Nimshauri nini Rafiki yangu baada ya kumpa mimba mke wa mtu

Nimshauri nini Rafiki yangu baada ya kumpa mimba mke wa mtu

Abatmwe

Senior Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
110
Reaction score
79
Nina jamaa yangu amepanga chumba kimoja uko Tandika, sasa katika nyumba iyo iyo chumba kingine kuna dada nae amepanga na mume wake. Jamaa kiukweli ni mtanashati fulani na kwa jinsi alivyo ni mtu wa vimwana sana. Kumbe yule dada alikuwa anamzimia sana yule jamaa yangu ingawa yule mdada ana mume wake mule ndani.

Sasa kilichotokea japokuwa hakunieleza kwa undani jamaa alikuwa anakamata ule mzigo wa mtu, na kwa bahati mbaya jamaa alikuwa hana kazi maalum kwaiyo yeye alikuwa anakamua sana mchana wakati yule mume wa yule demu akiwa kazini.

Walijenga mazoea sana kiasi kwamba mpaka chakula alikuwa anapikiwa na yule demu mchana, demu akishapika huwa anaweka chakula kwenye ndoo ya maji ya kuoga alafu kwasababu walikuwa wanaitumia wote na jamaa anajifanya kama anataka kwenda kuoga anachukua ile ndoo anaingia nayo ndani, anachukua chakula anakula.

Inavyoonekana majirani walishashtukia mchezo na mwenye mke alishapewa dodosi kuwa mkeo analiwa ila kilichokuwa kinamfanya asiamini jamaa alikuwa anaingiza vimwana sana mule ndani , hii ilimfanya hata yule mke wa mtu alikuwa anaona wifu ila jamaa alikuwa anasisistiza kuwa yeye anafanya vile ili kuweka mambo sawa mule ndani ili jamaa asishtukie mchezo, yule mke wa mtu ilibidi awe mpole.

Sasa kilichotokea ni kwamba jamaa kampa mimba yule mke wa mtu kwani kuna kipindi kirefu jamaa alisafiri na yule jamaa yangu ndo alikuwa anagonga kama ya kwake vile maana alikuwa analala nayo ndani kwake kabisa. Ila mwenye mke kwa furaha aliposikia habari za mimba ndo kwanza kalifurahia kuwa sasa anapata mtoto wakati mke mchezo mzima anaujua.

Sasa kilichotokea ni kwamba jamaa amenifata nimpe ushauri kuwa ahame ama la kabla ya mtoto kuzaliwa kwa sababu anajihisi kuwa anadamu kali kiasi kwamba mtoto atakae zaliwa lazima atafanana nae manake uyu jamaa ana mtoto mwingine kafanana nae kila kitu.

Nimeona ili jamabo niliweke umu kuomba ushauri wenu, nimshauri vipi uyu jamaa manake anajihisi aya mambo yatakuja lipuka mtoto atakapozaliwa.
 
Mwambie akae tu hapo hapo asubiri matokeo,mana kama mtihani ashafanya asubiri majibu!!na siku naye akiliwa usisahau kutupa mrejesho mtoa Maada!

Kweli kuna watu mafisadi wa mapenzi,eti chakula kwenye ndoo ya kuogea!!!!
 
Aendelee kukaa tu hakuna shida yoyote. Mwenye mke akija kujua atafurahi sana, anaweza akamnunulia zawadi ya gari huyo jamaa. Kwahiyo mshauri asiwe na wasiwasi kabisa.
Ha ha ha! Daddy ake E's umetishaaa! Kwakweli akae tu hakuna shida; wasiwasi wake tu!
 
Mwambie akae tu hapo hapo asubiri matokeo,mana kama mtihani ashafanya asubiri majibu!!na siku naye akiliwa usisahau kutupa mrejesho mtoa Maada!

Kweli kuna watu mafisadi wa mapenzi,eti chakula kwenye ndoo ya kuogea!!!!
Fisadi haswaaa! Yaani haka kajamaa ni kachafuzi! halafu bado analeta vimwana vingine na kumdanganya mke wa mtu eti anazuga wasishtukiwe!!
 
Kuna watu na viatu....amua moja kubaki hapo ung'olewe kucha
 
huwezi amini haya mambo huwa yanatokea. nilimaliza chuo kikuu nikaenda kufanya internship mkoa fulani. nikapanga chumba. pale kwenye chumba kulikuwa na wapangaji wanne, wanawake wote wameolewa na wana watoto. kuna dada mmoja mpare, alikuwa ameumbika sana, huwezi amini, mume wake alikuwa anasafiri wakati mwingine wiki, ila muda mwingi yupo mjini palepale ana duka kubwa la spare. alianza kwanza anataka awe ananifulia nguo, nikagoma. akaanza kutaka kunipigia uji wa ulezi, nikagoma, mama mwenye nyumba alikuwa na binti mzuri sana miaka 18 nikabeba akawa rafiki yangu wa karibu akawa ananipikia uji, anadeki chumba changu ila kipindi icho tulikuwa marafiki tu na mama yake alipoona nimeshamaliza chuo kikuu na binti mwenyewe hana akili ya darasani, alinyamaza tu wala hakumzuia kuwa karibu na mimi, tukawa marafiki ajabu.

kitu cha ajabu, yule mke wa mtu akaona haitoshi, akawa ananipikia chakula, nikifungua mlango naenda kuoga, nikirudi naona nyuma ya mlango kuna hotpot la ubwabwa na kihotpot kingine cha samaki wa kukaangwa chuzi zitoo...hahaha, mara ya kwanza nikawa nakula tu. ila baadaye nikaja kujistukia anaweza kuniwekea dawa ili nimpende, na mmewe alikuwa kama gaidi katili ajabu mama toka asubuhi hadi jioni hatakiwi hata kwenda sokoni na ni mswahilina swala tano/ushungi.(pamoja na kwamba alikuwa si mrefu si mfupi na ana kiuno cha mviringo mzuri sana).

kuna siku almanusura nilale naye, ananitaka kinguvu, akistukia bwanake amesafiri au anajua hatorudi mapema na pale nyumbani wapangajai wenzake hawapo anatia timu chumbani kwangu..inabidi mimi nitoke nje na kumtoa manake nilishaonywa na mama kuwa huko ninakoenda wanawake wanaweza kukuwekea dawa na mke wa mtu ni sumu mumewe akijua maisha yako yanaharibika siku hiyohiyo.

nikapata mchumba mpya mji uleule, hapo ilibidi ndani ya mwezi huo nihame ile nyumba nikaenda kupanga kwingine, kwasababu nilikuwa nimetangaza vita kati yangu na yule binti wa mwenye nyumba, mwenye nyumba mwenyewe aliniita na kunionya nisimwache binti yake.

ajabu sasa, yule mke wa mtu aligeuka mbogo kuona nimepata demu (ambaye ndio mke wangu hadi leo), alinitukana matusi yote ya nguoni, pale nyumbani walizichapa na wapangaji wenzie hadi nilishangaa hawa wake za watu vipi? sijawahi kurudi pale kwenye nyumba na niliacha kodi ya mwezi mmoja nikakimbia hadi leo. mwenye nyumba nasikia amekufa na yule demu ana watoto wawili.

mwenye mume sasa alikuja kujua, ila ni mimi nilienda kumwambia kwasababu yule mkewe alienda kutaka kupigana na mke wangu mtarajiwa, nikaona hapa mumewe akijua kabla ya mimi kumwambia anaweza kuamini maneno ya watu, nikajipeleka mwenyewe nikamwambia mkeo ananisumbua.palikuwa padogo almanusura mkewe arudishe same. walishapatana na wanaendelea na maisha ila nisingeenda kumwambia mmewe kuwa mkewe ananisumbua, yeye angesikia kwa watu angenivizia na kunitandika tu. yeye mwenyewe alinisifu kuwa bora nimeenda kumwambia manake nisingemwambia yeye angesikia kwa mwingine angeamini na asingekuja kuniuliza mimi zaidi ya kunikodia watu wanimalize. hao ndio wanawake walioko majumbani mwa watu hawaridhikiiiii.
 
Hiyo mimba sio yake mume aliposafiti jirani mwengine alipewa na ndie aliempa mimba
 
Nimechoka kusikia rafiki yngu, mke/mume warafiki yangu. Inabidi mbadilike jaman. Sema mimi
 
nakushauri tu uwe na ky karibu, muda wowote lolote laweza kukutokea...
 
Mwambie kila anaeizini na mke wa mwenzie na yeye ataziniwa hata na ukuta.. Na mtenda akitendwa atahisi kaonewa.. Midhali ameshainajisi ndoa ya mwenziwe na yeye asubiri hayooo.. What goes around.. comes around..
 
Ha ha ha ha shem huo ushauri wako kiboko japo unaweza msaidia lol.. Nimechekaje hapa mie.. Kweli mke wa mtu sumu..
shem siku hizi adhabu zimekua kali mwanaume akidakwa analiwa mwanamke akidakwa anakalia chupa....
 
Nina jamaa yangu amepanga chumba kimoja uko Tandika, sasa katika nyumba iyo iyo chumba kingine kuna dada nae amepanga na mume wake. Jamaa kiukweli ni mtanashati fulani na kwa jinsi alivyo ni mtu wa vimwana sana. Kumbe yule dada alikuwa anamzimia sana yule jamaa yangu ingawa yule mdada ana mume wake mule ndani.

Sasa kilichotokea japokuwa hakunieleza kwa undani jamaa alikuwa anakamata ule mzigo wa mtu, na kwa bahati mbaya jamaa alikuwa hana kazi maalum kwaiyo yeye alikuwa anakamua sana mchana wakati yule mume wa yule demu akiwa kazini.

Walijenga mazoea sana kiasi kwamba mpaka chakula alikuwa anapikiwa na yule demu mchana, demu akishapika huwa anaweka chakula kwenye ndoo ya maji ya kuoga alafu kwasababu walikuwa wanaitumia wote na jamaa anajifanya kama anataka kwenda kuoga anachukua ile ndoo anaingia nayo ndani, anachukua chakula anakula.

Inavyoonekana majirani walishashtukia mchezo na mwenye mke alishapewa dodosi kuwa mkeo analiwa ila kilichokuwa kinamfanya asiamini jamaa alikuwa anaingiza vimwana sana mule ndani , hii ilimfanya hata yule mke wa mtu alikuwa anaona wifu ila jamaa alikuwa anasisistiza kuwa yeye anafanya vile ili kuweka mambo sawa mule ndani ili jamaa asishtukie mchezo, yule mke wa mtu ilibidi awe mpole.

Sasa kilichotokea ni kwamba jamaa kampa mimba yule mke wa mtu kwani kuna kipindi kirefu jamaa alisafiri na yule jamaa yangu ndo alikuwa anagonga kama ya kwake vile maana alikuwa analala nayo ndani kwake kabisa. Ila mwenye mke kwa furaha aliposikia habari za mimba ndo kwanza kalifurahia kuwa sasa anapata mtoto wakati mke mchezo mzima anaujua.

Sasa kilichotokea ni kwamba jamaa amenifata nimpe ushauri kuwa ahame ama la kabla ya mtoto kuzaliwa kwa sababu anajihisi kuwa anadamu kali kiasi kwamba mtoto atakae zaliwa lazima atafanana nae manake uyu jamaa ana mtoto mwingine kafanana nae kila kitu.

Nimeona ili jamabo niliweke umu kuomba ushauri wenu, nimshauri vipi uyu jamaa manake anajihisi aya mambo yatakuja lipuka mtoto atakapozaliwa.

Hiyo dam kali ikoje?
 
Back
Top Bottom