Maalim,huyo jamaa lazima aelewe kuwa ni mara chache sana hutokea ukapenda na hapohapo na wewe ukapendwa(at first sight),lazima pia aelewe kuwa unapompenda mtu inabidi umuoneshe upendo wako ili naye akupende,nahii ndio sababu wadada wengi kabla ya kukubali kuwa na uhusiano na mtu basi atakuzungusha hata mwaka mzima na sio kwamba hakutaki ila tu anataka kujua unampenda kweli au la ili asijekujiingiza kwenye shimo akashindwa kutoka.Ushauri wangu kwa huyo jamaa asiwe mtu wa kukurupuka tu,eti leo kampenda binti kamfuata na kajibiwa sivyo anatoka na jibu kuwa ninapopenda sipendwi.Ajaribu kutulia wakati anapokuwa na binti anayempenda na awe mvumilivu kwa yote atakayojibiwa na aonyeshe upendo wakweli,maana hawa wapinzani wetu kuwaelewa ni vigumu kidogo.Na mara nyingi hupenda pale wanapokuwa wameoneshwa upendo,kwa hiyo avumilie ajipange upya na aache muda ujibu wasiwasi wake.