Nina 40M ninunue hisa CRDB, NMB au niwekeze UTT?

Vizia kama thamani itapandaa kuanzia february maana hapo milioni 3.1 ni makato utakaponunua na muda wa kuuza
 
Usinunue hisa crdb, nmb au popote pale. Nin ndg yang aliwekea mamilion lakn mwisho wa mwaka faida haikuzidi laki mbil. Sasa kwaiy fedha yako sikushauri
Faida inategemea na kiasi ulichowekeza
 
1. Chukua milioni 15 nunua hisa CRDB
2. Milioni 10 nunua I trust ETF ni buku kwa hisa ipo stage ya IPO na itakua listed kwenye DSE market january.
3. Chukua milioni 15 weka UTT

Tulia miaka miwili rudi angalia faida.

Then utaamua namna ya kuzidi kuchanganya hiyo mitaji....

Low risk vs high risk....
Umri unapozidi kwenda punguza high risk na uwekeze kwenye low risk.
 
ndugu, upo uwekezaji zaidi huo ulioutaja. upo ununzi wa HATIFUNGANI ZA SERIKALI, zipo Money Market Fund mbalimbali, uwekezaji kwenye REAL ESTATE.

ushauri wangu: PELEKA AKIBA HIYO kwenye HATI FUNGANI KWA USALAMA WA FEDHA ZAKO.

Endapo utafanikiwa kupata hatifungani ya miaka 25 na coupon ya asilimia 15, unao uhakika wa kuvuna Tshs MILIONI SITA KILA MWAKA. Mwishoni mwa mwaka wa kwanza fedha zako zitaongezeka na kufikia 46,000,000.

endapo fedha hizi utazipeleka kwenye HISA, itategemea na performance ya kampuni ulikowekeza. kwa mfano Hisa zikishuka na thamani ya fedha zako inashuka. Hisa za NMB kwa leo ni Tshs 8330 na CRDB 1340. Kwa 40M utapata hisa 4,801 NMB na hisa 29,850. Endapo hisa hizo zitashuka hata kwa 1% tayari 40M imepungua hivyo biashara ya hisa inazo hatari nyingi zaidi kuliko HATIFUNGANI (Tresury Bonds). Aidha, endapo bei ya hisa sokoni itapanda, utaongeza fedha zako pia.

Chaguo ni lako.
 
Kama ni mzee wa miaka 55 kwenda mbele aweke hati fungani.

Kama ni kijana 45 kwenda chini achanganye uwekezaji hisa na UTT.

40M sio nyingi za kuweka hatifungani....
 
Usinunue hisa crdb, nmb au popote pale. Nin ndg yang aliwekea mamilion lakn mwisho wa mwaka faida haikuzidi laki mbil. Sasa kwaiy fedha yako sikushauri

Tarehe 18/12/2024 bei ya hisa moja ya CRDB ilikua shilingi 650
Tarehe 18/12/2025 bei ya hisa imekua shilingi 1350

VIS ETF ilipokua IPO ilikua inauzwa 200 lakini leo inauzwa 350

Huyo ndugu yako alinunua hisa za kampuni gani??
 
1. Kwanini kulikuwa /kuna limit ya muda wa kujisajiri wakati watu wanafanya uwekezaji/biashara kila siku?

2. Inamaanisha baada ya huo muda wa kujisajiri ulipopita hawapokei watu wapya?
 
Nenda NBC bank ufungue Fixed Deposit Account uombe wakupe faida ya asilimia 10 kwa mwaka ambayo itakuwa ni milioni 4 toa asilimia 10 kodi ya serikali unabaki na shilingi 3,600,000 kwa mwaka.

Hivyo ina maana kila mwezi benki ya NBC itakuwa inakuwekea kwenye akauti yako shilingi 300,0000 ambayo kama unaona haikutoshi basi tafuta biashara nyingine japo itakuwa na risk kubwa zaidi.

Endapo utaiweka benki kwa zaidi ya mwaka moja labda miaka miwili basi uombe faida ya asilimia 15.
 
Nunua jyabaa kubwa , weka pesa zako huko
 
Hapa sijaelewa, yaani kuna uwezakano wa "kuomba asilimia fulani ya faida kwenye mabenki" na wakakubali? Mnakaa mnajadiliana kwamba naweka hela yangu fixed deposit lakini "nataka" mnipe asilimia fulani kwa mwezi/mwaka?
 
2025 still watu wanaweka pesa fixed deposits??
 
Hapa sijaelewa, yaani kuna uwezakano wa "kuomba asilimia fulani ya faida kwenye mabenki" na wakakubali? Mnakaa mnajadiliana kwamba naweka hela yangu fixed deposit lakini "nataka" mnipe asilimia fulani kwa mwezi/mwaka?
Ukisema nataka ni kama una amurisha, kinachofanyika ni majadiliano kisha mnafikia muafaka. Ninazungumzia benki ya NBC kwani ndio nina uzoefu nayo.
 
Ni ya uhakika zaidi labda kuliko njia zingine hizo, ukisoma andiko langu hapo juu ndio utaelewa vizuri zaidi.

UTT wanatoa 12% on average. M-Wekeza 13%, na mifuko ya uwekezaji wa pamoja mingine inatoa around humo humo tena bila withholding tax. Hiyo fixed deposits ina faida gani zaidi kuliko hizi mifuko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…