Nimvumilie mume huyu au nimuache?

Nimvumilie mume huyu au nimuache?

...hizi ndoa zinakuwa kama mtu anaishi na house girl wake vile?,....!

Mm n msichana nna miaka 26,nmeolewa na nna mwaka wa 4 sasa katka ndoa.mume wangu amenipita kama miaka 12 hiv
Tatzo ni mume wangu ana wivu sana,asisikie kitu hana haja ya kufatilia km n kweli au lah ye ananihukumu tu.ameshanitoa kwake zaid ya mara 3 nami narudi home, baada ya miez kadhaa huwa ananifata na kutaka nirud tukaish sote.

Nikirud matatizo n yaleyale, hana muda wa kuwa nami hata kidogo, akitoka asbh kurud usiku saa 8 au 9. Had ss cjabahatika kupata mtoto nahc kutokana na stress na hata tendo la ndoa n nadra sana kwetu kwan amehama chumba yapata miez 6 sasa,so ukitaka game had umfate na anaweza akakubal au akaushe.matuc ni jambo la kawaida kwake na gubu ,nyumba yangu, ktanda changu n maneno yake had inakuwa kero.
kila siku ni kuninyanyasa. yan nakosa raha ya kuwa na mwenza,hakuna hata muda wa kupga story na hata akitoka haagi kabsa.
Nampenda sana mume wangu nmejaribu kukaa nae na kuzungumza hakuna unafuu wwt had sasa.

Nmebahatka kumaliza degree ya kwanza chuo cha UD,nawaza nitafute kaz ili niondoke nikaanze maisha yangu upya, nnachowaza ndoa yangu n ya kanisan na kama mjuavyo ugumu wake, lakin upande mwingine nataman nam niwe na maisha ya furaha na mtu atakaenijal, kuniheshimu na kunipenda kwa dhat ,na ukizingatia umr wangu mdogo bado ntamvumilia for hw long!

Naomba mnisaidie kwa ushaur*
 
ahh anajifanya kidume full?
alitahiriwa na shoka?
pumba.v.u zake...wewe huyo akutak dada ...
kurud sa 9
kahama chumba
hana tyme na wewe
sa unasubiri nin?

ata hao madikteta unaowasikia akina mussolini sjui hitler walikuwa wanawasikiliza wake zao...wanazungumza na wake zao...wana tyme na wake zao...sasa YE NANI WA KUJIFANYA ASIKILIZ.HAAMBIWI WALA HASHAURIKI?..m tellng u kuna sehemu ambayo anatiii yote anayoambiwa ..infact anaamrishwa fanya ivi usifanye vile yaan anaendeshwa afu et anakuja kwako anajifanya komando ushuzi asiyeskia audio wala vdeo atak kuona?PAMADAKU.

ukiona mwanaume anafanya ivo it means HAKUTAKI.kuwa na nyumba ndogo sio issiue ,anaweza kuwa na nyumba ndogo na bado akakutrit na kukupenda km malkia wake....kuna mdada mmoja aliambiwa mme wake anafyodoa nje ahh akawajibu ili mrad anawai kurud.ananiheshimu.ninachotaka napata. na ananisikiliza ahh poa tu ngoja tu nkamwambie asisahau condomu uko anakokwenda....

uyo akutak dada...KATUMIA VTENDO KUKUPA SOMO...afu bado aujazaa nae ahh raha tupu yaan apo nasepa uku naimba mapambio kwa raha zangu...HANITAK JAMAN SASA NIFANYEJE?

Hayo ndio maneno, vumilia,vumilia,vumilia,vumilia,vumilia,vumilia,vumilia,vumiliaaaaaaaaaa
naona sasa unakuwa wimbo, miaka minne hakuna kinachoendelea, avumilie nini, kuna vinavyovumilika na vingine katu,
ashauliki, wa kazi gani kama haoni umuhimu wako??????? wapo watakaoona umuhimu wako, PIGA CHINIIIIII
 
kumuacha au kuendelea anaamua muhusika mwenyewe otherwise mahakama kama kutakuwa na ugonvi wa kupigana. pole sana. mara nyingi nimexperience wanawake wanaolewa na wanaume wakubwa kwa sababu ya shida fulani ikiwemo ya kiuchumi huwa wanakutana na hali kama hii. ni vema tukajifunza.
 
Dada lipo jambo unatuficha au hujatuambia ukweli hapa, naona unavutia kamba kwako tu!! kimsingi ndoa yeni ina matatizo makubwa na ni ya muda, na wewe ni mmoja kati ya watu ambao wamesababisha matatizo haya na si mumeo pekee... mpaka mume amehama chumba maana yake hakuamini tena, lipo jambo ulilomtendea ambalo limempotezea uaminifu kwako na hata hamu ya mapenzi na ndo mana hamuelewani... kama unataka wana jf wakusaidie kiukweli, jaribu wewe kuwa mkweli kwa kueleza kiuwazi juu ya nini hasa kinaendelea kiuhalisia... usivutie kamba kwako kwa kuonyesha kuwa mumeo ana matatizo au ndo chanzo cha migogoro... wewe pia una matatizo na vema ukayasema then ndo usaidiwe... JF is everything utapata tiba tu ukiwa wazi
 
Mm n msichana nna miaka 26,nmeolewa na nna mwaka wa 4 sasa katka ndoa.mume wangu amenipita kama miaka 12 hiv
Tatzo ni mume wangu ana wivu sana,asisikie kitu hana haja ya kufatilia km n kweli au lah ye ananihukumu tu.ameshanitoa kwake zaid ya mara 3 nami narudi home, baada ya miez kadhaa huwa ananifata na kutaka nirud tukaish sote.

Nikirud matatizo n yaleyale, hana muda wa kuwa nami hata kidogo, akitoka asbh kurud usiku saa 8 au 9. Had ss cjabahatika kupata mtoto nahc kutokana na stress na hata tendo la ndoa n nadra sana kwetu kwan amehama chumba yapata miez 6 sasa,so ukitaka game had umfate na anaweza akakubal au akaushe.matuc ni jambo la kawaida kwake na gubu ,nyumba yangu, ktanda changu n maneno yake had inakuwa kero.
kila siku ni kuninyanyasa. yan nakosa raha ya kuwa na mwenza,hakuna hata muda wa kupga story na hata akitoka haagi kabsa.
Nampenda sana mume wangu nmejaribu kukaa nae na kuzungumza hakuna unafuu wwt had sasa.

Nmebahatka kumaliza degree ya kwanza chuo cha UD,nawaza nitafute kaz ili niondoke nikaanze maisha yangu upya, nnachowaza ndoa yangu n ya kanisan na kama mjuavyo ugumu wake, lakin upande mwingine nataman nam niwe na maisha ya furaha na mtu atakaenijal, kuniheshimu na kunipenda kwa dhat ,na ukizingatia umr wangu mdogo bado ntamvumilia for hw long!

Naomba mnisaidie kwa ushaur*

we binti weee!!! yaani na degree yako bado jamaa anakufanya kama ndo umetoka sitimbi!
huna mume kimbia haraka sana acha unyonge wa kijinga!

Mume mwema mtu hupewa na Mungu.
 
Mm n msichana nna miaka 26,nmeolewa na nna mwaka wa 4 sasa katka ndoa.mume wangu amenipita kama miaka 12 hiv
Tatzo ni mume wangu ana wivu sana,asisikie kitu hana haja ya kufatilia km n kweli au lah ye ananihukumu tu.ameshanitoa kwake zaid ya mara 3 nami narudi home, baada ya miez kadhaa huwa ananifata na kutaka nirud tukaish sote.

Nikirud matatizo n yaleyale, hana muda wa kuwa nami hata kidogo, akitoka asbh kurud usiku saa 8 au 9. Had ss cjabahatika kupata mtoto nahc kutokana na stress na hata tendo la ndoa n nadra sana kwetu kwan amehama chumba yapata miez 6 sasa,so ukitaka game had umfate na anaweza akakubal au akaushe.matuc ni jambo la kawaida kwake na gubu ,nyumba yangu, ktanda changu n maneno yake had inakuwa kero.
kila siku ni kuninyanyasa. yan nakosa raha ya kuwa na mwenza,hakuna hata muda wa kupga story na hata akitoka haagi kabsa.
Nampenda sana mume wangu nmejaribu kukaa nae na kuzungumza hakuna unafuu wwt had sasa.

Nmebahatka kumaliza degree ya kwanza chuo cha UD,nawaza nitafute kaz ili niondoke nikaanze maisha yangu upya, nnachowaza ndoa yangu n ya kanisan na kama mjuavyo ugumu wake, lakin upande mwingine nataman nam niwe na maisha ya furaha na mtu atakaenijal, kuniheshimu na kunipenda kwa dhat ,na ukizingatia umr wangu mdogo bado ntamvumilia for hw long!

Naomba mnisaidie kwa ushaur*

ktk haya maandishi yako inaonekana bado kuna vitu vingi umevificha. mpaka mtu akahama chumba kulikuwa na sababu. sababu hii yaweza kuwa ni wewe , au mumeo mwenyewe.

utaweza kusaidiwa vizuri ikiwa utaweza kwanza kueleza makosa yote ambayo wewe umeyafanya. nahayo aliyo fanya mumeo. sisemi wewe unamakosa peke yako, lakini ninatia mashaka juu ya huyu mtu kugeuka kwa kiwango hiki. kuna mahali wewe huenda ulikosea na unadhani yeye hajui, au anajua na hujaonyesha nia ya dhati ya kujuta na kutubu kosa lako.ndiyo maana sasa anakuona hufai tena na huaminiki tena

kwa upande wake huenda kanusa mahali pazuri huko nje, sasa ni kama anajutia uamuzi wa kukuoa wewe, sasa anakufukuza lakini akiwaza anaona una umuhimu fulani. hapa hata sababu ya kukosa mtoto inaweza kuwa nio chanzo cha vurugu.

USHAURI

ndoa inafanyika kwa mwenye jinsia ya kike na jinsia ya kiume, na inakamilika kwa tendo la ndoa. kama wewe hupewi tendo la ndoa , na mnalala chumba tofauti unaweza kufanya haya yafuatayo
1. kama wewe unampenda sana mume wako na ungependa kuibeba hiyo hali waweza msamehe tu na uishi tu nae
2. kama unaona nhiyo hali haifai kwako na haivumiliki basi usiogope eti ndoa haivunjiki, kwa hiyo tafsiri ya ndoa hapo juu, ukiweza kulithibitishia kanisa kuwa hupati tendo la ndoa na munalala nae chumba tofauti kanisa lita tengua hiyo ndoa
3. unasema mumeo akisikia maneno tu anakutuhumu. hapo nadhani wewe unamatatizo, kwanini wewe unaingia ingia tu kwenye maneno ilihali unajua kuwa mwenzio anawivu?. jiangalie, ndoa ni kujitoa kwa mwenzio. kama unajua kuwa mwenzio anawivu , basi achana na mawasiliano tata , au kujiweka ktk mazingira yanayokufanya utiliwe mashaka.
4. wakati unawaza hayo 1-3 hapo juu, kumbuka siku ulipoolewa ulipoteza sehemu ya uhuru wako, na yeye ( mumeo ) alipoteza sehemu ya uhuru wake. sasa kama wewe siku zote unataka kuishi kama mtu asiyeolewa, kamwe hutaweza kukaa na huyo bwana. na hili ninahisi linajitokeza ktk wewe kuto kuaminiwa, siyo tu hakuamini bali wewe hutaki kuishi kama "mama aliye olewa"
 
dada yangu, unaposema ndoa kumbuka kuwa kuna changamoto zake!kusoma na kupata degree na kazi nzuri si kigezo cha kuvunja ndoa!pamoja na kumueleza yote unayotaka kufanyiwa, nakushauri pia ujitathmini ni kipi kinachomfanya kutoka kwako ahame chumba na kurudi usiku.mara nyingi huwa tunapenda kuwanyooshea wengine vidole kuwa wana makosa huku ya kwetu tukiyaziba yasionekane.umesema ndoa ni ya kanisa-je mmekuwa na maombi mfano ya pamoja na ya kwako mwenyewe ukimwombea mumeo??au tu kwa sababu uliolewa kanisani basi. nafikiri una wajibu wa kufanya kuilinda nyumba yako.pengine pia nikuulize dhamira yako ilikuwa ni nini wakati mnaoana?kuachana mbele ya safari au kuishi pamoja katika shida na raha??ushauri:
  • Zungumza nae;
  • ondoa kiburi na mambo yasiyofaa unayomfanyia mumeo ambayo hayapendi;
  • mwombee kwa Mungu(Mungu asipolinda nyumba alindae hulinda bure);
  • timiza ndoto zako ambazo ulikuwa nazo wakati wa uchumba na ndoa-
  • tafuta kuwa na ndoa yenye mafanikio-(to run awaya from the problem is not the way of solving the problem).watu makini hutafuta suluhisho......
aaaaaaaghhh!!!!... dadamnyonge pole sana, unasubiri mpaka upate pressure na ukiwa hoi ndo utoke, kwani unaishi wapi?? ebu weka namba yako ya simu apo, maisha yenyewe mafupi kwani hujui life span yetu bongo inaelekea miaka 50?? akseh achana na uyo babu, na unazidi kuchelewa malavidavi ya ukweli, achana nae uyo asojua kupenda, hajafundwa uyo, natumai uyo mumeo atakuwa ni mkulya
 
sitaki kuamini sana nilichokisoma., Nafikiri huyu mwanaume sio kichaa, yani ana akili timamu na isitoshe ana dini pia. Wawezaje kumfanyia binadamu mwenzio hayo, tena mkeo PASIPO SABABU ZA MSINGI.....!!! Hainiingii akilini kabisaaaaa. Nafikiri Dada Mnyonge kuna kitu hapa ambacho haujatuweka wazi. Imagine mmekaa miaka 4, mmesindwa hata kupata mtoto si kwamba mna tatizo bali tu kwa sababu ooh mara leo umerudishwa kwenu, oooh leo karudi saa tisa ooh kahama chumba... Jamani kweli.. Sasa hapo mnajenga familia ya aina gani! Aisee fungua akili yako bana , TAMBUA UDHAIFU WAKO...naamini upo coz hakuna binadamu aliyekamilika kama unahusika kwa namna moja au nyingine kumfanya a behave hivyo ujirekebishe. By the way, je mumeo alikuwa hivi wakati wa mahusiano au ndo amebadilika sasa! Au ndo ndoa ilikuwa ya faster faster kwa hiyo mahusiano yalikuwa ya muda sana, na hivyo vijisenti vyake labda vikakuvutia... na ndoa tena haya ukajikuta tayari umo ndani.
 
umewashirikisha wazee?kabla ya kuja huku kwanza ungeanza huko,labda usingeweka huu uzi!hustahili kuteseka hivyo,tena umesoma unakila sababu ya kuwa na amani na furaha,wazee wakishindwa nenda kamsemee kanisani,ikishindikana chapa lapa ila nimependa uvumilivu wako
 
Jichunguze mwenyewe kama sio chanzo cha mambo hayo. Isije kuwa akija home unamkera badala ya kumfurahisha akaamua kwenda nje.
Inaonekana unampenda ndio maana bado upo, na yeye anakupenda ndio maana anakufuata baada ya kukutimua.
Kaeni chini peke yenu muelezane kwa kina sababu ya mabadiliko. Ikishindikana andika hasara ondoka! Tena bila kuangalia nyuma
 
hilo jina kwa kweli linaonyesha u myonge sana pole kwa misuko suko iliyokupata
  1. je mmebahatika kupata watoto , wangapi??
  2. je anatabia ya ulevi??
  3. umehjaribu kushirikisha watu wa karibu??
  4. ulipokuwa unaongea nae alikuwa anaonyesha kuelewa usemacho??
yote ayo ya nini?? achana na shombo la uyo kizee na anakupotezea mda, natmai mpaka apo ushagundua kuwa huna mume bali umegeuzwa house girl, wewe tayari ni mseja tu, ingia mtaani bahati yako unazidi kuichelewesha mwenyewe
 
Samahani kidogo, kama tukimpata huyu mwenza wako na kumuuliza aseme kuhusu wewe na anavyoona unafikiri atatuambia nini kuhusu kiini cha tatizo?

mwanakijiji hapo umesema sahihi kabisa, maana isije watu tukaanza kumlaani huyo mwanaume kumbe usikute kuna kitu kikubwa zaidi, mfano jaribio la kuua, kufumaniwa nk.. Naunga mkono kabisa wazo la mwanakijiji.
 
tatizo tunapenda kulalamika kuonewa pasipo kujichunguza

Wanawake wengi kabla ya kulalamika hujichunguza na wengi hujilaumu kwa makosa wafanyiwao na waume zao! Na since Adam ni Bishanga tu ndiye anaye kubali pale anapokosea; wengine wote hukosea kwa sababu au wanawake wamefanya hili au hawakufanya (kutimiza wajibu)!
 
Dada mnyonge uwe serious PIGA CHINI uyo babuyo baradhuli pia hafai, yaani tunavyowachukulia wenzi wetu (wanawake) ni kuwaweka safi, kuwalisha pia kuwapendezesha ili mda wote awe mpya kwako ata katika mambo ya toDo dah goli kadhaa lzm umpe, lakini wewe ata chumbani sjui kakukimbiza au kakukimbia?? siku moja atakudedisha kwani kwa matendo yake, hakupendi uyo, anakuweka chini zaidi ya dekio, pia haouse girl
 
mwanakijiji hapo umesema sahihi kabisa, maana isije watu tukaanza kumlaani huyo mwanaume kumbe usikute kuna kitu kikubwa zaidi, mfano jaribio la kuua, kufumaniwa nk.. Naunga mkono kabisa wazo la mwanakijiji.

mdau,nadhan hujaelewa maelezo yangu vzr.hajawah kunifumania zaid ya kuhis tu fulan au fulan hata kwa
kusalimiana tu.hatak niwe karibu na rafk yyt tangu
nasoma,kila mtu alimuona hafai .na km nngetaka kuua
cdhan km tungekuwa nyumba moja had muda huu.
kuna wenza wanafanya mambo makubwa zaid ila husameheana na maisha huendelea,n lip hilo baya kuliko lote ntakuwa nmetenda lisiweze samehewa?
ckatai cwez nkawa perfect lazma nna mapungufu yangu,je wote waishio kwa aman ktk ndoa zao hawana mapungufu na hawagomban?mbona hawatendw hv!
 
Mi nahis anawaza mtoto sana, ukimzalia mtoto atatulia na mapenzi yatarudi....Kuna ndoa moja ilikua kama hivyo lakini baada ya jamaa kubambikiziwa mtoto alitulia na mapenzi yakarudi kama zamani INGAWA ALIDANGANYWA....
 
ktk haya maandishi yako inaonekana bado kuna vitu vingi umevificha. mpaka mtu akahama chumba kulikuwa na sababu. sababu hii yaweza kuwa ni wewe , au mumeo mwenyewe.

utaweza kusaidiwa vizuri ikiwa utaweza kwanza kueleza makosa yote ambayo wewe umeyafanya. nahayo aliyo fanya mumeo. sisemi wewe unamakosa peke yako, lakini ninatia mashaka juu ya huyu mtu kugeuka kwa kiwango hiki. kuna mahali wewe huenda ulikosea na unadhani yeye hajui, au anajua na hujaonyesha nia ya dhati ya kujuta na kutubu kosa lako.ndiyo maana sasa anakuona hufai tena na huaminiki tena

kwa upande wake huenda kanusa mahali pazuri huko nje, sasa ni kama anajutia uamuzi wa kukuoa wewe, sasa anakufukuza lakini akiwaza anaona una umuhimu fulani. hapa hata sababu ya kukosa mtoto inaweza kuwa nio chanzo cha vurugu.

USHAURI

ndoa inafanyika kwa mwenye jinsia ya kike na jinsia ya kiume, na inakamilika kwa tendo la ndoa. kama wewe hupewi tendo la ndoa , na mnalala chumba tofauti unaweza kufanya haya yafuatayo
1. kama wewe unampenda sana mume wako na ungependa kuibeba hiyo hali waweza msamehe tu na uishi tu nae
2. kama unaona nhiyo hali haifai kwako na haivumiliki basi usiogope eti ndoa haivunjiki, kwa hiyo tafsiri ya ndoa hapo juu, ukiweza kulithibitishia kanisa kuwa hupati tendo la ndoa na munalala nae chumba tofauti kanisa lita tengua hiyo ndoa
3. unasema mumeo akisikia maneno tu anakutuhumu. hapo nadhani wewe unamatatizo, kwanini wewe unaingia ingia tu kwenye maneno ilihali unajua kuwa mwenzio anawivu?. jiangalie, ndoa ni kujitoa kwa mwenzio. kama unajua kuwa mwenzio anawivu , basi achana na mawasiliano tata , au kujiweka ktk mazingira yanayokufanya utiliwe mashaka.
4. wakati unawaza hayo 1-3 hapo juu, kumbuka siku ulipoolewa ulipoteza sehemu ya uhuru wako, na yeye ( mumeo ) alipoteza sehemu ya uhuru wake. sasa kama wewe siku zote unataka kuishi kama mtu asiyeolewa, kamwe hutaweza kukaa na huyo bwana. na hili ninahisi linajitokeza ktk wewe kuto kuaminiwa, siyo tu hakuamini bali wewe hutaki kuishi kama "mama aliye olewa"

UKO SAHIHI SANA MKUU...... :eyebrows:
 
Back
Top Bottom