Nimuoe nani?


d) hili hapanaaaaaaaa
 
Hii sio mara ya kwanza kuskia hii mambo,.wala wewe sio wa kwanza kufanya huu ufirauni!at times kuna wanaume wanawapa baadhi ya wanawake sababu za kutoolewa kabysa!kwa mila zetu,ulishamuoa huyo,so hiyo ni total infidelity.
Mwambie mchumba wako all that you have done yeye ndo atachagua,ila i doubt the so called upendo unaosema!.Love sio maneno tu,your actions speak otherwise!
 

pole sana ndugu yangu,
kweli yaliyokukuta ni magumu na watu wamecomment kukulaumu,YES kwa upande mwingine wa kulaumu ila unahitaji ushauri.huyo mjamzito mtunze tu mwanae na ye mwenyewe huko kwingine.
yule dada uliemtolea mahari tayali ni mkeo kimila ila si kimungu.cha muhimu mkalishe chini mchumba wako mweleze ukweli na jinsi shetani alivokupitia na muombe msamaha na akuchukulie hivyo na mipango yenu ya ndoa iendelee.kama ni mwelewa na ni mke mwema mwenye kusamehe atakae kufaa maishani atakusamehe tu. kama likimuuma sana na akashindwa kusamehe basi ishia hapo na uende kuoa mjamzito.
 
Acha mambo ya kitoto Plato, wakati unaanza mahusihano mapya na huyo binti haukukumbuka kuwa una mchumba ambaye amukuvumilia miaka 3? Pili nani alikutuma kufanya ngono zembe na msichana ambae ameachana na boyfriend wake wa zamani? Sasa unauliza nini? Ndio mshahara wa uzinzi huo
 
Nashukuru sana kwa wote waliochangia.walionitukana,wana haki kufanya hivyo.napokea yote.walionishauri pia nashukuru,ninaendelea kutafuta balance.laumu imeuvunja moyo wangu.nimejilaumu na kujilaumu,muhimu ni way forward.naguswa mno na masuala haya.sitafuti haki wala huruma,natafuta njia ya kutuvusha salama.asanteni.
 

Plato, plato, plato! How many times i called you?. Hizo redi ni makosa yako, ungejitahidi kuepuka hayo yote yasinge kukuta. Anyway yamesha tokea, Ushauri wangu.. Usitake uonekane eti wewe ni mzuri kwa wote kwa sababu haupo hivyo. ndio maana ukawa una do bila kinga wakati una demu mwingine usha mlipia mahari. mpaka hapo you are coward. Chakufanya; Mmwage mmoja, usijifikirie marambili mbili, angalia moyo wako uliko dondokea zaidi. usihesabu miaka ya uchumba wala mimba....
 
Plato, Kama upo serious ni PM nikupe ushauri zaidi kwa hapa nikitoa huo ushauri nitaharibiwa siku, halafu nikijibu BAN juu
 

mkuu pole sana ila usibabaike hata kidogo.wala hasira za watu zisikuzingue.wangapi wameoa/wameolewa kabisa na ndoa na bado wanachakachua nje mpaka wanafumaniwa?sembuse wewe umetoa tu mahari hujaoa bado!!!!cha msingi tulia mtoto azaliwe na uhakikishe kua ni wakwako.then kati ya hao wawili utapima nani anafaa zaidi kumuweka ndani kwa kuzingatia vigezo vyako then unaoa.wakati wa kuoa unahakikisha unaemuoa anaelewa hali halisi.ila kwa sasa uchune mpaka vugu vugu lipoe kwanza.kikubwa ni kua makini next time swala lisijirudie.mtoto utalea ingekua ukimwi je?
take care, utapotea.kosa hufanywa mara moja tu!!
 
Dou! imekuwaje tena ukaanza uhusiano wa mapenzi na rafiki yako? Mwambie ukweli tu ili ajue kwamba una mchumba ila zaidi ya hapo fikiria kwamba ana ujauzito. pia angalia nani kati ya hao wawili anakidhi vitu unavyotaka kwa mke
Jambo la pili uchunguzi wangu unaonyesha, watu waliooana ambao walikuwa marafiki sana inaonyesha ndoa zao zilikuwa zina mafanikio sana sababu kila mtu hamna wa kumdanganya mwenzake. kila kitu cha mwemzake unakijua, weakness na stregth zote unazijua inakuwa rahisi. haya kijana uamuzi ni wako
 
Susy,Lizzy,Liz senior,Sweetdada,DenaAmsi,Fanta face,Marytina chonde chonde wapendwa kijana Plato hajaua mtu! Ni karata tu kazichanga vibaya na anaona zinamtokea puani. Binafsi niseme tu kwamba kuleta kiumbe duniani ni jambo la thawabu,tumpongeze kwa hilo na kumwombea dada mwenye mimba ajifungue salama.Yaliyobaki haya mbona yanaongeleka tu?
 
Dah pole kaka angu.
Hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea.
Nimeumia, lakini pia sitakiwi kuhukumu sana, manake sijawahi kuwa safi asilimia mia moja.
Hata kama sio katika uzinzi hata katika mengine tu.

Hebu nyenyekea mbele za Mungu wako, muombe rehema na Neema ya kupita hapo ulipo sasa.
Tulia kimya, kubali kila lawama na neno utakalotupiwa/nenewa na wazazi wa hao mabinti, rafiki na ndugu zao, na machozi watakayolia,
ndiyo, mshahara wa makosa yako. Uwe mpole, huku ukiomba hekima.

Mke mwema hutoka kwa bwana, haijalishi umelipa mahari, au umezalisha, Mungu anawawazia mawazo ya Amani hao mabinti kuliko hata mimi na wewe, tunavyowawazia. Tulia kabisa waombee hao mabinti, hasa huyo mwenye mimba Mungu amjalie ajifungue salama.
Apate nguvu na afya, baada ya hapo naamini hata akili itakuwa imetulia, na utafanya uamuzi sahihi.

Kumbuka ukifanya uamuzi sahihi, itakuwa faida kwenu nyote, kwani ukimuoa yule anayeendana nawewe, utakuwa na amani kwenye familia,
na huyo mwingine naye Mungu atamjalia mume mwema, na ataishi kwa furaha.

Pole sana, hii ndiyo dunia tunayoishi, wewe sio wa kwanza wala hautakuwa wa mwisho. Kikubwa unyenyekevu unahitajika sana hapa.
Ili uvuke salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…