Nimsaidieje mpenzi wangu?

Nimsaidieje mpenzi wangu?

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2010
Posts
4,219
Reaction score
4,608
Mpenzi wangu amechanganyikiwa,
anahitaji msaada wangu wa mawazo.
Nimeshindwa kumpa kwa kuwa hata mie nimechanganyikiwa.
Juzi kapata barua ya kufukuzwa kazi.
Kaenda nssf kufuatilia mafao yake, akaambiwa arudi na barua ya mwajiri.
Mwajiri kagoma kumsainia, kasema kwa kuwa alikuwa na mkopo kazini basi mafao yake yanachukuliwa na mwajiri.
Amekuwa akilia tu tangu asubuhi mpaka sasa, kila baada ya dakika tatu ananipigia.
Sina hata maneno mazuri ya kumpa moyo.
Naomba mnisaidie ushauri ili mama watoto apunguze maumivu.
Nampenda sana, akilia yeye na mimi naumia sana rohoni.
 
Huyo mpenzi wako inabidi ukae nae karibu kwa kipindi hiki,mwambie hiyo ndio mitihani ya maisha ,awe mvumilivu na ajipange upya kila kitu kinapita ..Lakini hiyo pesa ya NSSF ina maana huo mkopo unafyeka h Yote ?
 
Mkuu itabidi ujue kwa nini amefukuzwa kazi kiasi kwamba hadi mwajiri hataki kumwandikia barua. Ina maana alipofukuzwa hakupewa barua ya kufukuzwa kazi? Kama hakupewa barua basi kisheria bado ni mfanyakazi halali na ukifungua kesi atalipwa pesa yake ya mshahara kwa muda wote aliokuwa nje ya kazi. Kuhusu issue ya NSSF sidhani kama sheria inaruhusu mwajiri kuchukua pesa ya mwajiriwa hata kama alikuwa anamdai. Nashauri utafute wanasheria wakusaidie juu ya sheria za kazi. inawezekana anataka kuonewa kwa kutokuijua sheria.

Mtie moyo mkeo kuwa suala lake unalishughulikia kwa wanasheria na litaenda vizuri. Show her that you are on top of things. Na kuwa mwisho wa siku atapata haki yake. ASIOGOPE
 
Lazima mtambue nyote wawili kuwa kukosa kazi sio ndio mwisho wa maisha.Pesa inapatikana kwa njia nyingi sana.Na huu ndio wakati muafaka kwake kuwa mjasiriamali na kuacha maisha tegemezi ya kumtegemea mwajiri.Hili ni fundisho kwake na kwetu sote ambao tumaini letu tumeweka kwenye kazi zetu.
kwa vile wewe una kazi bado sioni sababu ya kuchanganyikiwa.msuport kifedha wakati anaangalia jinsi ya kuapta kazi nyingine.Na huyu mpenzi wako si alisoma? na ana vyeti? ndio mtaji wake mwingine.Kulia hakutasaidia kitu yeye apambane na changamoto......
 
Alikuwa Bank gani?
 
Alikuwa n. B.c. Ltd.
Bosi wake ni mwanaume
 
Alikuwa Bank gani?
Ivi kwani wafanyakazi wote wa Bank wamekopa?? hilo swali lako imebidi nicheke!!
kama mdau hapo juu alivyosema....sheria za kazi haziruhusu mtu kufukuzwa kazi kwa mdomo lazima uandikiwe barua ya kuachishwa kazi. Ishu ya NSSF atapa tu wala asiwe na shaka kama mnaweza muoneni mwanasheria awape ushauri zaidi.
 
Hizo barua zinachongwa mitaani tu........waulizeni watu haohao wa NSSF watawapa muongozo
 
Hizo barua zinachongwa mitaani tu........waulizeni watu haohao wa NSSF watawapa muongozo

hata mimi namshangaa anacholia lia. Niliwahi kukumbwa na issue kama hiyo, my bosi was a lady. Nikachanganya na zangu. Nilipopata mkwanja wangu, nikamtumia copy ya malipo niliyopata kumkejeli kwa kuwa alikataa kusaini barua zangu za NSSF.
 
hapo atafute lawyer tu .................haki yake kwa nini aipiganie uchochoroni?
 
Dont remind me of lady boses.....especially kwenye kutoa references....wabaya:A S 39:
 
mpe pole mpenzi wako. katika kipindi hiki kigumu unatakiwa kuwa close sana kumfariji maana inaelekea yuko weak sana inapotokea tatizo. kwani kuachishwa kazi ndio mwisho wa maisha? je huko NSSF ana kabilioni? nijuavyo hakuna uwezekano wa mwajiri wake kuchukua mafao yake ya NSSF unless otherwise walisaini mkataba utakaomtaka mwajiriwa kutumia mafo yako kulipia mkopo iwapo ataacha au kuachishwa kazi na ni mwajiriwa mwenyewe atatakiwa kufuatilia mafao yake.
 
hapo atafute lawyer tu .................haki yake kwa nini aipiganie uchochoroni?

The longest and most winding road to get your rights in Tz........by the time analipwa costs zitakula kwake.....dawa ni kuchonga mikono ya watu
 
Hebu kamsomee hii mistari kisha pigeni magoti muombe "afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwezake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kimwinua" (Mhubiri 4:9, 10)
 
Hebu kamsomee hii mistari kisha pigeni magoti muombe “afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwezake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kimwinua” (Mhubiri 4:9, 10)
 
Pole zake.
Mungu ni mwingi wa rehema, atamrehemu.
Mungu wetu ni baba wa yatima.
Asijali huyo shemeji yetu,
maadamu vyeti vyake vip, kuna chances kibaooo
 
Mwambie yeye si wakwanza kufanyiwa dhuluma ya aina hiyo kwa hiyo asihisi kama mtu asie na bahati duniani..hayo yote yatapita ajaribu kutafuta msaada wa kisheria LHRC hata WLAC.
 
Nakumbuka nilishawahi kupata msuko suko kazini. wife alichanganyikiwa kuliko hata mimi mwenyewe yaliyonikuta.
Wanawake ni rahisi sana kukata tamaa hasa kwa ishu kama hizi.
Cha msingi ni kumkumbusha kuwa haki ya mtu haipotei bali huchelewa.
Na kama ipo, ipo tu.
Never give up the fight.
Dedication song: Three litle birds by Bob Marley.
 
Back
Top Bottom