Nimsaidieje kisaikolojia atoke kwenye hii hali?

Nimsaidieje kisaikolojia atoke kwenye hii hali?

Umeshamuita mchepuko ajabu unataka umpe msaada wa kisaikolojia, kwani kabla ya kutoka nae mliokotana wapi?

Mwanamke umekutana nae barabarani akiwa na tabia zake, unataka umbadilshe is it possible?
 
Umeshamuita mchepuko ajabu unataka umpe msaada wa kisaikolojia, kwani kabla ya kutoka nae mliokotana wapi?

Mwanamke umekutana nae barabarani akiwa na tabia zake, unataka umbadilshe is it possible?
Najua nikikaa kimya, itamtesa sana
 
Wakuu habari?

Jana mida ya saa tatu usiku, niliamua kutoka na mpenzi wangu (mchepuko) na kwenda naye katika kiwanja kimoja angalau kujiburudisha pamoja na kupunguza msongo wa mawazo ya hapa duniani.

Tukiwa kwenye hicho kiwanja, tulikula, kunywa pamoja na kucheza mziki; ilipofika saa tisa na nusu usiku tuliamua kurudi nyumbani kwa sababu tulikuwa tumechoka sana pamoja na kulewa.

Baada ya kufika nyumbani na kujisachi kwenye mifuko yangu ya koti, nikagundua kuna kiasi fulani kimebaki na sijakitumia. Nikazihesabu na baada ya kujiridhisha nikaziweka kabatini.

Mwenzangu akajua labda nilikuwa nimelewa na sina kumbukumbu yoyote; sasa leo jioni akawa anajiandaa ili aweze kuondoka, ikanibidi niende kabatini ili niweze kumpatia chochote.

Ile nafika tu, nikakuta salio liko pungufu; ndipo nilipoanza kuhoji, akawa mpole kiasi na kuanza kulalamika hawezi kuchukua chochote bila kuniomba. Mbaya zaidi nikawa namtajia kiasi halisi ya fedha zilizokuwepo, na kumthibitishia sikupoteza kumbukumbu.

Nikawa kidogo mkali, na nikasema sipendi kuwa kwenye mahusiano na mtu mdokozi; ndipo nikaamua kutoka nje ili nimuachie nafasi apumue.

Ile nimekaa nje kama dakika tano hivi, akaniita na kuniambia, ''hela zako ni hizi hapa nimezikuta hapa chini, na huwa sipendi mimi kuitwa mwizi''

Nikamwambia abaki nazo tu, kwa sababu nilishajua zimepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Baada ya hapo akawa mkimya na kununa, kuongea hataki; mpaka jamaa wa boda akaja kumchukua na akaondoka bila ata kuniaga.

Nahisi atakuwa ameona aibu na nafsi inamsuta kwa alichokifanya,ingawa mimi nimemsamee na sijamtuhumu kuwa yeye ni mdokozi; mbaya zaidi ana ujauzi wangu.

Najua hii hali itamtesa kisaikolojia, baada ya kugundulika yeye ni mdokozi.

Sasa wakuu, nimsaidieje kisaikolojia atoke kwenye hii hali?​
UZINZI NI ZAIDI YA DHAMBI...DHAMBI UIFANYAYO JUU YA MWILI WAKO.

UZINZI NI LAANA...UNASUMBUA FAMILIA YAKO NA WATOTO WAKO KWA UPUMBA** WAKO
 
UZINZI NI ZAIDI YA DHAMBI...DHAMBI UIFANYAYO JUU YA MWILI WAKO.

UZINZI NI LAANA...UNASUMBUA FAMILIA YAKO NA WATOTO WAKO KWA UPUMBA** WAKO
Tatizo wanawake ni wengi kuliko wanaume, tusipojitolea wapo wanawake watakosa wapenzi kabisa
 
Back
Top Bottom