Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

Mambo haya ya akina Mkono ni dalili mbaya kwa nchi yetu; tumo njiani kuelekea kwenye machafuko makubwa sana kama tutaendelea katika njia hii.

wenyewe wanasema "you haven't seen nothing yet"!

Mkjj na wengineo huko majuu, na hata hapa Bongo wenye kujua tunaomba mtutolee mifano kadhaa mliyowahi kuiona huko ya wanasiasa kuwa wafanya biashara wakati huo huo wakiwa katika shughuli za siasa.

Mifano ipo mingi tu.. they all ended up in jails!

Katika Tanzania suala la maadili halipo, wao wanareason kuwa kama si kinyume cha sheria basi twaweza kufanya. Wakati wenzetu huku hawaangalii sheria tu kwenye vitabu bali pia maadili ya kazi au fani husika. Lakini wenzetu wamefikia kuandika sheria kuhusu maadili hayo.

Sasa kama alivyofanyaga Msekwa na wengine, kwa vile Sheria haikatazi wao kuwa wajumbe wa bodi au Waziri wa Madini hakatazwi kufungua kampuni ya uchimbaji madini akiwa madarakani basi wao wanafanya.. !

Ndio maana sheria siyo tu zinasema nini kifanywe, bali pia zinakataza nini kisifanywe. Kwa hizi za kwetu nyingi ni za hilo la kwanza wakati hilo la pili linawatisha utadhani mizimu ya "watu wa kale"...
 
If no one has never intoduced such a bill then that's a shame. ....but then again this is an African country. What do you expect?....not much!!!!

Yes, it is. In Africa what matters is a leader's wisdom rather than the law, which is why change in leadership means a total change in the citizen's way of life. Again, bills are introduced by and at the pleasure of the government.

Our MPs are there to debate (or rather to endorse or just to have a look!) what the government presents. That is why some of us will never cheer at change on few faces on the government. We shall smile when an overhaul of the system happens, probably this happens during our lifetime!
 
Mkjj:
Ule upuuzi wa Azimio la Arusha haupo tena; kwa hiyo hatuna mipaka. Watu watachoka na haya haraka sana. Tusubiri kidogo.
 
Kwanza nashuru mjadala umekuwa objective...and this is what I always like!

Haya ndio yaliojiri.

1. Balali au mtu mwingine yeyote ana haki ya kutetewa, kusikilizwa etc.

2. Law firm yoyote ina haki ya kuchukua mteja yeyote mwenye haki ya kutetewa... and that is their business.

3. Conflict of interest, Mtunga sheria anapokuwa wakili etc...

4. Nchi isiyokuwa na maadili na mfumo wa kuongoza mambo ethics, policy and legal framework... instead depending on leader wisdom to lead and to make decision on critical nation issues.

5. Ethics za wanasheria hakuna kutangaza biashara, same to hospital/medicine etc,,,

Ahsantani... kwa maelimu yenu!!!
 
[/b]

wewe kweli KASHESHE!
Sasa huo unazi unatoka wapi tena wakati watu wanatoa mawazo yao?
Sual hapa sio right to legal representataion ya Balali wala right to work ya wakili Mkono; suala ninaliliona mimi ni hili
1. Mkono mwenyewe ni mtuhumiwa wa the same case..tangu lini mtuhumiwa mmoja akamtetea mwenzie kama wakili? labda tubadili kwanza sheria

2. Mkono ni mwanasiasa ndani ya chama tawala. Ikiwa raisi wa nchi amemuondoa kazini kiongozi wa ngazi za juu kwa tuhuma nzito za ufisadi; je, unafikiri ni sahahi kwa kiongozi mwingine wa serikali hiyohiyo kusimama mahakamani kumtetea? mimi nafikiri kufanya hivyo ni kuidhalilisha raisi ambaye yeye Mkono ameapa kumheshimu na kumtii yeye kama Mbunge.

3. Kaulizwa?
Kama yeye ni wakili, asijitangazie kuwa yuko tayari kumtetea mtuhumiwa; why, every other lawyer in the world is ready and willing if approached with a good case and fee; kwanini anajieleza; he may be jumping the gun here for good many reason

4. Kwanini Mkono ndiye awe mtetezi wa watuhumiwa ambao wananchi wote wa Tanzania wana interest na kuona wanatiwa hatiani..bado kumbukumbu zetu za kesi ya Ditto ziko fresh; WHY HIM? Is this a syndicate of some sort; where the big boy says ;let me do this to cool their steam off but i will find you a good lawyer friend of mine to get you out? What Is this game?

5. Mkono + the other guys implicated in this dirty scandal are moving freely simply because the powers that be decided to keep the dirty report to themselves; but worse still; they decided to limit the terms of reference of those who did the auditing. Hii amount inayopigiwa kelele hapa is but a peanut compared to what is actually taken; What is Mkono's share in that? nani hajui kuwa jambazi mwenye pesa ni vigumu kumfunga? tena kwenye hii nchi ambayo majaji wanapigiwa simu na kupigia wenzao wanaposoma hukumu? nani hajui role ya viongozi waliobaki na washirika wao amabao walitajwa kwenye ile mafioso tree iliyotolewa hapa JF na kufika bungeni; so, WHO IS PAYING WHO TO DEFEND WHO?

My conclusion: Mkono anawakilisha kile walichopanga hata kabla ripoti haijatolewa. Tena sitashangaa kama iko kamati inawasoma maoni yenu ili kupima joto kabla hawajaja na The Way Forward
Tena nawapongeza wale wananchi waliojichukulia sheria mkononi na kujigawia hayo mashamba; it goes to show that wananchi wameshoshwa na the whole legal process which is full of political pressure and is suffering from rushwaism

Mkono's statement, if we may call it that, is evidence of how stupid our leaders and their fisadi group think Tanzanians are.
They should tune their TV channels to Kenyan side to get a glimpse of a poor man's expression of hatred to the ruling powers
Wasicheze na akili za watu!

na kwa mtizamo huo hapo juu.....ndio wabunge wanatakiwa kutunga sheria za kubana ili hawa watu wasituchezee.....halafu sheria yenyewe ni rahisi tu, maadili ya viongozi and conflict of interest....just refer Azimio la Arusha rekebisha kidogo....weka muswada bungeni.

Kasheshe,
Ukiangalia vema mada zilizopita....pale ambapo viongozi wetu wamefanya vema walipewa credit zao.............and not necessarily aliyetoa pongezi au aliyeona awe FD...........pengine naye hakuiona hiyo mada kama wewe vile ambavyo hukuziona sehemu alizopongezwa............kibaya hapa ni kuwa wanafunikwa na mabaya ambayo ni mengi kuliko mazuri wayafanyayo!!!!

EL alipongezwa kwa
1.Juhudi zake kwa mradi wa maji toka lake Victoria
2. hiyo yako ya City Water na DAWASA
3. Kutembelea Bandari na kuona matatizo na kujaribu kuyatafutia ufumbuzi nk nk nk nk
 
Kwanza nashuru mjadala umekuwa objective...and this is what I always like!

Haya ndio yaliojiri.

1. Balali au mtu mwingine yeyote ana haki ya kutetewa, kusikilizwa etc.

2. Law firm yoyote ina haki ya kuchukua mteja yeyote mwenye haki ya kutetewa... and that is their business.

3. Conflict of interest, Mtunga sheria anapokuwa wakili etc...

4. Nchi isiyokuwa na maadili na mfumo wa kuongoza mambo ethics, policy and legal framework... instead depending on leader wisdom to lead and to make decision on critical nation issues.

5. Ethics za wanasheria hakuna kutangaza biashara, same to hospital/medicine etc,,,

Ahsantani... kwa maelimu yenu!!!

Good summary!!
 
Tulilipigia kelele hili kwenye mada ya Ditopile pale ambapo Mkono alikuwa ni wakili wake wakati yeye ni mtunga sheria.. something is very wrong..

Hatusemi kuwa Wanasheria wasiwe wabunge au wabunge wasiwe wanasheria, tunasema not at the same time... Mkono akitaka kuchukua kesi ya kuitetea, ajivue Ubunge kwanza na arudi uraiani.

Kwanini tunawakataza Polisi na wanajeshi kuwa wanasiasa at the same time? Which brings me to kesi ya Jaji Mkuu, kwanini Jaji Mkuu aendelee kuwa Brigedia Jenerali wa JWTZ? au ameshastaafu?

Hivi majuzi wakati wanachagua mkuu mmojawapo wa Intelligence services zao hapa US ambaye ni mwanajeshi mjadala mkubwa ulikuwa yeye atavaa uniform gani? ya Pentagon au ya uraiani.

Mwishoni waliona asivae magwanda yake ili asije kuonekana mtiifu kwa Pentagon na siyo kwa wakuu wa kiraia.

Sikumbuki kama ilibidi atoke Jeshini au kutovaa uniform tu..
 
Tulilipigia kelele hili kwenye mada ya Ditopile pale ambapo Mkono alikuwa ni wakili wake wakati yeye ni mtunga sheria.. something is very wrong..

Hatusemi kuwa Wanasheria wasiwe wabunge au wabunge wasiwe wanasheria, tunasema not at the same time... Mkono akitaka kuchukua kesi ya kuitetea, ajivue Ubunge kwanza na arudi uraiani.

Yes, lakini kwa mujibu wa sheria au busara? i) Kama ni busara hizo hatunazo kwa hiyo count out! ii) Hakuna sheria inayowazuia, so sheria count out! iii) Wapendekeza sheria bungeni ni haohao jamaa wa serikali ambao hizi sheria zilizopo au zisizokuwepo zinawasaidia, so hawatatunga ingine ili wajiminye. iv) Conclusion, nothing will happen, Mkono atamtetea Balali kama atataka kama alivyofanyikisha Dito kukaa nje mpaka watakapoamua au mpaka watanzania watakaposahau (ukizingatia kuwa watanzania sio wagumu kusahau);

JF tutaendelea kupiga kelele, 2010 itafika tutachagua CCM kwa kisingizio kuwa zimwi likujualo, wapinzani hawajawa tayari, hawana sera, na visingizio vingine kibao! JK atatoa hotuba ingine nzuri pale bungeni na mihadi na masafari yataendelea hadi 2015. Mwathirika: Tanzania na watanzania.

Kuwa na uchungu katika ile nchi inahitajika uwe na moyo wa jiwe!
 
Kwenye ile dossier ya Slaa nakumbuka Anna Muganda akitajwa kama mmoja wa wakurugenzi wa Meremeta. Mwanakijiji unaweza kujua kama kamati ya Mark Bomani imekwisha tembelea mgodi wa Buhemba ? Mgodi huu uko at the center of the saga.
 
Huo mfano wa Marekani una afadhali kidogo kwa sababu wao walikuwa wanajadili magwanda. Hii ya Mkono kuwa mbunge mtunga sheria na wakili kwa wakati mmoja haiingii akilini kabisa...it is not complicated logarithm...the conflict of interest is so obvious to obscene levels. Mbona kina Clinton, Gonzalez, Obama etc...hawa-pactise sheria bana?

Ndio maana nimesema only in Africa unakuta migongano ya kimslahi kama hii...yaani ujinga mtupu...actually ni beyond ujinga! Where is the common sense?
 
Huo mfano wa Marekani una afadhali kidogo kwa sababu wao walikuwa wanajadili magwanda. Hii ya Mkono kuwa mbunge mtunga sheria na wakili kwa wakati mmoja haiingii akilini kabisa...it is not complicated logarithm...the conflict of interest is so obvious to obscene levels. Mbona kina Clinton, Gonzalez, Obama etc...hawa-pactise sheria bana? Ndio maana nimesema only in Africa unakuta migongano ya kimslahi kama hii...yaani ujinga mtupu...actually ni beyond ujinga! Where is the common sense?


acha kabisa, we have become more stupidy than stupidity itself!
 
Mimi nadhani tunasukumbwa na maxim isemayo "more positions more ulaji" bila kujali positions hizo ni zipi? Ndiyo maana sasa naelewa vizuri kwanini Azimio la Arusha lilizikwa maana lingekuwa hai... kuna watu wangekuwa wanalia kila siku..
 
Kuna mtu anajua kwa nini Mkonoi alikataa kujibu hoja za wapinzania hata kama zilitolewa kisiasa lakini leo ndiyo haya tunayaona.

Je kwa nini alishindwa kwenda Mahakamani maana alitajwa yeye binafasi . Ndiyo mchezo wao hawa jamaa ?
 
Nchi ni lazima ifuate sheria. Na Mkono anachofanya ni kufuata haki zake za katiba (period).

Hata kama harakati mnazozifanya hapa ni nzuri na zina manufaa kwa nchi, juhudi hizo zisivuke mipaka ya kuzuia haki za watu za kutafuta ulaji.
 
Nyani,
Tanzania hakuna kitu kama conflict of interest. Unakumbuka former spika aliwahi kuwa kwenye bodi ya Vodacom. Naibu waziri wa madini aliwahi kuwa mwanasheria wa kampuni za wawekezaji wa madini.
 
Tena naambiwa kwamba Tanzania hakuna maadili . Wanasema ukiwa mchapakazi hata kama unalala na mke wa waziri mwenzio utaendelea na cheo chako cha uwaziri ili mradi una uwezo na kazi na si maadili kaa wazungu .
 
Hakuna cha kushangaza hapa, Ballali ndiye alikujaza mapesa ya kifisadi shilingi bilioni 8 kwa kazi ambayo haijulikani. Hatujui mgawo wenu ulikuwaje katika ufisadi huo.
 
Jamani sii huyu huyu anayesema kwa majisifu kuwa yeye ni Ghali...huduma zake hazitoki buree kiasi kwamba gharama zake zinalingana ama zimezidi zile za mawakili wa OJ...
 
Huyo MUKONO ni mbunge wa Musoma Vijijini.Asante. Mimi na Familia yangu na ukoo wangu wote KATU hatutofanya kosa tena kumpa kura fisadi huyu.NITAPIGA kampeni za ukoo bila kuombwa na mtu kuondoa FISADI hili.

Musoma-majita watu wanashindia maembe kwa mlo,shuleni wanafunzi wanasomea chini ya miti kama Bulinga s/m,Kurugongo,chimati,kwikerege nk leo huyu mbunge badala atetee hela yetu irudishwe ili tupate japo hela ya madarasa jimboni kwake yeye anatetea ujinga huu.

Ni haki sawa ya kila mtu kutetewa ila kwa ili angekaa pembeni.Mukono zingatia kuwa kushitakiwa huko kwa Balali kutatokana na Uchunguzi wa kina wa WATAALAMU kuhusu saga ya BoT uliompelekea rais kumfukuza kazi huyo fisadi mwenzio.Sasa wewe ofisa wa serikali tena mbunge wangu tena wa CCM ambaye mwenyekiti wako katoa maamuzi wewe unapingana ane???

Ngoja.Tutaonana wakati wa uchaguzi.Hakiya Mungu.
Hii Hii iii Machozi.uwiiiiii kamasi
 
Majita
Niweke sawa . Majuzi nimepita pale Magorombe , Busegwe na maeneo kadhaa nimekuta kachonga barabara nakujenga shule ua chief nani sijui . Kapendelea wazanaki na nyie kuwaacha ama lile ni eneo gani?

Maana watu wa jimbo lake wanamwita Mbunge wa Mkoa wewe unasemaje ? Nimepita jimboni kwake na hata nikalala pale Busegwe Parokia ya Zanaki pale Magorombe nikiwa naangalia maendeleo yake kumbe ni nusu tu ?
 
Back
Top Bottom