Nimsaidiaje mhitimu wa kidato cha 4 alayepata Division Zero(0)?

Nimsaidiaje mhitimu wa kidato cha 4 alayepata Division Zero(0)?

commm

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2019
Posts
1,709
Reaction score
1,963
Heshima kwenu wakuu.

Kama kichwa hapo juu kinavyojieleza. Nina mdogo wangu alifanya pepa ya form 4 mwaka jana (2020) lakini matokeo yametoka amepata Division Zero(0)

Nawezaje kumsaidia huyu mdogo wangu.

Ahsanteni.
 
Mkuu mitihani ya bongo ni mitihani kweli kwenye matokeo pia. Kama anataka kusoma asikate tamaa apige hizo paper za kurudia mtihani hata masomo machache achague atembee nayo Mimi nawakumbuka jamaa zangu kibao waliletewa matokeo Kama hayo wakipokuja kurudia walifanya maajabu na wengine sasa hivi wameshika vitengo vikubwa ila mwanzo walikatishwa ndoto zao na NECTA.

Yupo mmoja alipiga paper zote harafu akapata divion one toka zero mpaka akapangiwa shule kwenda advance ya serikali wakati paper alipiga private na akaamua kumaliza huko huko private akaondoka na One tena advance ya EGM, waliopata zero pcb na kuja kusoma EGM wengi tuu shida wadogo yakiwatokea matatizo kidogo tuu na walezi wanakata tamaa maisha ni Vita hakuna kurudi nyuma kivyovyote vile.
 
Sawa ila nadhani kwa upande wa kurudia, itakua ngumu kwa sababu hata mwenendo wake ulikua wa kusua sua tangu madarasa ya chini.
 
Pole kwa bwana mdogo wako kwa ufaulu huo,maisha lazima yasonge.Mpeleke vyuo vya veta apate ujunzi ambao anaupenda,ili aweze kujitegemea.
Nimpeleke akachukue ujuzi gani mkuu? Mnaweza nishauri na hapo.
 
Kuna vyuo vya serikali vya fani anaweza kwenda kubwa kujua utashi wake kwenye hilo.
 
Nimpeleke akachukue ujuzi gani mkuu?, unaweza nishauri na hapo
aaah embu kaa nae chini na wewe mbona unataka kutafuniwa kila kitu. Ujuzi anatakiwa aseme yeye kama ni ufundi nguo au fundi Umeme. Hujasema ni jinsia gani we kaa nae na umsikilize, naweza kwambia ufundi nguo wakati yeye anapenda kuwa fundi mjenzi au fundi seremala
 
Mpeleke kwenye ufundi mkuu, ku-reseat niwachache wanatoboa, then kwa hali ya nchi ilivyo akiwa na ujuzi wowote atatoboa kuliko areseat. Ni mawazo yangu tu
 
Kwa nini mnabeba sana watu? Na ww ulipata division 0? Kama haukupata, ni kwa nini yeye apate?

Inabidi watu muwe wakali. Ni uzembe tu na kutoweka juhudi. Mwambie sasa basi. HAUTAMSAIDIA TENA. AENDE KIJIJINI AKAKAE HUKO.

Akae huko hadi apate akili. Sasa hivi hata hajui anataka nini. Utampeleka VETA kupoteza hela zaidi na juhudi zako

Achana naye kwanza. Mpe hata miaka mitatu akue kiakili. Ajue maisha sio lele mama. Atambue akipata msaada asiufanyie mzaha. Atambue ni ninianakitaka maishani. Atafanya fanya kazi kuna moja ataipenda. Akikua kiakili ndio umsaidie
 
Mpeleke kwenye ufundi mkuu,kureseat niwachache wanatoboa, then kwa hali ya nchi ilivyo akiwa na ujuzi wowote atatoboa kuliko areseat. Ni mawazo yangu tu.
Kuliko VETA, bora aende gereji akapigwe spanner za manyoka wanazopigwa. Ndio atapata akili. Huyo utasikia anataka kujifunza magari tu. Wote failure wa division 0 wanapenda vitu vizuri ila hawataki kuvifanyia kazi.
 
Heshima kwenu wakuu.

Kama kichwa hapo juu kinavyojieleza. Nina mdogo wangu alifanya pepa ya form 4 mwaka jana (2020) lakini matokeo yametoka amepata Division Zero(0)

Nawezaje kumsaidia huyu mdogo wangu.

Ahsanteni.
1. Kama upo maeneo mazuri kwa kilimo. Mtafutie shamba akalime
2. Mpeleke VETA akajifunze ufundi aweze kujiajiri. Ufundi kama uselemala au ujenzi kwa kijana wa kiume na ushonaji au upishi kwa kijana wa kike unampa nafasi nzuri ya kujiajiri.
Ushauri wangu ni huo
 
Heshima kwenu wakuu.

Kama kichwa hapo juu kinavyojieleza. Nina mdogo wangu alifanya pepa ya form 4 mwaka jana (2020) lakini matokeo yametoka amepata Division Zero(0)

Nawezaje kumsaidia huyu mdogo wangu.

Ahsanteni.
Pole sana mkuu

Kaa naye chini umsikie mawazo na mipango yake. Kisha umpe mwongozo na msaada afanikishe ndoto yake.

Ilisemwa kufeli Masomo sio kufeli Maisha. Kikubwa ni support toka kwa wanaokupenda.
 
Back
Top Bottom