Kwanza tafakari kwa makini kwanini umepata point 30 ni si 21 au zaidi ya hapo yaani matokeo ya ujumla ya shule yenu yalikuaje ukilinganisha na matokeo yako, pia je ulipata hizo point kwa kuwa ulikuwa husomi kwa bidii, au ulipata point hizo kwa kuwa ulikuwa mtoro darasani (kiujumla angalia sababu zilizokufanya upate hizo point yaani kama wewe mwenyewe ndio ulisababisha kwa kutotumia fursa vizuri au shule uliyosoma haikuwa nzuri n.k). Baada ya hapo sasa angalia hizo sababu kama mojawapo imechangia kisha chukua hatua ya kutafuta sehemu kwa ajili ya kurudia mtihani huku moyoni ukijiwekea ahadi ya ushindi. Lakini kama ulikuwa mtoro nakushauri jaribu kujipanga kwa kufanya mtihani mwakani ila mwaka huu tumia kwa kujiandaa na kurekebisha makosa yako.
Kimsingi elimu ya O-level ni muhimu kuliko elimu zote kama mambo yalikuwa hayapandi vizuri hapa hata huko uendako ngazi za juu utaishia kutumia nguvu kubwa ili ufaulu kumbe mambo mengine uliyapuuzia huku O-level.
Waone waliokutangulia madarasa watakusaidia maana hata kama ukitafuta shule nzuri kama hujapikwa vizuri tangu form one bado utakuwa hujatatua tatizo, wewe waone walimu wazoefu watatumia uzoefu wao kwa kutengeza program za muda mfupi na utaweza kikubwa utambue sababu zilizokufanya upate hizo point na kuzifanyia kazi