Nimfanyaje huyu dada? Yamenikuta leo asbh


Jestina, mimi sina hizo tabia unazofikiria za kumnyanyasa mtu kwa kutumia uwezo mdogo wa kiuchumi nilionao. Lifti huwa natoa kwa watu wote na jinsi zote, ila sikuwahi kupata changamoto kama hii. Na kwa taarifa yako mi huwa sitongozi mtu hovyo maana ninaheshimu imani na msimamo wangu. Ila nashukuru kwa ushauri kuwa nisimpe lifti tena. Nakushukuru
 
Unauliza umfanyaje kwani ulikuwa unataka kumfanya nini?? Kama hataki lifti nenda zako
Kwani mmeshirikiana kununua hiyo gari mpaka ujiulize maswali mengi hivyo??

Wewe una lako jambo sio bure
 
kuna sehemu umetoa habari zisizo sahihi, kuna kamchezo mlipanga kukafanya....maana haiingii akilini yeye ku react namna hiyo kama uhusiano wenu ulikuwa ni wa kupeana lift tu.
 
kaingia mitini huyu!
lazima alishachombeza bi shost kafika bei kala mzigo alafu anataka kumpotezea
angalia kijana utawabeba hadi wale wa yule shekhe yaya
 
Kwa kukudhalilisha mbele ya jirani yako, endelea na utaratibu uliokuwa nao mwanzo, mpite kama humwoni otherwise utaendelea kuwekewa masharti yasiyo rasmi ndani ya himaya yako.
 
mazungumzo yako na huyo Dada wa mwAnzo yaonyesha ulimpa matumaini fulani nae akajenga fikra kwamba utabeba mzigo. Sasa kamkuta huyo mwingine kwenye siti aliyodhani yake kafura. Acha kuwapa lifti mademu watakuletea shida bure. Wao wakiwa na magari hawatoi. Nahisi pia hujatulia. BADILIKA.
 
Sioni kama kuna ukweli katika hilo maana sababu ya yeye kutotaka kupanda haipo,hapa inaonekana kuna jambo zaidi ya lifti.
 
Ni story tata kwakweli. sasa kama ilikua ni salamu tu hadi mnafika mjini kwanini asonye na kama huyo jirani yako ni rafiki tu kwanini uone umezalilishwa au mkuu ulikua unampango wa kuwa zaidi ya jirani.
 
wengi wamekujibu vizuri.. Kwa kuongezea usimnyime tena,labda akatae mwenyewe lifti. Na akiingia mwelimishe kimtindo,usimwambie point blank kuwa ulifedheheka kwa tukio lake. Umwambie aelewe, hakuna mwenye hakimiliki ya hilo gari wala seats za ndani yake..! Mweleze kimtindo aelewe kuwa kwa vitendo vyake hivyo anaweza kujipotezea ama kushusha PR yake. She never knows,the next interview ya kazi mpya, kwenye panel na mtoa lifti uliyemziria naye yumo! Au kukosa racket, channels mbalimbali,na madili mengine yanayopatikana kwa kufahamiana.
 
kaingia mitini huyu!
lazima alishachombeza bi shost kafika bei kala mzigo alafu anataka kumpotezea
angalia kijana utawabeba hadi wale wa yule shekhe yaya

si lazima.. Mi nadhani hakumuapproach moja kwa moja. Na huenda HP hakuwa na nia hiyo kabisa. Ila maneno kama,''Mi nakupa lifti mrembo kama wewe,siwezi kupigwa?!'' viutani vya mtindo huo,bidada hakawii kukusubiria utamke rasmi..ye tayari moyo kashaufungua. Na HP angejaribu amualike lunch,au dinner,hata juice kwenye macafé. Angeshangaa,anaitwa jina la 'Dear' kila wakati! Kwa hiyo huyo dada anahisi amekatiliwa penzi lake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…