Perege niliwahi kuwafuga...faida yao
-Wanazaliana saana.
-Ni wadogo hawawi wakubwa kama sato n.k
-Chakula chao sio kingi (gharama). wanakula hata mabaki ya vyakula.
Changamoto.
-predators( hapa unaweza kurudi ukakuta nusu wa samaki wanaelea kwenye maji).
-walizaliana wakawa wengi kuliko bwawa.. njiandae kwa backup.
-kuna nyasi sio rafiki kwa samaki(usafi wa Bwawa kuwa nao makini).
-mbegu... uwe unasafisha bwawa kila baada ya muda na kuingiza mbegu mpya.
napenda saana hii kitu.....nafanya namna nirudie... hata kama sio biashara basi kwa Nyumbani
maji ya chumvi na baridi hili nalo kubwa.
sikia...Kila kata ina Mabwana samaki mtafute mfanye rafiki atakusaidia vya kutosha.
lakini zingatia yafuatayo.
kwanza, kiasi cha mtaji kinategemea ukubwa wa mradi. na kwa maoni yangu huo mtaji ni tosha kabisa.
pili, eneo la kufugia... sio kila eneo ni rafiki kwa ufugaji wa samaki. udongo. kuna udongo ambao ni mzuri kwa maji na kwa samaki wenyewe... wataalam watauchunguza kisha watakuambia. kwa uzoefu wangu samaki hawapendi mchanga au lile tope zito.
tatu, upatikanaji wa Maji. hili ndilo la Muhimu nalo. samaki wanhitaji maji. na yawepo muda wote yamejaa bwawani. bwawa hakikisha linakuwepo karibu na vyanzo au pembezoni mwa maji yasiyo ya msimu.
pia kuwa makini na mvua inaweza kujaza bwawa kesho ukakuta hauna samaki wamesombwa na mafuriko.
nne, Samaki wanaoshuriwa kufungwa ni sato, kambale na perege. mimi nilifuga na naweza kusema bado wapo perege sema tofauti mimi sio biashara. hawa wanashauriwa na wataalamu maana wanahimili kuwekwa kwenye mabwawa.
unapochimba bwawa hakikisha unazingatia makazi ya samaki, tunnel za kuingizia na kusafishia maji ya bwawa na mambo utakayoelekezwa na mtaalam. kwa uchache.