SoC02 Nimfiche wapi Binti yangu?

SoC02 Nimfiche wapi Binti yangu?

Stories of Change - 2022 Competition

Nsama

Senior Member
Joined
Jul 15, 2022
Posts
192
Reaction score
249
Dunia gunia wahenga walisema, Pilika za maisha hasa utafutaji umetufanya kuwa busy na kusahau wanaotuhitaji zaidi.

Ubusy wa kazi na Safari umenifanya nisipate muda wa kukaa na familia yangu. Nina binti yangu mdogo wa miaka minne,mama yake ni mtumishi na yeye akitoka asubuhi hurudi jioni au usiku maana mahali anapofanyia kazi ni mbali. Muda mwingi nikiwasiliana na mama yake kupitia simu ya mkononi huwa naomba kuongea nae (huyo binti yangu).

Juzi aliniuliza Baba unakuja lini? nikamjibu mwanangu nakuja nikimaliza kazi, akauliza utaniletea zawadi, nikamwambia ndio mwanangu. Nikamwambia kula maisha mwanangu akanijibu nakula maisha na maharage, hahahaha nikacheka mwanangu hajui maisha ni nini yeye anajua maisha ni chakula.

Hapa kwenye maisha ndio nikatafakari ukuaji wake utakuaje, mtoto Anaamka saa kumi na moja alifajiri anaandaliwa na binti wa kazi kwenda shule wakati mwingine wazazi wake bado hatujaamka. Najiuliza usalama wa mwanangu huwa ukoje?, Hizi basi zao(za wanafunzi) huwa zinakaguliwa?, huwa anaenda shule usingizi haujaisha mwanangu makuzi yake yatakuaje?, Nani anamuangalia mwanangu maaadili yake yatakuaje?, nyumbani akirudi Ana binti wa kazi usalama wake utakuaje /ukoje Mmaana Visa vya mabinti wa kazi kuua/kutesa watoto vimeongezeka, Nani anashinda nae anajifunza Nini ambacho sijui(Yuko umri wakujaribu mambo).

Nilifikilia mengi Kwamba siku binti yangu akikuwa atakuwa na sifa, tabia na siha njema ambazo ningependa awe nazo. Maana kwa kiasi kikubwa sishiriki katika ukuaji wake nachoweza ni kutoa pesa ya Ada maana ulezi Ni zaidi ya ada kwa mtoto.

Mtoto wangu sionani nae naishia kuongea nae kwenye simu Ila muda wa kumwagilia moyo(Pombe) napata. Je upendo kwa mwanangu ninaujenga kwenye zawadi tu ninazomuaidi kumpelekea?.

Sijawahi kukaa siku nzima na mwanangu Mara nyingi narudi amelala na anaondoka nimelala. Je mwanangu huyu asipoona upendo wangu ataweza kuwapenda watoto wake kweli(maana upendo hurithishwa)?.

Mara chache Sana nimekaa nae na nipale nilipopigiwa simu mtoto anaumwa au tatizo limetokea. Mtoto Kama anapitia matatizo shuleni na nyumbani atamuambia Nani Kama anashinda na binti wa kazi tu?.

Nasikia kesi za watoto kulawitiwa,kubakwa,kuteswa Hadi kuuwawa nimebubujikwa machozi. Nimetafakari yote hayo nikafilia nimfiche wapi binti yangu huyu Ili asikutane na hii Dunia iliyojaa mabaya kwa watoto kama unyanyasaji wa kingono, uteswaji,ubakaji.

Naanza kumuhofia yule mzee wa jirani ambaye amejenga mazoea na watoto wa kike na kuwaita wachumba, Nahofia mwanangu kwakuwa sishindi nae atakuwa anaitwa mchumba, Nahofia matendo mabaya kwa mwanangu.

Tabia mbaya ndio zimkuwa urithi kwa watoto wetu maana hatushiriki ipasavyo katika ukuaji wao, watoto wanajifunza tabia mbaya Kama wizi, uongo,kutoheshimu wakubwa kutukana n.k

Hii ni tafakuri,mtazamo au fikra ya kubuni nimewaza maisha ya Sasa tumekuwa busy na kusahau wanaotuhitaji zaidi.

Mambo ya kuzingatia kwa wazazi au walezi kwa watoto
  • Hakikisha una hakiki maudhui anayoangalia mwanao Kama Tamthilia, video za Muziki,katuni na filamu. Kuna filamu nyingi maudhui yamelenga watu wazima pia Kuna baadhi ya filamu zinakinzana na tamaduni zetu. Mfano filamu nyingi za magharibi na Amerika Zina maudhui ya Ngono na lugha chafu.
  • Kama simu janja yako Ina picha na video za utupu(pornography) Hakikisha mtoto wako hagusi, ikiwezekana funga na weka mbali ili isiwe rahisi kufikika. Dunia ya Sasa imekuwa ya utandawazi watoto wetu nao wanataka wajue tunacho angalia kwenye simu zetu na pia Wana vitu wanavyopenda Kama katuni na games. Ikiwezekana mtoto atafutiwe kifaa chake(simu/tablet) ili isiwe rahisi kushika simu yako.
  • Mzazi au mlezi fatilia maendeleo ya mtotohasa ya kielimu, Mtoto anapopewa kazi za nyumbani shiriki nae na muelekeze inapobidi. watoto ni rahisi kukata tamaa tuwatie moyo pale wanapopata ugumu hasa kwenye masomo yao. Safari ya Elimu ni ngumu iliyojaa miiba tusipowatia moyo watoto ni rahisi kukata tamaa.
  • Mfundishe mwanao stadi za kazi hasa kazi za mikono na zile zinazochochea ubunifu. Watoto wetu ndio vijana na wazee wa kesho tunapaswa kuhakikisha wanapata maarifa ya mambo mbalimbali Kama kazi za mikono na juzi tofauti tofauti kulingana na mazingira wanayoishi au mambo wanayoyapenda. Mfano Baba ni Fundi selemara au Mama ni Fundi wa kushona nguo Hakikisha mtoto anapata ule ujuzi wa msingi hii itamsaidia baadae pia itamfanya awe mbunifu zaidi.
  • Tuwawezeshe(support) kwenye mambo wanayo yapenda hasa sanaa na Michezo. Wazazi tusiwakitishe tamaa watoto wetu kwenye mambo Kama mpira wa miguu,mpira wa kikapu, Muziki na hata utayarishaji wa Muziki. Ukimkataza mtoto unaweza kuwa umewapoteza Diamond,alikiba,Nikki mbishi,Burna boy, Dr dre,Leo Messi, Christian Ronaldo, Edgar Davis, Selena william, au Aretha Franklin wa baadae.
  • Hakikisha mtoto anapata Chakura Bora, ili akue mwili na akili. Mzazi Hakikisha mtoto anakula matunda na mboga mboga pia apumguze matumizi ya vyakura na vinywaji venye sukari nyingi kwani vinasababisha magonjwa ya kisukari na unene.
  • Hakikisha mtoto anafanyiwa uchunguzi wa Afya ya mwili na akili Mara kwa Mara, hii itamsaidia kugundua magonjwa yanayochelewa kuonekana ili yaweze kupatiwa ufumbuzi kwa wakati.
  • Mfundishe mwanao tabia njema, pia mfundishe Maadili ya Dini na tamaduni anayoishi. Watoto wetu wanahitaji miongozo kutoka kwetu wazazi, tuwaelekeze katika njia nyoofu ili wawe mfano Bora katika jamii. Naamini hakuna mzazi anaependa mtoto wake awe kahaba,jambazi,kibaka, mwizi,tapeli n.k Ni furaha iliyo kuu mzazi kumuona mtoto anafanikiwa na kuja kuwa mtu anaye aminiwa na jamii yake.
  • Mzazi mfundishe mtoto wako kujiamini. Watoto walio wengi wana nidhamu ya woga na hii inawapunguzia kujiamini. Kutojiamini kwa watoto wetu kunawafanya iwe rahisi kurubunika, Dunia ya Sasa imejaa waharibifu Kama wanaopenda kufanya mapenzi na watoto(pedophile),wanaowachochea kufanya uovu(viongizi wa makundi Kama ya Panya road) n.k , Sasa mtoto akiwa anajiamini rahisi kukataa.
  • Pia, mzazi Jenga utamaduni wa kuongea na mwanao, hii itamfanya awe mtu Bora zaidi, itamfanya mtoto akuelezee shida/matatizo yake. Kwa jamii ya kiafrika ni nadra mzazi kujenga urafiki na mtoto hii inawaletea matatizo watoto wetu pale wanapohitaji miongozo na maelekezo yetu hasa kipindi Cha balehe.

Ombi mzazi au mlezi Tenga muda kwa ajiri ya mwanao

kama utavutiwa na makala hii naomba Kura yako
 
Upvote 103
Katika suala la malezi
Mama hakikisha ajira/biashara yako inakupa nafasi na watoto
 
Dunia gunia wahenga walisema, Pilika za maisha hasa utafutaji umetufanya kuwa busy na kusahau wanaotuhitaji zaidi.

Ubusy wa kazi na Safari umenifanya nisipate muda wa kukaa na familia yangu. Nina binti yangu mdogo wa miaka minne,mama yake ni mtumishi na yeye akitoka asubuhi hurudi jioni au usiku maana mahali anapofanyia kazi ni mbali. Muda mwingi nikiwasiliana na mama yake kupitia simu ya mkononi huwa naomba kuongea nae (huyo binti yangu).

Juzi aliniuliza Baba unakuja lini? nikamjibu mwanangu nakuja nikimaliza kazi, akauliza utaniletea zawadi,nikamwambia ndio mwanangu. Nikamwambia kula maisha mwanangu akanijibu nakula maisha na maharage, hahahaha nikacheka mwanangu hajui maisha ni nini yeye anajua maisha ni chakula.

Hapa kwenye maisha ndio nikatafakari ukuaji wake utakuaje, mtoto Anaamka saa kumi na moja alifajiri anaandaliwa na binti wa kazi kwenda shule wakati mwingine wazazi wake bado hatujaamka. Najiuliza usalama wa mwanangu huwa ukoje?, Hizi basi zao(za wanafunzi) huwa zinakaguliwa?, huwa anaenda shule usingizi haujaisha mwanangu makuzi yake yatakuaje?, Nani anamuangalia mwanangu maaadili yake yatakuaje?, nyumbani akirudi Ana binti wa kazi usalama wake utakuaje /ukoje?maana Visa vya mabinti wa kazi kuua/kutesa watoto vimeongezeka, Nani anashinda nae anajifunza Nini ambacho sijui(Yuko umri wakujaribu mambo).

Nilifikilia mengi Kwamba siku binti yangu akikuwa atakuwa na sifa,tabia na siha njema ambazo ningependa awe nazo. Maana kwa kiasi kikubwa sishiriki katika ukuaji wake nachoweza ni kutoa pesa ya Ada maana ulezi Ni zaidi ya ada kwa mtoto.

Mtoto wangu sionani nae naishia kuongea nae kwenye simu Ila muda wa kumwagilia moyo(Pombe) napata. Je upendo kwa mwanangu ninaujenga kwenye zawadi tu ninazomuaidi kumpelekea?.

Sijawahi kukaa siku nzima na mwanangu Mara nyingi narudi amelala na anaondoka nimelala. Je mwanangu huyu asipoona upendo wangu ataweza kuwapenda watoto wake kweli(maana upendo hurithishwa)?.

Mara chache Sana nimekaa nae na nipale nilipopigiwa simu mtoto anaumwa au tatizo limetokea. Mtoto Kama anapitia matatizo shuleni na nyumbani atamuambia Nani Kama anashinda na binti wa kazi tu?.

Nasikia kesi za watoto kulawitiwa,kubakwa,kuteswa Hadi kuuwawa nimebubujikwa machozi. Nimetafakari yote hayo nikafilia nimfiche wapi binti yangu huyu Ili asikutane na hii Dunia iliyojaa mabaya kwa watoto kama unyanyasaji wa kingono, uteswaji,ubakaji.

Naanza kumuhofia yule mzee wa jirani ambaye amejenga mazoea na watoto wa kike na kuwaita wachumba, Nahofia mwanangu kwakuwa sishindi nae atakuwa anaitwa mchumba, Nahofia matendo mabaya kwa mwanangu.

Tabia mbaya ndio zimkuwa urithi kwa watoto wetu maana hatushiriki ipasavyo katika ukuaji wao, watoto wanajifunza tabia mbaya Kama wizi, uongo,kutoheshimu wakubwa kutukana n.k

Hii ni tafakuri,mtazamo au fikra ya kubuni nimewaza maisha ya Sasa tumekuwa busy na kusahau wanaotuhitaji zaidi.

Mambo ya kuzingatia kwa wazazi au walezi kwa watoto
  • Hakikisha una hakiki maudhui anayoangalia mwanao Kama Tamthilia, video za Muziki,katuni na filamu. Kuna filamu nyingi maudhui yamelenga watu wazima pia Kuna baadhi ya filamu zinakinzana na tamaduni zetu. Mfano filamu nyingi za magharibi na Amerika Zina maudhui ya Ngono na lugha chafu.
  • Kama simu janja yako Ina picha na video za utupu(pornography) Hakikisha mtoto wako hagusi, ikiwezekana funga na weka mbali ili isiwe rahisi kufikika. Dunia ya Sasa imekuwa ya utandawazi watoto wetu nao wanataka wajue tunacho angalia kwenye simu zetu na pia Wana vitu wanavyopenda Kama katuni na games. Ikiwezekana mtoto atafutiwe kifaa chake(simu/tablet) ili isiwe rahisi kushika simu yako.
  • Mzazi au mlezi fatilia maendeleo ya mtotohasa ya kielimu, Mtoto anapopewa kazi za nyumbani shiriki nae na muelekeze inapobidi. watoto ni rahisi kukata tamaa tuwatie moyo pale wanapopata ugumu hasa kwenye masomo yao. Safari ya Elimu ni ngumu iliyojaa miiba tusipowatia moyo watoto ni rahisi kukata tamaa.
  • Mfundishe mwanao stadi za kazi hasa kazi za mikono na zile zinazochochea ubunifu. Watoto wetu ndio vijana na wazee wa kesho tunapaswa kuhakikisha wanapata maarifa ya mambo mbalimbali Kama kazi za mikono na juzi tofauti tofauti kulingana na mazingira wanayoishi au mambo wanayoyapenda. Mfano Baba ni Fundi selemara au Mama ni Fundi wa kushona nguo Hakikisha mtoto anapata ule ujuzi wa msingi hii itamsaidia baadae pia itamfanya awe mbunifu zaidi.
  • Tuwawezeshe(support) kwenye mambo wanayo yapenda hasa sanaa na Michezo. Wazazi tusiwakitishe tamaa watoto wetu kwenye mambo Kama mpira wa miguu,mpira wa kikapu, Muziki na hata utayarishaji wa Muziki. Ukimkataza mtoto unaweza kuwa umewapoteza Diamond,alikiba,Nikki mbishi,Burna boy, Dr dre,Leo Messi, Christian Ronaldo, Edgar Davis, Selena william, au Aretha Franklin wa baadae.
  • Hakikisha mtoto anapata Chakura Bora, ili akue mwili na akili. Mzazi Hakikisha mtoto anakula matunda na mboga mboga pia apumguze matumizi ya vyakura na vinywaji venye sukari nyingi kwani vinasababisha magonjwa ya kisukari na unene.
  • Hakikisha mtoto anafanyiwa uchunguzi wa Afya ya mwili na akili Mara kwa Mara, hii itamsaidia kugundua magonjwa yanayochelewa kuonekana ili yaweze kupatiwa ufumbuzi kwa wakati.
  • Mfundishe mwanao tabia njema, pia mfundishe Maadili ya Dini na tamaduni anayoishi. Watoto wetu wanahitaji miongozo kutoka kwetu wazazi, tuwaelekeze katika njia nyoofu ili wawe mfano Bora katika jamii. Naamini hakuna mzazi anaependa mtoto wake awe kahaba,jambazi,kibaka, mwizi,tapeli n.k Ni furaha iliyo kuu mzazi kumuona mtoto anafanikiwa na kuja kuwa mtu anaye aminiwa na jamii yake.
  • Mzazi mfundishe mtoto wako kujiamini. Watoto walio wengi wana nidhamu ya woga na hii inawapunguzia kujiamini. Kutojiamini kwa watoto wetu kunawafanya iwe rahisi kurubunika, Dunia ya Sasa imejaa waharibifu Kama wanaopenda kufanya mapenzi na watoto(pedophile),wanaowachochea kufanya uovu(viongizi wa makundi Kama ya Panya road) n.k , Sasa mtoto akiwa anajiamini rahisi kukataa.
  • Pia, mzazi Jenga utamaduni wa kuongea na mwanao, hii itamfanya awe mtu Bora zaidi, itamfanya mtoto akuelezee shida/matatizo yake. Kwa jamii ya kiafrika ni nadra mzazi kujenga urafiki na mtoto hii inawaletea matatizo watoto wetu pale wanapohitaji miongozo na maelekezo yetu hasa kipindi Cha balehe.

Ombi mzazi au mlezi Tenga muda kwa ajiri ya mwanao

kama utavutiwa na makala hii naomba Kura yako
Sijasoma uzi kwanza nimesoma heading tu ngoja nikoment kwanza halafu ntarudi kusoma uzi[emoji41]
Ukweli mchungu ni kwamba tangu kabinti kakiwa kadogo kuna mijamaa inakamezea mate na wanasubiri kakue kidogo wakapige mb oo
 
Wabongo tumeiga maisha ya Wazungu, ila Wazungu hawaishi na Mahouse girl, wazungu hata kwenye TV twaona wanajishughulisha wenyewe...

Tuhame huko kwenye mahouse girl kama walezi wa watoto wetu, tujiwekee muda wa kazi na muda wa familia
 
Safi sana mleta mada, uzi una madini tupu. Big up.

Tuutie ndimu uzi huu kwa video hii kuntu:

"Ongea Na Mwanao"... Long live maalim Nash.

-Kaveli-

Hahaha......hivi zuzu alishatoka maandishi matatu?.

Mimi nimnazi Sana wa hip-hop, hopefully uko poa Kaveli long time haujaonekana jukwaani.
 
Sijasoma uzi kwanza nimesoma heading tu ngoja nikoment kwanza halafu ntarudi kusoma uzi[emoji41]
Ukweli mchungu ni kwamba tangu kabinti kakiwa kadogo kuna mijamaa inakamezea mate na wanasubiri kakue kidogo wakapige mb oo
Usisahau ku-like na ku-vote
 
Wabongo tumeiga maisha ya Wazungu, ila Wazungu hawaishi na Mahouse girl, wazungu hata kwenye TV twaona wanajishughulisha wenyewe...

Tuhame huko kwenye mahouse girl kama walezi wa watoto wetu, tujiwekee muda wa kazi na muda wa familia
Mkuu kwema....Awali ya yote huwa nawafatilia kwenye uzi wa yanayojiri Ukraine na mkuu figafiga, na kule jukwaa la sport kwenye uzi pendwa wa kubet.

Nirudi kwenye Mada, Watu wanakuwa busy kiasi kwamba watoto wanajilea na kuanza tabia mbaya bila wazazi kujua.

Tunaishi maisha ya "Kizungu" ambayo hata wenyewe hawayaishi. Ipo namna Kama Taifa lazima tufanye.
 
Asante
Katika suala la malezi
Mama hakikisha ajira/biashara yako inakupa nafasi na watoto
KateMiddleton Asante kwa Maoni yako, Wamama hasa single mom Hakikisha una muda wakuwa na watoto wako. Hata wale ambao Ni wanandoa hawana budi kugawana majukumu ili kuwa karibu na Familia. Usisahau ku-vote na ku-like.
 
Malezi ya pale nyumbani ni Mama
Baba ni by the way😅
 
Sijasoma uzi kwanza nimesoma heading tu ngoja nikoment kwanza halafu ntarudi kusoma uzi[emoji41]
Ukweli mchungu ni kwamba tangu kabinti kakiwa kadogo kuna mijamaa inakamezea mate na wanasubiri kakue kidogo wakapige mb oo
Kuna wale wanapenda kuita vitoto vidogo mchumba, Ni kuwa nao makini.
 
Hao ndo hawafai kabisa maana atajifanya kumzoea mtoto na kumuita mchumba anamletea pipi na biscuit then kifuatacho anaanza kuloweka utambi mdogo mdogo mpaka mnakuja kustukia mtoto keshakuzwa kabla ya muda
 
Mkuu Dunia imechafuka....Hadi viongizi wa Dini nao sio wakuwaachia watoto, refer kesi ya makasisi wa kikatoliki Papa Kila siku anawaombea msamaha.
 
Nikufiche wapi xxxx nikiangalia watoto wa jirani wao ndio hufanya kazi za uchuuzi kwa kutembeza karanga barabarani.
 
Likizo zimeisha, ni muda wa kujiandaa na ada na term mpya kwa wanafunzi.

Nafasivya malezi kwa sasa inarnda kuwa kwa walimu.
 
Hivi hawa watoto ambao wanajazana kwenye hizi bar/club za dar weekend ndio kusema wanajilea, maana inasikitisha
 
Habari ya kusikitisha
Screenshot_20220830-214403_1.jpg
 
Watoto walio na mahitaji maalumu tusiwafiche, wanahitaji huduma muhimu kama watoto wengine kama elimu na Afya.
 
Unaepita kwenye uzi huu usiache kuvote
 
Back
Top Bottom