Nimezuiliwa kuingia hospitalini kisa ebola

Nimezuiliwa kuingia hospitalini kisa ebola

Selikavu

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2017
Posts
6,346
Reaction score
14,546
Habari za Asubuhi wakuu

Leo nimejiimu mapema nikamwone Mgonjwa Hospitali ya wilaya ya Nyamagana Mwanza ..

Cha ajabu nimezuiliwa na walinzi kwamba mtu anayeruhusiwa kuingia ni Mwenye chakula cha mgonjwa tuu ili kuepuka maambukizi ya ebola

Swali langu limekuja je serikali imeshatoa tamko kwamba dude hili limefika au la... na kama ni kweli hizi hatua kwel ni za kupambana na maambukizi ama kuzua taharuki tuu maana najua Ebola ni another issue

Naomba kuwasilisha
 
Nipe namba za hao walinzi niwatumie Hela ya supu chaap.
"Mfanyiwe nini enyi Wagalatia msio na akili"
😒
 
Wakichukua hatua hamtaki...

Wakikaa kimya hamtaki .....

Wakiongea mnasema waongo...

Wakiongea ukweli mnasema uongo wanazua taharuki....
🙌🙌
Ebola unaifahamu au unaisikia mkuu
 
Ngoja kwanza, umejitazame kwenye kioo, inawezekana unaonyesha unakila dalili za ugonjwa huu hatari ndio maana askari wakakutilia shaka pengine upo nao.
 
Back
Top Bottom