NIMR ni kimeo, haina faida kwa nchi, ifutwe tu

Tatzo la NIMR ni kutokukubali kuendana na wakati yani kwenye upigaji ndo wako vizuri hasa kwenya uendeshaji wa miradi ya malaria, kichocho, na matende hapo huwa ni kula hela tu, ila kwenye tafti ni blaa blaa tu
Hizo kazi za kuendesha miradi ya malaria, kichocho na matende zingeweza kufanywa na watu wa idara mojawapo pale wizara ya afya na kwenye halmashauri zetu, siyo na taasisi ya medical research. Hizo ni public health projects, na hazihitaji kuongozwa wala kusimamiwa na medical researchers, hizo hata watu waliosomea community development na sociology ndio kazi zao kupita kwenye jamii kuhimiza matumizi ya chandarua, matumizi ya choo bora nk. Tunaona hata huku mitaani watu wanaohimiza kwamba "Usichukulie Poa Nyumba ni Choo" ni akina Mrisho Mpoto na Shilole, wasanii wenye influence kwa hadhira.
Medical Researchers hawapaswi kuvamia kazi ambazo sio medical research. Wanapaswa wafanye tafiti za tiba walete majibu ya changamoto zilizoko katika tiba ya binadamu: dawa bora, vifaa tiba, mbinu bora za operesheni na mengine ya aina hiyo katika tiba.

Sasa hawa wenzetu huko NIMR baada ya kuona medical research imewashinda ndio tunawasikia kila siku wakiimba matende na mabusha na kugawa dawa za minyoo mashuleni. Dawa hizo zilitafitiwa zamani na kuthibitishwa ubora wake huko zilikotoka kwa mabeberu, hapa kwetu zimepata usajili na kuruhusiwa kutumika, eti NIMR wako busy kugawa dawa! Hiyo kazi hata ukimpa mwalimu wa shule ya msingi ukamwambia gawia kila mtoto kidonge kimoja anywe na glasi moja ya maji atashindwa?
 
Unamapepo wewe sio bure,
 
Hebu tuorodheshee tafiti ambazo NIMR imefanya na faida ambazo nchi imepata kwa tafiti hizo. Usilete madesa utaumbuka, watu wanayo majibu hapa.
Nimejaribu ku-search kwenye intene t nimekuta these achievements
•Contributed to efficacy data for reviewing National Antimalarial Drug Policy in mainland Tanzania (CQ to SP and SP to ALU), also for Zanzibar (CQ to AQ/AS)

•Provided data to support use of Albendazole / Ivermectin for global elimination of lymphatic filariasis and Onchocerciasis

•Pioneering data to show ITNs can reduce malaria morbidity
•Still responsible for 4 out of 8 sentinel sites for monitoring antimalarial efficacy
•Malaria vaccine trials, RTS,S /AS02 and MSP3.
•Capacity building through research activities
 
Wewe jiwe vipi? Kwani kozi zinazohusu afya ni udaktari na unesi tu? Hakuna kozi za IT mahususi kwa ajili ya afya,hujawahi kusikia kozi za business Administration katika masuala ya afya?
Haya mjibie mwenzako "anayejua vizuri Muhimbili" Unaweza kuwa msemaji wa hospitali kubwa kama Muhimbili bila kuwa na background ya masuala ya Afya?
Hilo ndilo suali la msingi huko kwingine mnarukia rukia tu.
Swali lingine, mtu wake aliyesoma mifugo atafafanya kazi kitengo gani Muhimbili?
Dogo ebu kua basi..we unadhani wanao lipa mshahara pale muhimbili ni madaktari..wanao endesha IT ni manesi..kua na akili hizi ni taasisi zinachukua watu wa taaluma mbalimbali ili kuwezesha utoaji wa huduma.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tatzo la NIMR ni kutokukubali kuendana na wakati yani kwenye upigaji ndo wako vizuri hasa kwenya uendeshaji wa miradi ya malaria, kichocho, na matende hapo huwa ni kula hela tu, ila kwenye tafti ni blaa blaa tu
Pale hamna kitu naona wahusika wameanza kuja kujitetea na kudefend humu ....
 
Hata jeshi, polisi na TISS ni taasisi, unaweza kuwa msemaji wa hizo taasisi kama wewe sio mmoja wao?
Dogo ebu kua basi..we unadhani wanao lipa mshahara pale muhimbili ni madaktari..wanao endesha IT ni manesi..kua na akili hizi ni taasisi zinachukua watu wa taaluma mbalimbali ili kuwezesha utoaji wa huduma.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nakumbuka mwaka flani tuliwapa NIMR pesa ili wakatafiti cases za cholera mtaani. It was more of an assessment na sio “research” as such. Professor ndio alitaka kulead hiyo assessment

Hii ndio NIMR yetu.
Pole sana mtaalam. Ni kimeo hiyo kitu inayoitwa NIMR.
Kama nchi tunahitaji kutafakari tena kama tunahitaji NIMR au la. Kama kweli tunahitaji taasisi inayofanya medical research, NIMR kwa hakika haifanyi kazi hiyo. Inahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa sana ya kimuundo ili iweze kuendana na dhima ya medical research.
Vinginevyo kwa kuwa medical research zinazofanyika Muhimbili, Bugando, Benjamin Mkapa, MOI na kwingineko zinatufaa na matokeo yake yanaonekana, basi tuimarishe tafiti katika taasisi hizo tuachane na kimeo cha NIMR.
 
Labda tukuulize wewe ipi kazi nzuri imefanywa na NIMR ? Mtoa mada ametoa data za kutosha kuonyesha NIMR ni wastage of money ..... Wewe unaita ameandika upumbavu ...basi thibitisha upumbavu wake la sivyo ukishindwa wewe ndo kilaza wa kiwango cha Tarmac road..et intelligence, intelligence gani hyo taasis nying duniani za tafiti tiba zina outbreak news namna zinavyokabiliana na Korona kutafta chanjo , NIMRI wako kimya et intelligence ..huu ujinga sjui unatokea wap hii nchi
 
Wapi nimesema kwamba wote wanoafanya kazi Muhimbili lazima wawe wamesoma medical?! Huna hoja kilichobaki unalazimisha kusema kitu ambacho huwezi kukithibitisha.
Nimekuuliza msemaji wa hospitali nyeti kama ya Muhimbili inawezekanaje akawa mtu asiye na background kwenye masuala ya AFYA!
Mpaka sasa hujajibu umebaki kuruka ruka tu kama maharage yanayochemshwa kwenye sufuria na madai ya kishamba kwamba unaijua Muhimbili yote na TISS wote.Jibu hoja zangu, acha kutishia nyau watu wazima.
 
Naona umekuja kimipasho. Funguka zaidi.
Katika porojo zote hizi ulizoandika, umejibu hoja ipi?
Umezidi kuthibitisha kuwa NIMR haina tija. Kazi kulamba ruzuku tu, hakuna suluhisho lolote la changamoto za tiba mliloleta tangu hii NIMR ianzishwe hadi leo, mnarithishana vizazi vya wapigaji tu
 
kitu kipo ila hakitoshelezi na kuna sababu kwanini hakitoshelezi
Sababu gani ?? Lack of fund? Yaan mnakaa kimya mpak wananchi tuanze kuchunguza chunguza et kuna sababu ..aiseee Raisi anatakiwa ashushe nyundo Kali Sana hapo NIMRI to fu-ck them .....
 

Mkuu....SUA wanajitahidi kidogo!
 
Ni kweli mkuu lakini ndo kichaka chao cha kupigia hela tena kwenye hizo project huwa wana mpaka watu wao wameisha wapanga, kwenye suala la utafiti ni changamoto ndo maana unaona hata madawa na vifaa tiba vingi tunategemea kutoka nchi za nje
 


Acha kuzunguka mkuu, sio wewe. Uliyesema hakuna mtu anayefanyakazi muhimbili bila kuwa na background ya afya?! Huu ni uongo, wako wengi tu hawana background yoyote kwenye medical, nimekuwa nafanyakazi mradi wenye mahusiano na muhimbili kwa zaidi ya miaka 5 , nimeingia pale almost kila week mara 2 au tatu randomly,

Sijui kiwango chako cha elimu na ufahamu , japo Nina doubtful nacho, wapi nimesema naijua muhimbili yote na tiss yote?! Mbona unaanza kuleta maneno yakwenye taarabu. Wewe ni mshamba huna ukijuacho ni taburasala.
 
NIMR ilikuwepo!! itakuwepo, ruzuku italambwa sana utakake!!usitake!! vimba pasuka!! wewe ndo unapasha kitu ambacho hukijui!
Narudia haitakufa ukiona imekufa ipo kivingine! siyo ruzuku ya Pesa ya Madafu ile!!! uliza ujibiwe!!
 
Sababu gani ?? Lack of fund? Yaan mnakaa kimya mpak wananchi tuanze kuchunguza chunguza et kuna sababu ..aiseee Raisi anatakiwa ashushe nyundo Kali Sana hapo NIMRI to fu-ck them .....
for your information siko NIMR, ila nasema kinachojadiliwa hapa. Nani kasema lack of funds? inaelekea una ubaya na NIMR... wewe ni kiumbe mdogo kuathiri NIMR. Nenda mabibo uone wanachokifanya, Nenda NIMR makao makuu kaone wanachokifanya, tembelea centres zao uone wanachokifanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…