Nimuoe yupi kati ya watatu hawa?

Nimuoe yupi kati ya watatu hawa?

Ngoja tu na mimi nikuonye braa...
Hauko peke yako ,ila na wenzako wote wenye tabia kama yako(material man)..!
Wapo wa kike wenye tabia kama zenu ambao wametanguliza mbele vitu,vitu tu,zawadi na pesa.. !!
Sitaki kusema tu SIYO VIZURI ila kwa watoto wa Kiume ni HATARI pia..
Hivi ukizungumzia Simu,pesa ndogo,ndogo na zawadi kutoka kwa wadada...
Unanitia Shaka na Hofu sana..
Hivi ukiwekewa/ukipewa GARI wewe, utausimamia kweli UWANAUME WAKO..???
Sina hakika..
Dont be material..
Be man..
 
Wee kaka inaelekea unapenda sana kulelewa na kuhudumiwa ambapo sio tabia nzuri na sio kipimo cha mapenzi hicho. Oa unayempenda na sio anayekupa vitu.
 
wataarifu wote kwa ugumu unaopata kufanya maamuzi ..waambie wote umewashort list sasa challlenge unayoipata ndo hiyo hujui yupi umchague na kumvike pete ..otherwose nachoweza kukushauri ni kuwa wapigiwe kura na kila mmoja apewe muda wa kujieleza ili kuwa na level playing ground...sijui umeshanifahamu???
 
Siku unawatafuta hao wabinti uliomba ushauri hapa jukwaani? Kwanza sidhani kama kuna mtu hapa jukwaani anayejua hata mmojawapo kati ya mabinti hao, fanya uamuzi wa busara halafu nakupa ushauri wa bure "acha umalaya".
 
Wenyewe wanajua kama unawapanga kama bamia sokoni?
 
oa muuzaji mtoke ngoma droo hao utawapasua vichwa tu
 
we mbwiga sana kijana, hakuna unayempenda hapo, maana usingemiliki mademu watatu kwa wakati mmoja, we sema tu unasafiria nyota zao kujikwamua na maisha magumu ya chuo ya kutegemea boom. Yaani we ni mwanaume mchunaji huna lolote, unapenda kulelewa wewe. Chunga sana na hiyo tabia. Unahongwa bukku 20 unaona unapendwa! We kweli ni ndezi
 
Wenyewe wanajua kama unawapanga kama bamia sokoni?

wazinzi huwa hawasemi kuwa wamewapanga. Huyo ni mzinzi kama walivyo wazinzi wengine. Yaaani kijana hana hata kazi wala mshahara anamiliki mademu watatu, imagine siku akimaliza chuo na kupata job yenye mshiko atamiliki wangapi?
 
Hi everyone.

Mimi ni mgeni humu javini naomba kuchangia hii mada.

Kifupi acha kuwapotezea muda hao kinadada. Wewe si muoaji. ungekuwa muoaji muda mrefu ungekuwa umefanya maamuzi wa yule ambaye ulianza naye. kwanza unasema unawanawake 3 uliwapata kwa pamoja au kwa nyakati tofauti? nimekuona bonge la **** kwa kuchezea feeling za watu. mwanamke akisema anawanaume watatu mnasema mhuni. vip kuhusu wewe tukuiteje ilihali bado mwanafuzi?

we ni mgen sawa ila mbona hujajitambulisha vizuri? Jaza mwaswali yafuatayo:-
1.sex
2.marital status
3.age
4.residance
5.education
6.occupation
 
pls acha kbs kuchezea hisia za hawa viumbe.kila unayekutana naye unamuweka ktk foleni ya ahadi ziczo tekelezeka hiyo wakwe2 kaaukijua itakuja kukusumbua na kukuathir kisaikolojia kwa taabu watakazo jibu kwako hapo baadaye
 
Mmoja amegraduate Udom mwaka huu,ananisisitiza sana nimuoe kwani tayari ameniona nafaa kua mumewe.

Wa pili anachukua diploma ya ualimu mwaka wa kwanza,huyu tayari amewajulisha wazazi wake kua tayari amepata mchumba na si siku nyingi amewahidi kunipeleka kwa utambulisho.

Mwingine na watatu,ni darasa la saba ila ni mfanyabiashara,hapendi kuona mimi napata taabu pale ninapokua na tatizo na hujitahidi kunitumia pesa kama hivi nilivyo hapa chuoni.

Nisaidieni kimawazo,kwani wote pia wanaupendo wa dhati pamoaja nami.Kwa mfano:aliopo diploma amenitumia simu wiki ilopita,wa udom alinipatia sana fedha ya kula nikiwa field,wakati huo bodi ya mikopo walikua hawajanipa fedha na watu mwanzoni mwa wiki alinitumia 20,000/=kukabiliana na matatizo madogo-madogo.

Nifanyeje mimi,mwenzenu.Napata wakati mgumu kujua nimuoe nani na niwache wakinani!
Ww jifanye kidume unavizuzua vibinti vya watu. Badala ya kuchangamkia masomo unashabikia vitu unavyohongwa. Kibaya zaidi unajinadi kuwa ni mpenda vya kupewa. Kumbuka dunia ya leo imekaa kushoto kulia. Zipo njemba zinakusoma udhaifu wako. Watakurushia laki 5 tu chaaali unaolewa kijana. Tafakari, chukuwa hatua. Zingatia masomo. Acha uzinzi ni nooomaaa...
 
Manachuo gani anaweza kuoa, labda kama wewe ni in service.Watu tunakaribia mwaka mtaani bila kazi sasa ingekuwaje kama tungekuwa na mawazo ya nimuoe yupi kati ya watatu kama wewe.Ni wazi wewe si in service ndo maana una dhiki jambo linalokufanya uone mapenzi ni material things.Hujazungumzia yupi yuko vizuri kitandani kwa mfano, jambo ambalo ni muhimu mno ktk masuala hayo.Nami nadhani huna uwezo wa kuoa bwana soma kwanza, kama unaendelea kufanya nao ngono endelea tu ila kuoa tusidanganyane.
 
Kamanda hapo hujawapenda hao mabinti, ila umependa hivyo wanavyokupatia. Wao wanafanya kila jitihada kukuonesha kuwa wanakujali, lakini wewe unachoangalia ni pesa zao. We cha maana ni kuangalia ni yupi unayempenda, bila kuangalia anakupatia nini. Kumbuka jukumu la kuja kutunza familia ni la kwako wewe kama baba mtarajiwa, na wala si la mkeo mtarajiwa. Leo wanakuletea, ukishaoa wanataka uwapelekee! Vua gamba, na ufanye uamuzi mgumu wa kukataa mazoea ya wawili kati yao ili ubakie na mmoja. UNATAKIWA UVUE GAMBA KAMANDA, biashara nia asubuhi, jioni ni mahesabu.
 
Ngoja tu na mimi nikuonye braa...
Hauko peke yako ,ila na wenzako wote wenye tabia kama yako(material man)..!
Wapo wa kike wenye tabia kama zenu ambao wametanguliza mbele vitu,vitu tu,zawadi na pesa.. !!
Sitaki kusema tu SIYO VIZURI ila kwa watoto wa Kiume ni HATARI pia..
Hivi ukizungumzia Simu,pesa ndogo,ndogo na zawadi kutoka kwa wadada...
Unanitia Shaka na Hofu sana..
Hivi ukiwekewa/ukipewa GARI wewe, utausimamia kweli UWANAUME WAKO..???
Sina hakika..
Dont be material..
Be man..

Good point. Big up man!!!
 
Dogo tafuta kazi kwanza utaingia ofisini utakutana na totoz kali kali utajuta maliza shule uanze kazi dogo ukiwa stable kiuchumi utafanya maamuzi mazuri zaidi.Kwa sasa upo tegemezi sana hata kuoa sikushauri
 
wazinzi huwa hawasemi kuwa wamewapanga. Huyo ni mzinzi kama walivyo wazinzi wengine. Yaaani kijana hana hata kazi wala mshahara anamiliki mademu watatu, imagine siku akimaliza chuo na kupata job yenye mshiko atamiliki wangapi?

kama unawado wote namshauri awaowe wote ili uishi maisha ya full dezo mnzinzi we
 
Unaonekana wewe ni material na unapenda kulelewa, nia yako unataka ushariwe yupi atakulea!!
 
take this.
ngoja tu na mimi nikuonye braa...
Hauko peke yako ,ila na wenzako wote wenye tabia kama yako(material man)..!
Wapo wa kike wenye tabia kama zenu ambao wametanguliza mbele vitu,vitu tu,zawadi na pesa.. !!
Sitaki kusema tu siyo vizuri ila kwa watoto wa kiume ni hatari pia..
Hivi ukizungumzia simu,pesa ndogo,ndogo na zawadi kutoka kwa wadada...
Unanitia shaka na hofu sana..
Hivi ukiwekewa/ukipewa gari wewe, utausimamia kweli uwanaume wako..???
Sina hakika..
Dont be material..
Be man..
 
Back
Top Bottom