Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Mambo haya ya akina Mkono ni dalili mbaya kwa nchi yetu; tumo njiani kuelekea kwenye machafuko makubwa sana kama tutaendelea katika njia hii.
wenyewe wanasema "you haven't seen nothing yet"!
Mkjj na wengineo huko majuu, na hata hapa Bongo wenye kujua tunaomba mtutolee mifano kadhaa mliyowahi kuiona huko ya wanasiasa kuwa wafanya biashara wakati huo huo wakiwa katika shughuli za siasa.
Mifano ipo mingi tu.. they all ended up in jails!
Katika Tanzania suala la maadili halipo, wao wanareason kuwa kama si kinyume cha sheria basi twaweza kufanya. Wakati wenzetu huku hawaangalii sheria tu kwenye vitabu bali pia maadili ya kazi au fani husika. Lakini wenzetu wamefikia kuandika sheria kuhusu maadili hayo.
Sasa kama alivyofanyaga Msekwa na wengine, kwa vile Sheria haikatazi wao kuwa wajumbe wa bodi au Waziri wa Madini hakatazwi kufungua kampuni ya uchimbaji madini akiwa madarakani basi wao wanafanya.. !
Ndio maana sheria siyo tu zinasema nini kifanywe, bali pia zinakataza nini kisifanywe. Kwa hizi za kwetu nyingi ni za hilo la kwanza wakati hilo la pili linawatisha utadhani mizimu ya "watu wa kale"...