Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah pole kaka angu.
Hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea.
Nimeumia, lakini pia sitakiwi kuhukumu sana, manake sijawahi kuwa safi asilimia mia moja.
Hata kama sio katika uzinzi hata katika mengine tu.
Hebu nyenyekea mbele za Mungu wako, muombe rehema na Neema ya kupita hapo ulipo sasa.
Tulia kimya, kubali kila lawama na neno utakalotupiwa/nenewa na wazazi wa hao mabinti, rafiki na ndugu zao, na machozi watakayolia,
ndiyo, mshahara wa makosa yako. Uwe mpole, huku ukiomba hekima.
Mke mwema hutoka kwa bwana, haijalishi umelipa mahari, au umezalisha, Mungu anawawazia mawazo ya Amani hao mabinti kuliko hata mimi na wewe, tunavyowawazia. Tulia kabisa waombee hao mabinti, hasa huyo mwenye mimba Mungu amjalie ajifungue salama.
Apate nguvu na afya, baada ya hapo naamini hata akili itakuwa imetulia, na utafanya uamuzi sahihi.
Kumbuka ukifanya uamuzi sahihi, itakuwa faida kwenu nyote, kwani ukimuoa yule anayeendana nawewe, utakuwa na amani kwenye familia,
na huyo mwingine naye Mungu atamjalia mume mwema, na ataishi kwa furaha.
Pole sana, hii ndiyo dunia tunayoishi, wewe sio wa kwanza wala hautakuwa wa mwisho. Kikubwa unyenyekevu unahitajika sana hapa.
Ili uvuke salama.
LD nina moja tu la kusema..UNA BUSARA SANA!Mungu akuzidishie.
Now you are talking,ushauri maridadi kabisa! ngoja nikupige na senks nyingine kwa niaba ya Plato....THANKS....BIG UP LD!Dah pole kaka angu.
Hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea.
Nimeumia, lakini pia sitakiwi kuhukumu sana, manake sijawahi kuwa safi asilimia mia moja.
Hata kama sio katika uzinzi hata katika mengine tu.
Hebu nyenyekea mbele za Mungu wako, muombe rehema na Neema ya kupita hapo ulipo sasa.
Tulia kimya, kubali kila lawama na neno utakalotupiwa/nenewa na wazazi wa hao mabinti, rafiki na ndugu zao, na machozi watakayolia,
ndiyo, mshahara wa makosa yako. Uwe mpole, huku ukiomba hekima.
Mke mwema hutoka kwa bwana, haijalishi umelipa mahari, au umezalisha, Mungu anawawazia mawazo ya Amani hao mabinti kuliko hata mimi na wewe, tunavyowawazia. Tulia kabisa waombee hao mabinti, hasa huyo mwenye mimba Mungu amjalie ajifungue salama.
Apate nguvu na afya, baada ya hapo naamini hata akili itakuwa imetulia, na utafanya uamuzi sahihi.
Kumbuka ukifanya uamuzi sahihi, itakuwa faida kwenu nyote, kwani ukimuoa yule anayeendana nawewe, utakuwa na amani kwenye familia,
na huyo mwingine naye Mungu atamjalia mume mwema, na ataishi kwa furaha.
Pole sana, hii ndiyo dunia tunayoishi, wewe sio wa kwanza wala hautakuwa wa mwisho. Kikubwa unyenyekevu unahitajika sana hapa.
Ili uvuke salama.
Umeriharibia siku yangu yote.
Plato, Kama upo serious ni PM nikupe ushauri zaidi kwa hapa nikitoa huo ushauri nitaharibiwa siku, halafu nikijibu BAN juu
Hapa mambo ni magum.tafuta dini inayoruhusu uoe wote uongeze na mwingine,
Multiple choice;
a). Waoe wote kwa maana umejitakia kwa tamaa zako, na uwe tayari kumuongeza na mwingine....! Lakini ujue kuwa kila mwanaume akiwa na wanawake wawili, basi pembeni ana mume mwenzie.....!
b). Waache wote, na hivyo pia uwe tayari kuendelea na maisha ya ukapera daima huku ukiwa na laana zisizo na suluhisho hadi motoni.....!
c). Kaa kimya, kwa maana when the time is over, it will tell who you have to marry.....! Na kwa vyovyote uaminifu hautakuwepo kwenye ndoa hiyo daima maishani mwako....!
d). Yote hayo yakikushinda basi jiue aidha kwa sumu au kwa kamba, ili wote wakukose na uzikwe ukiwa na amani kama ndio kusudio lako....!
Nashindwa kufanya maamuzi.nisaidieni mawazo.yanisaidie kufanya maamuzi. Nina wasichana 2,mmoja ni mchumba wangu,uchumba wetu una miaka 3 sasa,na tumetoa zaidi ya mahari.nilimpromisse kumuoa mwaka kesho akasema atanisubiri na amefanya hivyo.ninampenda sana.nadhani naye ananipenda.lakini upande mwingine rafiki yangu wa miaka mingi(msichana) mhitimu wa university ambaye aliachana na boyfriend wake na akakaa zaidi ya mwaka bila uhusiano.ikatokea tumezoeana sana ndg zake wengi wakanijua tukawa kama ndugu.mwaka jana nikiwa na mchumba tayari tukaanza kuwa na mahusiano ya mapenzi.akawa anaongea kuwa anaridhika nami hata nikimuoa kwani ananifahamu.sasa imetokea akapata mimba,na yeye kafurahi kwamba si nitamuoa.hajui habari za mchumba wa tangu kabla yake.mimba ina miezi 4 sasa.UTATA: Nimuoe nani kati yao,inaniwia vigumu kuvunja promisse kwa mchumba aliyenivumilia kwa miaka 3 sasa,wakati huohuo inaniwia vigumu kumtelekeza niliyempa mimba na kubadili maisha yake.pili nafikiri nn kitatokea kwa uamuzi wowote nitakaochukua.kwangu limekuwa zito,nishaurini.asante