Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,828
- 3,579
1. Miaka yote zaidi ya 40 ya uwepo wa NIMR, wameongeza nini katika ufahamu wa mambo ya tiba Tanzania? Ni utafiti gani waliowahi kuufanya ukaleta tija katika kupunguza au kuondoa tatizo lolote la kiafya? Jibu ni zero.
2. Hivi kuna dawa yoyote sokoni (dawa ya maana yenye viwango stahiki, na siyo ile michanganyiko ya pilipili kichaa na tangawizi waliyoiga kutoka kwa waganga wa kienyeji) au vifaatiba hospitalini au maarifa mapya yoyote ya tiba yaliyowahi kugunduliwa na NIMR? Jibu ni hakuna.
3. Nina jamaa zangu nimesoma nao History na English pale Mlimani, eti nao wanafanya kazi NIMR wananiambia wanaitwa "Research Scientist". Hiki ni kituko! Scientist wa history, English, Kiswahili, sociology na Political Science anafanya nini kwenye MEDICAL research? Ingekuwa HEALTH research ningewaelewa kwa kuwa afya ni suala mtambuka lenye mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayoathiri afya, lakini medical research ni mambo ya maabara, madawa, mawodini huko wanakotibiwa wagonjwa, operations mpya mpya kama hizi za moyo na figo nk. Tunasikia huko Jakaya Kikwete institute, Benjamin Mkapa Hospital na hata MOI wakifanya innovations mpya mpya, lakini mchango wa NIMR kwenye hizi innovations uko wapi?
4. Mkurugenzi wa NIMR ni profesa wa Marine Biology. Hii ndiyo medical research? Hakuna medical researcher nchi hii mwenye sifa ya kuwa mkurugenzi wa NIMR? Sasa marine biologist na medical research wapi na wapi? Ndio chanzo cha kwenda kudesa michanganyiko ya waganga wa kienyeji na kutuambia ni dawa za korona!
5. Kwa ujumla NIMR ni kimeo, haina faida kwa nchi, ifutwe tu.