Nimeyakumbuka maisha yangu ya uyatima; Uyatima ni noma sana ndugu zangu

Pole sana mkuu.

Story yako inafanana na ya kwangu kwa kiasi kikubwa. Nimepoteza wazazi nikiwa shule ya msingi, nikalelewa na shangazi ambaye upendo wangu kwake hauelezeki. Mungu ampe maisha marefu shangazi yangu.

Wenye wazazi shikilieni haswa, hao watu hawana replacement. Niliiona dunia ikinizomea siku mwenyekiti wa kitongoji chetu alipoleta taarifa ya kifo cha mama baada ya mzee kutangulia miaka mitatu nyuma. Hadi leo nikipata nafasi huwa najifungia nalia sana
 
Hauko peke yako angalau wewe ulionja malezi ya baba na mama wengine wapo hawajawahi kupata fursa za wazazi
 
And therefore you are the best woman any man would wish to marry. Hongera usibadilike
 
 
Hongera kwa kupambana kijana. Naomba wote waliokunyanyasa uwape shukrani za dhati. Ni MUNGU tu alipenda upate changamoto hizo ili ujifunze. Tazama wote waliopewa malezi bora Walifeli.
 
Mungu ni mwema akawainulia shangazi ambaye hakuwaacha. Poleni Mungu atujalie uzima hadi tukuze watoto wetu wajitegemee. Watu makatili sana hadi kwa yatima hawana huruma
 
Mkuu Mali za baba yako kama ni tangible,mfano magari,nyumba, viwanja,bank account kuna hela,hasa hasa km alikuwa ni mfanyakazi wa serikali, unaweza fungua mirathi na kila kitu kikarudi kwa watoto, yaani wewe na ndugu zako kwa kwenda mahakamani.
Kama ndugu wamechukua Mali za baba yako na hawakukusaidia,bora urudishe mikononi mwako kwa sheria.
Kwa maelezo ya ziada njoo inbox
 
Nafkiri jamaa anaogopa kuoa sababu akioa automatic ataacha mbegu duniani, sasa uskute anawaza jinsi mbegu yake itakavyoteseka yeye akiwa hayupo, huku mwanamke ana'enjoy mali zake na janaume jingine!
Mchizi aliwahi sema anao watoto kama sikosei

Ila hataki ndoa na mtu yeyote[emoji2]
 
Laiti kuwa single ndio ungekuwa utamaduni wa dunia wote walioa na kuolewa wangekuwa na matatizo ya kisaikolojia[emoji2]

Binafsi sina tatizo na maisha aliyojichagulia mtu maadam havunji sheria za nchi na asili.

Hayo ni maisha,aachiwe mwenyewe ,wala mtu hapaswi jiumiza kichwa mambo yake aachie mwenyewe.

Siwaelewi watu wanaotaka uishi kama wao au wanaokuponda kwa maamuzi juu ya maisha yako.

Siwaelewi kabisa
 
Nenda Naye apate kilicho Bora..


Uamuzi mzuri Sana huu...


Familia na mengine yatakuja yenyewe..

Kila Jambo Lina mda wake..mkuu..
 
Huyu mtoa mada ni dizaini ya wale ndugu lawama. Hawa huwa hanawaga shukrani zaidi ya lawama kwa waliowasaidia kufika hapo walipo. Analaumu ndugu hawajamsaidia lakini ukifatilia stori yake unakuta kuna maeneo meng tu kasaidiwa na hao anaowaponda.

Ndomaana kuna jamaa yangu alisema hataki kusikia mambo ya kukaa na watoto wa ndugu nyumbani kwake. shukrani zao ndo zinakuwaga kama hizi. eti nimejisaidia mwenyewe nyooo...mtoto toka lini akajisaidia mwenyewe na akainuka?
 
Mzee wee ni mama wa kambo nn..mbona unaroho mbaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madam salama?
Povu la nini?

Hebu tulia kwanza.

Wapi nimesema ""nimejisaidia mwenyewe nyoo....""

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…