Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Nimeona draw ya nusu fainali ya CAFCL nimezidi kuumia. Mamelodi ambaye ndio kapewa nafasi yetu amepangwa na timu dhaifu ya Esperance.
Kwa tuliyoitazama Esperance ilivyokuwa hatua ya makundi na robo fainali, huu ni mteremko kwa Mamelodi.
Mamelodi anaenda kushinda nje ndani na kutinga fainali kwa mserereko. Inaniuma sana sababu nafasi hii ilikuwa ya Yanga.
Na kwa ninavyoziona timu zikizobaki, Ahly alivyocheza vibaya na Simba, Mazembe tuliyoipiga nje ndani mwaka jana, Yanga ingeweza kushinda hata kombe lenyewe hili na kutinga kombe la Dunia.