miezi mwaka litakuwa halikutembea ila engine imeshafanya kazi kila siku masaa 10.
2. Fikiria pia unaamua gari lako hilo unalifunga kamba na kulivuta kwa gari lingine kila siku kwenye mizunguko yako yote, tuseme km 150 lakini hulipigi start, dash itasoma imetembea km 150/day x 24 kwa mwezi tuseme kuna weekend n.k. Engine itakuwa as new maana haitumiki.
Hii wauza magari hawataki mtu ajue lakini ndio ukweli gari la kwanza litakuwa na km chache zilizotembea lakini engine ni mbaya maana imechakazwa na gari la pili limetembea km nyingi lakini engine ni mpya.
Muhimu ni kufuata manuals za manufacture wa gari wanataka oils za specification gani na kubadili baada ya muda gani, engine yoyote ile itadumu.