Nimsaidieje kisaikolojia atoke kwenye hii hali?

Nimsaidieje kisaikolojia atoke kwenye hii hali?

Kuna kipindi nilikuwa sehemu kikazi mbali na nyumbani nikawa na binti mmoja kama tulizo la upweke.

Ilikuwa kila ninapomuhitaji anakuja na shida zake ndogo ndogo namtatulia. Ilikuwa ni binti decent kimuonekano.

Siku moja ilikuwa nina safari ya kurudi nyumbani. Nilishinda nae siku nzima maana safari ilikuwa ni usiku. Mida ya jioni kulikuja wageni ikabidi yeye abaki chumbani mimi nikawa sebuleni. Kabla ya kwenda sebuleni niliweka pesa nyingi kidogo kwenye droo chumbani lakini nilijua kabisa kiasi chake.

Baada ya wageni kuondoka na muda wa safari kuwadia nilitoa zile pesa na kumpa cha kumpa na kuondoka.

Nilipofika airport kuweka vitu sawa nikagundua ile pesa imepungua kama $500, nikajua moja kwa moja ni yeye.

Baada ya wiki nilirudi huko huko kuendelea na majukumu. Kitu ambacho alikuwa hajui yule binti ni kuwa chumbani kuna camera ambazo kama sio mzoefu huwezi kushtukia.

Nilifika nakutoa SD card na kuangalia siku husika na kumuona binti akichukua pesa na kuficha kwenye sidiria.

Nilimpigia kumjulisha nimerudi na kweli akaja kuniona. Nikamuuliza kama alichukua pesa kwenye droo. Demu alikataa kabisa.
Hapo hapo nakamtumia ile clip ya camera ikimuonyesha anachukua pesa. Alipoifungua message na kuona tu alinyanyuka bila kuaga na kutokomea zake.

Sikumuona tena na hata namba yake ikawa haipatikani tena.

Mwanamke akishikwa wizi na pozi linaisha. Huyo wako atajiondoa mwenyewe maana anahisi thamani yake imeshuka kwako kwa kujua ni kibaka.
Ila we jamaa inaonekana mzinzi sana.
 
Tatizo nyie wanaume uwa mnazingua mtu anaweza akakuomba elf50 unamwambia Leo Sina ngoja ngoja lkn mnatoka mnaenda bar mnakunywa na kuwanunulia friends zako pombe zaidi ya hiyo elf50 na mm nipo hapo sa hapo nikiona hela zinazubaa kwanini nisichomoe Mungu mwenyewe atanisamehe hapo
 
Mwanamke unaekunywa nae mpaka saa tisa hafai kuoa.
 
Back
Top Bottom