Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 21,237
- 31,811
Hivi kwenye bajeti yetu umewahi kusikia walau serikali imetenga bajeti kwajili ya tafiti mbalimbali?Exactly. Nimeona mahojiano kwenye TV na mkurugenzi mmojawapo (siyo mkurugenzi mkuu Prof Mgaya), akasema wanafanya research kwa kutegemea grants ambazo watoaji wa grants hizo ambao ni mataifa ya nje ndio wanaoamua research agenda. Kwa hiyo tuna taasisi ya utafiti wa tiba (ndiyo tafsiri ya institute of medical research, ingawa wenyewe wanaita taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu) ambayo haina uwezo wa kuendesha research agenda zake. Matokeo yake imejaza "scientists" wasiokuwa wa tiba kwenye ranks zake: sociologists, politicians, linguists, historians, marine biologists na wengine wa hivyo, eti hawa ndiyo waendeshe agenda za medical research! Hii siyo dharau?
Ndiyo maana tafiti zake ni kichefuchefu kitupu, hata sisi tuliosoma "ungwini" tunawashangaa.
Kwenye wizara husika umeshawahi kusikia walau wizara kutenga bajeti kwajili ya tafiti mbali mbali zinazohusiana na wizara yenyewe ?
Kama hatuna bajeti ya tafiti hizo taasisi nitafanya tafiti kwa fungu gani?