Nina 10M nahitaji kufuga Samaki naombeni ushauri

Tumbili

Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
52
Reaction score
56
Hi wadau wa JF. Mimi nina kamtaji kwangu kadogo kama 10M, uku nikiwa na 5M kama back up plan. Nataka nifanye biashara ya kufuga Samaki kitaalam, eneo ninalo Kigamboni kisarawe II zaidi ya heka tano.

Je kwa mtaji huo wa 10M + 5M ya back up biashara hiyo inafanyika?...., je aina gani ya Samaki natakiwa niwafuge?. Naombeni muongozo manake mie ni mgeni kabisa kwenye biashara hiyo japokuwa nina uzoefu mkubwa sana kwenye biashara nyingine.

Nawakaribisha wadau.
 
Ulipo hapo kuna maji ya chumvi au baridi kwanza tuanzie hapa.
 
Ni Perege Mzee baba.
Tatizo mpaka sasa nina eneo na pesa hata bwawa bado sijachimba na wala sina utaalam wowote.

Kwanza nataka jua kwa mtaji huo wa 10M + 5M unatosha kuanzisha biashara hiyo from scratch, kwani eneo ninalo tayari.

Pili nataka nijue nini natakiwa kufanya?, kama kuna consultant wa kumuona etc.

Kwakifupi naomba ushauri jinsi ya kuifanya hiyo biashara kwa mtu mwenye mtaji huo, na eneo from scratch.
 
Ni Perege Mzee baba.
Perege niliwahi kuwafuga...faida yao
-Wanazaliana saana.
-Ni wadogo hawawi wakubwa kama sato n.k
-Chakula chao sio kingi (gharama). wanakula hata mabaki ya vyakula.

Changamoto.
-predators( hapa unaweza kurudi ukakuta nusu wa samaki wanaelea kwenye maji).
-walizaliana wakawa wengi kuliko bwawa.. njiandae kwa backup.
-kuna nyasi sio rafiki kwa samaki(usafi wa Bwawa kuwa nao makini).
-mbegu... uwe unasafisha bwawa kila baada ya muda na kuingiza mbegu mpya.

napenda saana hii kitu.....nafanya namna nirudie... hata kama sio biashara basi kwa Nyumbani


maji ya chumvi na baridi hili nalo kubwa.

sikia...Kila kata ina Mabwana samaki mtafute mfanye rafiki atakusaidia vya kutosha.

lakini zingatia yafuatayo.

kwanza, kiasi cha mtaji kinategemea ukubwa wa mradi. na kwa maoni yangu huo mtaji ni tosha kabisa.

pili, eneo la kufugia... sio kila eneo ni rafiki kwa ufugaji wa samaki. udongo. kuna udongo ambao ni mzuri kwa maji na kwa samaki wenyewe... wataalam watauchunguza kisha watakuambia. kwa uzoefu wangu samaki hawapendi mchanga au lile tope zito.

tatu, upatikanaji wa Maji. hili ndilo la Muhimu nalo. samaki wanhitaji maji. na yawepo muda wote yamejaa bwawani. bwawa hakikisha linakuwepo karibu na vyanzo au pembezoni mwa maji yasiyo ya msimu.

pia kuwa makini na mvua inaweza kujaza bwawa kesho ukakuta hauna samaki wamesombwa na mafuriko.

nne, Samaki wanaoshuriwa kufungwa ni sato, kambale na perege. mimi nilifuga na naweza kusema bado wapo perege sema tofauti mimi sio biashara. hawa wanashauriwa na wataalamu maana wanahimili kuwekwa kwenye mabwawa.

unapochimba bwawa hakikisha unazingatia makazi ya samaki, tunnel za kuingizia na kusafishia maji ya bwawa na mambo utakayoelekezwa na mtaalam. kwa uchache.
 
pesa inatosha hiyo.... niliona kuna jamaa humu anatoa hii huduma kuna uzi wake alianzisha.

upo mkoa gani?
 
Mimi naomba nikushauri hivi kama utaweza nina rafiki yangu anafanya cage fish farming na aliniambia kuna maeneo yamewekwa kwa ajili hiyo na kibali ni bure kabisa.

Uzuri wa njia tajwa hapo juu wewe ni kuandaa cages,kununua vifaranga na chakula kwani wanategemea hicho chakula.

Uangalizi tu ni kwamba investment cost inarudi kuanzia miaka 5+ lakini hela ya uendeshaji isiporudi ndani ya cycle husika jitafakari.
 
Kwa mtaji wako unaweza kuanza kufanya mradi huo kama eneo unalo la kutosha na upatikanaji wa maji ni mzuri(maji baridi),..kwa kuwa unaanza gharama lazima iwe kubwa japo ukiweza kukamilisha faida yake ni nono huko mbeleni..

NB:tumia "cage system" mambo yatakuwa "wow".
 
Daby


Mkuu nashukuru sana kwa maelezo unayonipa. Eneo lipo Kigamboni kisarawe II. Kusema ukweli nataka kuifanya issue kitaalam kidogo.

Nashukuru kwa kunambia kuwa kila kata kuna bwana samaki embu ngoja nifuatilie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…