Sawa ila nadhani kwa upande wa kurudia, itakua ngumu kwa sababu hata mwenendo wake ulikua wa kusua sua tangu madarasa ya chini.Mkuu mitihani ya bongo ni mitihani kweli kwenye matokeo pia. Kama anataka kusoma asikate tamaa apige hizo paper za kurudia mtihani hata masomo machache achague atembee nayo Mimi nawakumbuka jamaa zangu kibao waliletewa matokeo Kama hayo wakipokuja kurudia walifanya maajabu na wengine sasa hivi wameshika vitengo vikubwa ila mwanzo walikatishwa ndoto zao na NECTA.
Yupo mmoja alipiga paper zote harafu akapata divion one toka zero mpaka akapangiwa shule kwenda advance ya serikali wakati paper alipiga private na akaamua kumaliza huko huko private akaondoka na One tena advance ya EGM, waliopata zero pcb na kuja kusoma EGM wengi tuu shida wadogo yakiwatokea matatizo kidogo tuu na walezi wanakata tamaa maisha ni Vita hakuna kurudi nyuma kivyovyote vile.
Nimpeleke akachukue ujuzi gani mkuu? Mnaweza nishauri na hapo.Pole kwa bwana mdogo wako kwa ufaulu huo,maisha lazima yasonge.Mpeleke vyuo vya veta apate ujunzi ambao anaupenda,ili aweze kujitegemea.
Jaribu kumchunguza na kumdadisi anapendelea nini zaidi,ndio usimame naye kwenye anachokipendea.Kamwe usimlazimishe kwenye fani ambayo hajaonyesha interest.Nimpeleke akachukue ujuzi gani mkuu?, unaweza nishauri na hapo
aaah embu kaa nae chini na wewe mbona unataka kutafuniwa kila kitu. Ujuzi anatakiwa aseme yeye kama ni ufundi nguo au fundi Umeme. Hujasema ni jinsia gani we kaa nae na umsikilize, naweza kwambia ufundi nguo wakati yeye anapenda kuwa fundi mjenzi au fundi seremalaNimpeleke akachukue ujuzi gani mkuu?, unaweza nishauri na hapo
Kuliko VETA, bora aende gereji akapigwe spanner za manyoka wanazopigwa. Ndio atapata akili. Huyo utasikia anataka kujifunza magari tu. Wote failure wa division 0 wanapenda vitu vizuri ila hawataki kuvifanyia kazi.Mpeleke kwenye ufundi mkuu,kureseat niwachache wanatoboa, then kwa hali ya nchi ilivyo akiwa na ujuzi wowote atatoboa kuliko areseat. Ni mawazo yangu tu.
1. Kama upo maeneo mazuri kwa kilimo. Mtafutie shamba akalimeHeshima kwenu wakuu.
Kama kichwa hapo juu kinavyojieleza. Nina mdogo wangu alifanya pepa ya form 4 mwaka jana (2020) lakini matokeo yametoka amepata Division Zero(0)
Nawezaje kumsaidia huyu mdogo wangu.
Ahsanteni.
Pole sana mkuuHeshima kwenu wakuu.
Kama kichwa hapo juu kinavyojieleza. Nina mdogo wangu alifanya pepa ya form 4 mwaka jana (2020) lakini matokeo yametoka amepata Division Zero(0)
Nawezaje kumsaidia huyu mdogo wangu.
Ahsanteni.