Nimpendae han'pendi....An'pendae simpendi!

Nimpendae han'pendi....An'pendae simpendi!

Maalim Jumar

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2010
Posts
1,259
Reaction score
118
Ndugu zangu members wa JF!
Hili nimefikishiwa ni tatizo lake huyo X...jamaa anahitaji msaada...ameenda kwa wataalam...wengi kati yao wakamwambia ati ana Jinn mahaba.
Nilimkatalia kwa uelewa wangu.
Sasa amesema kwa huyo anaempenda lakin hapendwi..ati yupo radhi akikubaliwa kwa gharama yeyote atatoa...maana jamaa anajiweza kipesa..ni mtu anae jituma katika mihangaiko ya kupata mkate wake..na huduma muhimu hapa jijini.
Itakua ana tatizo gani?
Tumsaidieje?
Naamini hili tatizo mijini hua ni kubwa kuliko vijijini.
Nimemuwakilisha....karibuni wakuu!
 
anasema anayo list book yake ...alipoona idadi ni kubwa ndipo akaanza kutafuta msaada vile ni taabu kwake..tena akiongea kama anataka kububujikwa machozi...yaani anatia huruma!
 
Wala hana tatizo!Mwambie ajaribu kwingine!
Ahsante kwa ushauri Lizzy.
Ntamwambia...japo sijui kama atanielewa...vile amenambia amejaribu sasa ni idadi kubwa kwake!
 
Ahsante kwa ushauri Lizzy.
Ntamwambia...japo sijui kama atanielewa...vile amenambia amejaribu sasa ni idadi kubwa kwake!
Kama kweli huyo anaemtaka hampendi aachane nae!Kumng'ang'ania haitasaidia chochote zaidi yakumpa msongo wa mawazo!Akae mbali nae...apunguze mawasiliano kama yapo...akwepe kukaa mwenyewe..kujichanganya inasaidia sana kupunguza mawazo!Pia itamsaidia kukutana na watu wapya...pengine atakae mpenda nae akampenda!
 
Akasome nyota kwa Sheikh Yahaya huyo
 
Akasome nyota kwa Sheikh Yahaya huyo
Labda hata huko amefika...ndio vile akaja kwangu. Nami kwa uwelewa wangu na imani yenu wana JF atapata utatuzi wake.
Anatia huruma ilhali hana kasoro kihivyo!
 
Kama kweli huyo anaemtaka hampendi aachane nae!Kumng'ang'ania haitasaidia chochote zaidi yakumpa msongo wa mawazo!Akae mbali nae...apunguze mawasiliano kama yapo...akwepe kukaa mwenyewe..kujichanganya inasaidia sana kupunguza mawazo!Pia itamsaidia kukutana na watu wapya...pengine atakae mpenda nae akampenda!
Yeye si mmoja ndie anaemhitaji...ni wengi ameisha wahitaji. Mambo ndio hayo hayo.
Kaka/baba wa watu au Dada/mama wa watu. Inamuumiza.
 
Mpende akupendae,asiyekupenda mng'ang'anie mpaka akupende.
 
Mpende akupendae,asiyekupenda mng'ang'anie mpaka akupende.

wengine hawapendeki kabisa, hata umuoneshe mapenzi ya namna gani utaishia kuumizwa moyo tu, cha msingi hapo aachane na habari za mapenzi kabisa
 
wengine hawapendeki kabisa, hata umuoneshe mapenzi ya namna gani utaishia kuumizwa moyo tu, cha msingi hapo aachane na habari za mapenzi kabisa
Niliwahi kukutana na mmoja wa warembo na hakuwa ananipenda lakini niling'ang'ania mpaka akalegeza kamba na mambo yakawa poa,tatizo tunataka mambo haraka haraka ndio maana tunaona hatupendwi.
 
Maalim,huyo jamaa lazima aelewe kuwa ni mara chache sana hutokea ukapenda na hapohapo na wewe ukapendwa(at first sight),lazima pia aelewe kuwa unapompenda mtu inabidi umuoneshe upendo wako ili naye akupende,nahii ndio sababu wadada wengi kabla ya kukubali kuwa na uhusiano na mtu basi atakuzungusha hata mwaka mzima na sio kwamba hakutaki ila tu anataka kujua unampenda kweli au la ili asijekujiingiza kwenye shimo akashindwa kutoka.Ushauri wangu kwa huyo jamaa asiwe mtu wa kukurupuka tu,eti leo kampenda binti kamfuata na kajibiwa sivyo anatoka na jibu kuwa ninapopenda sipendwi.Ajaribu kutulia wakati anapokuwa na binti anayempenda na awe mvumilivu kwa yote atakayojibiwa na aonyeshe upendo wakweli,maana hawa wapinzani wetu kuwaelewa ni vigumu kidogo.Na mara nyingi hupenda pale wanapokuwa wameoneshwa upendo,kwa hiyo avumilie ajipange upya na aache muda ujibu wasiwasi wake.
 
Ahsante Paka Mw**si.
Jamaa amenieleza mengi sana!
Yote nilijitahidi kumweleza...aksema anapokua amempenda basi anajitahidi kua kama FARA!
ANAKUA MWENYE SUBIRA,MPOLE PIA ANAKUA ANAKAA NAE KWA MIEZI ZAIDI YA MINANE.
Ila yeye anacholalamika katika uchunguzi wake...kwanini alipopenda hapendwi?
Na ataejitokeza kwake akampenda basi yeye anakua hampendi?
 
Back
Top Bottom