NIMR ni kimeo, haina faida kwa nchi, ifutwe tu

Hivi kwenye bajeti yetu umewahi kusikia walau serikali imetenga bajeti kwajili ya tafiti mbalimbali?

Kwenye wizara husika umeshawahi kusikia walau wizara kutenga bajeti kwajili ya tafiti mbali mbali zinazohusiana na wizara yenyewe ?

Kama hatuna bajeti ya tafiti hizo taasisi nitafanya tafiti kwa fungu gani?
 
Yesi ni kweli vyuo vya kati ndiyo vinavyopeform.Naliendele mtwara,TARI uyole na kwingineko. Lakini ukiangalia kwa kina utakuta kuna mkono wa mabeberu kwa nyuma yake umewezesha mafanikio.
Mbona NIMR hawafanikiwi kwa mkono huo huo wa mabeberu wakati ni PhD tupu zimejaa pale?
 
Wale jamaa hawako serious kabisa.

Ile kachumbari mtu yeyote anaweza kutengeneza badala ya kwenda kuinunua kwa hela kubwa namna ile.
Ndio maana fomula ilikuwa disclosed kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini Mkuu! Hizi za mabeberu fomula ni top secret!
 
Ha ha ha haaaa! Mbona mnawafokea sana wakuu? I guess wenyewe wapo wanayasoma haya wajirekebishe. Kiukweli kama wamejaa sociologists kwenye taasisi ya utafiti wa madawa hapo kuna tatizo kubwa sana
ITEGAMATWI ni kijiji fulani kipo huko wilayani Urambo vipi unauhusiano wowote na kijiji husika?
 
Mkuu kwemaaa?, una ushahidi na ubachokisema? NIMR kwa upande Wa suala ka kutokomeza malaria nchini naona kama wsmejitahidi sana,ni asilimia ndogo imebaki.
 
Walishawahi kuomba bajeti wakazinguliwa ? ... Kwa tatizo lilivyo critical nilitegemea kumuona mkrugenzi akilisemea kwenye media na wao wamefanya nin na wamefikia wap na changamoto ni ipi.....wao wamelala tuu wameenda Madagascar kukopy formula ya tormato sauce na kuja kutuwekea et covidol ......kama mkrugenzi mwenyewe kasomea marine biology haishangazi kuona ukimya kama huu......ni moja ya vitengo vibovu kuwahi kutokea nchi hii
 
Umesimuliwa ukakimbilia kuja kubandika bango humo kana kwamba una akili sana kumbe bure tu.

Kama huna uwezo wa kujua taaluma halisi za watu ni ngumu sana kwa ninyi wanasiasa uchwara kuelewa nini maana ya usalama wa nchi na raia wake. Ninaweza kuwa nataaluma yangu halisi lakini ili niweze kuingia mahali fulani ninasomea taaluma nyingine wezeshi kuingia ndicho kilichopo lakini wewe unatupigia kelele kama mtoto mdogo aliyezaliwa leo ambaye ni sharti aliye kuthibitisha ni mzima na ana afya ya kuhisi mazingira yanayomzunguka kwa muda huo sio rafiki.

Rekebisha tabia hiyo kubagaza wanataaluma. Kama ulisomea HGL, HGK, HGE nk lakini hukujiongeza kusomea vitu vingine usiwaonee nongwa wenzio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…