Nimwache akapange au niondoke mimi?

Nimwache akapange au niondoke mimi?

Mtoto wa jinsia gani Mkuu? Maana hata akikataa mtoto kukupa kama kiumeni atajipeleka mwenyewe kwa bibiake mzaa wewe ila kama wa kike mchukue faster asije kudapt upuuzi wa mamake.

Kaka wewe nadhani ni malaika na sijui kama kuna malaika mvumilivu kama wewe. Sisi wakristo biblia inasema wazi kuwa ukimhubiria mtu au kumuonya na asisikie maneno yako basi simama kung'uta mavumbi uende zako. Naomba simama kama mwanamme acha kutudhalilisha Mkuu. Na ungekuwa karibu ningekupa ya uso ili nizibue akili yako labda imekaa vibaya
 
Wakati wengine unatamani upate mwanaume wa kukuweka huru kwa wazazi na kukupenda kwa dhati.
Kuna wanawake wengine sijui ndokuzoea kudanga. Anatamani akapange Ili adange.
Mchukue mwanao na utapata mwanamke wa kumlea Vizuri tu Mbona.
Kuna wanawake wenye roho nzuri atamlea Kama mwanaye tu Mbona. Mwache hapo we Nenda kaanze Maisha mapya.
Dada nimekupenda bure kabisa kwa ushauri wako. Huyo mkaka akipata mwanamke mwenye sifa za mwanamke naamini watafika mbali sana

Wanaume wa hivyo sijui wapo wangapi kwa sasa hapa duniani
 
story ni ndefu sana,ila kwa kifupi tu,fikiria kumuacha huyo mwanamke aende zake,vinginevyo utapata taabu sana
 
Kuondoka anasema mpaka mwakani, mimi nimechoka sana na nikimwona najawa na hasira sana kiasi kwamba huwa naondoka tu home na kwenda matembezi yangu sometimes naenda kulewa. I am so stressed kiasi kwamba sitaki ugomvi kabisa


Pole sana kwa majanga unayopambana nayo. Simama kwenye nafasi yako kama mwanaume. Jeuri analeta yeye pia masharti ya kutengana anafanya yeye, Alishakuona bwege ndiyo maana anakusumbua. Nakushauri amua siku moja bila kumpa notice tena kwa kumaanisha na usirudi nyumba. Atakuuwa kwa pressure huyo.
 
Kum.a.mae wallahi we jamaa hizo sio akili zako ushatengenezwa kitambo tu!!
 
Dada nimekupenda bure kabisa kwa ushauri wako. Huyo mkaka akipata mwanamke mwenye sifa za mwanamke naamini watafika mbali sana

Wanaume wa hivyo sijui wapo wangapi kwa sasa hapa duniani
Mimi Nahisi kabaki peke yake tu
 
Pole mkuu, bado una muda wa kuanza upya,achana nae uyo kabisa!,ukimng'ang'ania utakuja kujidhuru kwa anayokufanyia.
 
Kwa hizo tabia inaonesha yeye ndo alikuwa anamnyanyasa dadake. Mwachie kila kitu, we sepa kaanze upya. Mwanao akikua mfate umuweke Boarding school mana pesa unazo.
 
Habari wanaJF, naomba mnishauri pia kwa hili.

Nilikutana na binti mmoja mwaka 2012 katika mazingira ya kazini na tukaingia katika mahusiano, binti huyo alikuwa akiishi kwa dada yake mkubwa ambaye wamechangia mama. Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba dada yake huyo alikuwa akimnyanyasa na kitendo kile kiliniuma sana nikaamua kumpangishia chumba akaanza maisha yake hapo, hiyo ilikuwa ni 2013. Tuliendelea na mahusiano mpaka niliamua kujitegemea mwaka 2015 na tangu mwanzo wa mahusiano yetu alikuwa akija mpaka nyumbani kwetu na ndugu zangu wote wanamfahamu. Aliamua kuja kuishi na mimi hivyo nilimkaribisha tukaishi wote, sasa hapa ndo matatizo yakaanza.

Alianza kuzua migogoro ndani na hatukuwa tunaelewana mara nyingi, nilikuwa na biashara nikamweka asimamie biashara ile nilikuwa najua inaingiza kiasi gani lakini tangu aanze kusimamia iliyumba na hakuwa ananishirikisha mauzo ya siku. mostly jibu lake lilikuwa biashara mdogo mdogo, mwaka huo huo akashika mimba na Mungu akajalia akajifungua 2016 March, kipindi hicho nilikumbwa na mtikisiko mkubwa kiuchumi hivyo hali haikuwa nzuri. Katika maisha yetu alikuwa ni mtu wa kufanya maamuzi peke yake na nikijaribu kuhoji inakuwa ugomvi nikaamua kukaa kimya kuepusha shari. Hivyo aliwaleta ndugu zake kuishi kwangu bila idhini yangu maana hali ya uchumi ilikuwa si nzuri. Akaanza kulaumu kuwa ndugu zangu wanamchukia ilhali yeye alikuwa akienda kwetu hafanyi chochote ni kuketi tu muda mwingine hamsemeshi mtu anakuwa busy na simu yake. Tukitoka anaanza kutupa lawama kwangu kwamba ndugu zangu na mama yangu hawampendi. Nilijaribu kumwelewesha na kumwambia kuwa mama hapendezwi na tabia ya yeye kujitenga maana kama anahitaji kuolewa na mimi lazima achangamane na familia yangu lakini haikufua dafu. Hali hiyo iliendelea hata kufikia hatua mama yangu akimpigia simu hapokei kwa makusudi, nikimuuliza anasema hajisikii kuzungumza na simu, mama akipiga kwangu nikimpa pia jibu ni lile lile.

Hali hiyo ilinitesa sana maana nikiangalia maisha yake ya nyuma napata ugumu kumuacha maana namsikitikia mwanangu atateseka sana. Nilifanikiwa kupata kazi nyingine hapa Dar na kuhamia hapa mwaka 2017 July, nilianza kazi vizuri na nikawa natuma pesa za kutumia kama kawaida nilikuwa nikituma laki 2 kila mwezi kwa ajiri ya matumizi, na biashara ile ilikuwa ikiendelea kama kawaida japo sikuwahi kujua mapato yake kabisa. Cha kushangaza ni kwamba kila baada ya wiki mbili niliambiwa hakuna pesa ya kutumia na hakuna chakula mtoto hana chakula pia, ilinibidi nitoe pesa yangu ya kujikimu niitume kwao kitu ambacho kiliendea kuwa hivyo kwa muda wa miezi 5. Wakati mwingine sikuwa na pesa kabisa kwa sababu ya matumizi kwake kuwa mengi na nilijaribu kuhoji pesa inatumika vipi ilizua mgogoro sana. Na alikuwa mtu wa kulalamika na kunitumia sms za matusi[Zipo Zote] kunitukana lakini sikuangalia hayo maana imani yangu ilikuwa ni kujenga familia na huyo dada. Mwaka jana mwezi wa 12 nilimwambia ajiandae ahamie huku hivyo vitu vyote nikampa melekezo avipeleke kwa mama yangu na ndivyo tulivyokubaliana. Nilituma pesa ya nauli Tshs 210,000/= Kwa ajili ya safari (100,000/=) na kumalizia kodi ya nyumba (100,000/=) lakini huwezi amini kabla ya siku moja safari kuanza aliniambia kuwa hana pesa ya nauli nimtumie nauli.

Nilishikwa na hasira sana na tayari nyumba niliwambia wakabidhi kwa mwenyewe, Vitu aliamua kuita ndugu zake wakaja kuchukua bila kunishirikisha. Nilipigiwa simu na mdogo wangu akiniambia mbona mambo yako tofauti na mlivyopanga? kwa hekima niliwaambia wadogo zangu waondoke tu lakini pia haikutosha ndugu zake na huyo dada walianza kuwamwagia wadogo zangu matusi kiasi cha kushangaa kuna nini mpaka iwe hivyo. Nilimpigia huyo dada na kumuuliza kuhusu tukio hilo niliambulia matusi ya ajabu sana na hapo nimetoa tena pesa nyingine ya nauli ili tu mwanangu awe karibu yangu.

Nikajisemea kuwa akifika nitamhoji anieleze vizuri, lakini alipofika alikuwa ni mtu mwenye maneno mengi sana na matusi makali, niliamua kuachana nayo hayo na kufungua ukurasa mwingine wa maisha (Kumsamehe). Tukaishi maisha ambayo kila siku anazua jambo, wakati mwingine namsalimu haitikii, namsemesha hajibu ikafika wakati nikaamua kumtizama tu. Nilipanga niende kwao kutoa mahali mwezi wa 11 mwaka huu lakini kwa tabia hizi sidhani kama naweza. NImeshajaribu kuzungumza naye, kumshirikisha mchungaji wa kanisa analosali, kwa muda fulani nikaona mabadiliko lakini hali ilirudi vile vile. Ilifika kipindi nimetoka kazini nikamkuta ndugu yake kaja kumsalimu, kabla sijaingia ndani nilisikiwa wakinizugumza vibaya sana. Nilichukia sana lakini nikamwambia Mungu kwamba ikiwa mimi ndiye nimemfanya mtu huyu awe hapa sina haja ya kuchukia kwa hiki anachonena kuhusu mimi. Niliingia ndani nikabadili nguo zangu na kutoka kwenda matembezi.

Hivi karibuni kuna ndugu yangu alikuwa anaolewa huko kanda ya ziwa, nikamwambia huyo dada apige hesabu ya mahitaji yake na mtoto kwa ajili ya harusi. Alinipa hesabu yake nikasema sawa ilikuwa around 200K nikatafuta pesa Mungu akajalia nikapata 1M nikamwambia kuna pesa hii imepatikana so wajiandae kwa ajili ya kwenda kwenye harusi. Tulipanga kwenda kufanya shopping the next day. Tulikwenda kariakoo kuanza shopping, cha ajabu yale aliyopanga kununua nikaona anatafuta nguo za mama yake (Kitu ambacho hakuwa amenishirikisha na ilikuwa nje ya budget) nilikaa kimya nikamnunulia mwanangu, yeye alipomaliza kununua alivyokuwa ananunua akanambia anahitaji pesa ya kujinunulia yeye pia.

Seriously nilishikwa na hasira sana maana haikuwa katika budget, na ukizingatia tunakwenda kwa siku chache tu na hatukupanga kufanya yote hayo maana kulikuwa na mambo mengine ya muhumi ya kufanya baada yakurudi dar. Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwangu maana aliongea maneno makali sana kiasi kwamba nikashikwa hasira nikampa hiyo pesa aliyohitaji, aliema asante but sikumjibu kabisa. Tulikwenda nikijua tunafikia kwenye tukio lakini kumbe kwake ilikuwa ni tofauti tulipo fika alinambia nimpeleke kwa dada yake, nilifanya kama alivyohitaji. Nikategemea asubuhi atakuja ajishughulishe katika shughuli za tukio hakuonekana simu hapokei mara nakuja baada ya nusu saa mpaka ikafika jioni. Kesho yake nikamwambia ajitahidi kuwahi aje kujumuika na kusaidiana na wenzake lakini alikuja saa nne asubuhi na kunifuata moja kwa moja anaomba pesa aende salon. Sikumpa nilimwambia sina maana tayari alishaniudhi. Akaingia ndani kwamba anakwenda kubadili nguo aje kufanya kazi, kumbe haikuwa hivyo akaondoka kwenda zake salon. Sasa tangu hapo hakukanyaga tena kwetu, mpaka siku ya harusi yenyewe ndo akaonekana tena. Tulijumuika na baada ya sherehe kuisha nilianza maandalizi ya kurudi Dar, siku iliyofuata akaniambia anahitaji kuzungumza na mama yangu, mimi na ndugu zangu nikasema sawa. Akatuita tukaketi kumsikiliza akaomba msamaha wa kilichotokea na kuhusu matusi yaliyotukanwa kwenye sakata la vitu na mengine mengi wakamsikiliza na wakamwambia wao hawana tatizo kabisa, akanaambia nimsindikize kwenda kwa dada yake nikamsindikiza.

Huko njiani alinitolea maneno makali sana nikajiuliza kwamba huo msamaha aliokuwa akiomba alimaanisha nini? au alikuwa akiwajaribu ndugu zangu na mama yangu? sikutaka mengi wala sikujibu kitu nikamfikisha nikaondoka. Sasa mwezi huu ilikuwa niende kwao nikatoe mahali lakini moyo wangu sasa haumuhitaji tena maana naona tunakoenda nitafanya kitu cha ajabu juu yake kinachoniumiza ni mwanangu tu.

Nilimweleza kuhusu kuachana mimi na yeye akasema ataenda kupanga chumba hapa hapa Dar kitu ambacho nikifikiria mazingira hayo kwa mwanangu siyo kabisa, naombeni ushauri wenu nifanyeje? maana jambo hili limenichosha sana. binti ni mzuri but tabia zimenishinda
Ushauri unatolewa baada ya kusikiliza malalamiko ya pande zote mbili... hapa utaambiwa yale tu unayotaka uambiwe most of which yanaweza umiza upande wa pili.., kwa maelezo yako kwa hali ya kawaida haiwezekani kuishi na mwanamke wa aina hiyo from the begining... lakini wewe umeweza na bado unaendelea kuweza kitu kinachonifanya nipate mashaka na ukweli wa maneno yako.
 
Aisee we ni mmoja kati ya wanaume wavumilivu sana...mm nisingeweza kukaa na mwanamke wa aina hyo hata kdgo...mm nilikuwa na maswaiba kama yako ingawa yako yamezid kidogo..nilichofanya,nilimwacha mtoto kwa mama ake..baada ya kufikia umri wa kuanza masomo nikampeleka boarding school...problem solved
 
Kosa la kwanza ulilofanya ni kukubali awe mke wako, na hili ni kosa la wote waliokubali kuoa au kuolewa, kosa la pili ni hilo la kumwacha unalotaka kufanya. Naomba ufahamu mambo haya matatu kuhusu aina za watu katika kila mgogoro unaotokea, 1. kuna watu wanaoepuka migogoro kwa kuipuuza au kuiona ni kitu kidogo tu na kuifanya kama haipo, 2. Kuna wanaotafuta ushindi katika kila mgogoro unaotokea kwa kufanya yafuatayo, kushambulia kwa maneno mengi na makali, kulia nk, 3. Kuna wanaotafuta suluhu kwenye kila mgogoro unaotokea kwa kuangalia wamechangiaje kusababisha mgogoro uliyotokea na kuomba msamaha au kutoa msamaha. Ndugu kwa maelezo yako, naona wewe ni aina ya watu wanaoepuka migogoro kwa kuipuuza na kuifanya kama ni kitu kidogo tu, halafu mbaya zaidi mke wako ni aina ya watu wanaotafuta ushindi katika kila mgogoro kati yenu. Maoni yangu; kwa aina yenu ninyi wawili hamtawahi fanya maendeleo makubwa ya maisha yenu ingawa uwezo mnao, kwa aina yako mwanaume ya kuepuka migogoro mke wako atakuongoza na kukutawala kwa kuwa yeye ni aina ya watu wanaotafuta ushindi katika kila migogoro na wewe utakubali tu yaishe ili maisha yaendele. Ushauri wangu, tafakari zaidi kuhusu mwenendo wenu na wajibu wako katika nyumba yako kwani kila kichwa na mwanamke ni mwanaume. Mungu alikuumba uwe kiongozi kwa mkeo na watoto wako na mkeo awe msaidizi wako, usipokuwa mwangalifu utakuwa msaidizi na mkeo atakuongoza. Ukipenda tuongee zaidi ni follow ndugu.
 
Mkuu hapa wa kulaumiwa ni wewe kwa sababu kwa tabia zake ulikua unatakiwa kumuacha 2017 mwanzoni kabsa ila hukuchukua hatua.

Gunia la misumari halibebwi kichwani
 
Sasa amerudi yupo hapa kwangu nilimwambi tuachane anadai nimpe muda ajipange ataenda kujitegemea, but mimi ninafikiria kuondoka tu nimwachie kila kitu nikaanze maisha yangu upya
WEWE JAMAA UMELOGWA WEWE...MPUMBAVU MKUBWA WEWE...

SIDHANI KAMA WEWE NI MWANAUME HALISI...

ETI NIMWACHIE VITU VYOTE NIKAANZE...KWANZA UMEMUOA...? WEWE JAMAA HELA UNATOA TU HUNA SHIDA...HELA ZISIZOKUWA NA MAELEZO YA KUTOSHA UNATOA TU...WEWE NI MPUMBAVU...ETY NIMWACHIE VITU NIENDE...YEYE HAPO HANA CHA KUMILIKI...HATA MTOTO NI WAKO...CHUKUA ISHI NAE HATA KWA MAMA AKO ATABARIKIWA...HILO SHETANI ACHANA NALO...

SASA NIKUAMBIE TU UKWELI...
NAFAHAMU UNAWASAIDIA SANA NDUGU ZAKO...

ILA UKWELI NI KWAMBA WAZAZI NA NDUGU ZAKO WASHAKUONA ZEZETA...NA WANATAMANI KUKUAMBIA UKWELI WEWE NI ZEZETA KWA HUYO MWANAMKE...ILA WAKIKUAMBIA HUENDA UKAMIND UKAKATA HUDUMA BURE..

ILA WEWE HUWEZI KUWA MWANAUME...ETY UNAVUMILIA YOTE HAYO...
 
Kosa la kwanza ulilofanya ni kukubali awe mke wako, na hili ni kosa la wote waliokubali kuoa au kuolewa, kosa la pili ni hilo la kumwacha unalotaka kufanya. Naomba ufahamu mambo haya matatu kuhusu aina za watu katika kila mgogoro unaotokea, 1. kuna watu wanaoepuka migogoro kwa kuipuuza au kuiona ni kitu kidogo tu na kuifanya kama haipo, 2. Kuna wanaotafuta ushindi katika kila mgogoro unaotokea kwa kufanya yafuatayo, kushambulia kwa maneno mengi na makali, kulia nk, 3. Kuna wanaotafuta suluhu kwenye kila mgogoro unaotokea kwa kuangalia wamechangiaje kusababisha mgogoro uliyotokea na kuomba msamaha au kutoa msamaha. Ndugu kwa maelezo yako, naona wewe ni aina ya watu wanaoepuka migogoro kwa kuipuuza na kuifanya kama ni kitu kidogo tu, halafu mbaya zaidi mke wako ni aina ya watu wanaotafuta ushindi katika kila mgogoro kati yenu. Maoni yangu; kwa aina yenu ninyi wawili hamtawahi fanya maendeleo makubwa ya maisha yenu ingawa uwezo mnao, kwa aina yako mwanaume ya kuepuka migogoro mke wako atakuongoza na kukutawala kwa kuwa yeye ni aina ya watu wanaotafuta ushindi katika kila migogoro na wewe utakubali tu yaishe ili maisha yaendele. Ushauri wangu, tafakari zaidi kuhusu mwenendo wenu na wajibu wako katika nyumba yako kwani kila kichwa na mwanamke ni mwanaume. Mungu alikuumba uwe kiongozi kwa mkeo na watoto wako na mkeo awe msaidizi wako, usipokuwa mwangalifu utakuwa msaidizi na mkeo atakuongoza. Ukipenda tuongee zaidi ni follow ndugu.
Ktk yotee uliyoandika mm naona yanavulika isipokuwa 1yaan anakataa kupokea cmu ya mamayako mzazi tena hata akikupigia no yako hataki kuongea nae nani kama mama ktk dunia hii ukubali mama yako mzazi azereleuliwe ati kwa sababu ya mtt kwan huyo mtt hawezi kulelewa na mt mwingine je akifa itakuwaje umekosea sana na ulikosea kuendelea nae cku tu alipoanza kumzereu mama yako nataman nikutafutie tusi hapa lkn naogopa mkuu
 
Jinga kabisa wewe...unatuaibisha wenzio.....cha kufanya kama unamuonea mwanao huruma, mwache huyo mwanamke na mtoto hapo nyumbani ...timua zako tafuta ustaarabu mwengine..ila matunzo endelea nayo yale yanayoeleweka tu.
 
Back
Top Bottom