Nina Division 4 ya 30..Nataka kurist

Nina Division 4 ya 30..Nataka kurist

Watu kwa kujishaua....!!hmmmm
mibendera fata upepo tu inayoogopa kushushuliwa,isiyojiamini. Kuingia jf inahuu ..mtu tu kujipanga na muda na kwenda na wakati,jf jf..book book!
Mtu tu akili yake kama kichwani ukishindwa kujipanga na kujitambua hata ukisema siendi chooni naogopa kufeli..utafeli tu!

Mwaya dogo pole kwa matokeo mabaya,we anzia form3 shule nzuri na umwombe sana Mungu kuwa unataka kufaulu,pia usome sana. Ukipata shule we jinenee kuwa 'nimekuja kufaulu'kwa imani na uifanyie kazi,LAZIMA UFAULU,wenzako huwa wanafanya hivyo.
 
wala usijali wewe mbona genius? div 4 hapo umefaulu kabisa, apply cbe
 
chakukusaidia kijana nenda ukaanze kidato cha tatu ili ufanye mtihani kama school candidate kwani kurisiti si suluisho
 
ww acha ujinga pia jiheshimu sasa enzi zako ww zinamsadia nin mleta mada?

Jiheshimu wakati unawajibu waliokuzidi. Mmezidi kukremisha mabongo fleva wakati hayawasaidii hata kujifunza hicho kiswahili chenyewe. Mkubwa akiongea kitu anamaanisha punguza ropo kama unatafuta mume
 
Jiheshimu wakati unawajibu waliokuzidi. Mmezidi kukremisha mabongo fleva wakati hayawasaidii hata kujifunza hicho kiswahili chenyewe. Mkubwa akiongea kitu anamaanisha punguza ropo kama unatafuta mume

Unaongea kama mtu asiyejitambua, ukiwa forum nyingine unaandika vitu vya maana sasa ukija huku akili sijui unaziacha wapi, Mtu ambaye amefeli mtihan si wa kuvunjwa moyo wa kulahumiwa bali ni wakupewa ushauri ili asikate tamaa na eventually afikie ndoto zake.
 
Kwanza tafakari kwa makini kwanini umepata point 30 ni si 21 au zaidi ya hapo yaani matokeo ya ujumla ya shule yenu yalikuaje ukilinganisha na matokeo yako, pia je ulipata hizo point kwa kuwa ulikuwa husomi kwa bidii, au ulipata point hizo kwa kuwa ulikuwa mtoro darasani (kiujumla angalia sababu zilizokufanya upate hizo point yaani kama wewe mwenyewe ndio ulisababisha kwa kutotumia fursa vizuri au shule uliyosoma haikuwa nzuri n.k). Baada ya hapo sasa angalia hizo sababu kama mojawapo imechangia kisha chukua hatua ya kutafuta sehemu kwa ajili ya kurudia mtihani huku moyoni ukijiwekea ahadi ya ushindi. Lakini kama ulikuwa mtoro nakushauri jaribu kujipanga kwa kufanya mtihani mwakani ila mwaka huu tumia kwa kujiandaa na kurekebisha makosa yako.

Kimsingi elimu ya O-level ni muhimu kuliko elimu zote kama mambo yalikuwa hayapandi vizuri hapa hata huko uendako ngazi za juu utaishia kutumia nguvu kubwa ili ufaulu kumbe mambo mengine uliyapuuzia huku O-level.

Waone waliokutangulia madarasa watakusaidia maana hata kama ukitafuta shule nzuri kama hujapikwa vizuri tangu form one bado utakuwa hujatatua tatizo, wewe waone walimu wazoefu watatumia uzoefu wao kwa kutengeza program za muda mfupi na utaweza kikubwa utambue sababu zilizokufanya upate hizo point na kuzifanyia kazi
 
Mtu ambaye amefeli mtihan si wa kuvunjwa moyo wa kulahumiwa bali ni wakupewa ushauri ili asikate tamaa na eventually afikie ndoto zake.

Na anapokosea unatakiwa umwambie wapi amejikwaa na wala sio kumtafutia wapi alipoangukia. mmezoea kudanganywa mnatakiwa muumie ndio mtajirekebisha usifikiri ukifeli unapigiwa makofi bali unapigwa makofi, jitahidi kutofautisha hizo tungo mbili zitakusaidia
 
We kama kweli unataka shule kuna kituo safi cha kurisiti wengi wanapata credit kama unataka kiko moshi karibu na majengo sec au nicheki 0652253800

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Jamani kwa kweli mimi nina Division four ya point 30 hivyo familia imeamuru ni rudie mtihani.
Naomba msaada ivi ufauru unaanzia ngap kwa mtu anaye risit yani D inaanza na ngapi mpaka C,
shule zipi ni bora kwa mikoa ya iringa na mbeya

background yako imekaaje dogo?inawezekana kuanzia form one ulikuwa unakuwa wa kwanza kutoka mwisho.
 
Maelezo yako yanaonyesha ulistahili kabisa kupata Daraja la nne la alama 30. Hivi kweli mwanafunzi wa kidato cha nne, hujui hata kuandika maelezo yanayovutia mtu kusoma? Hakika ulistahili, mimi nakushauri, ni bora ukafanye kazi nyingine elimu kwako ni sawa na ardhi na mbingu. You are very far from the line of success in education, please try another carrier if you can.
 
Kwenye uandishi kafanya kosa dogo tu kama wewe ulilo fanya hapa

try another carrier

Aliye fanya mtihani ni yeye na aliye feli ni yeye ila lawama asilmia kubwa naitupia serikali alafu walimu kisha wazazi na mwisho (kama nilowataja awali wote wamefanya sehemu yao) mwanafunzi.
sasa kwakuwa wewe una 4 ya 30 na "UMEAMRIWA! kurist" nakushauri ukubali kwa moyo mkunjufu kisha ukasome SANA/KWA JUHUDI uki mtegea Mungu (kama unamwamini) na hata mazingira yakiwa mabaya kwa juhudi zako + maombi kwa Mungu utafanikiwa.
wazazi/familia yako wanaweza kuonyesha kujali zaidi masuala yako ya elimu kwa atleast kukutafutia shule ya kurist
Usiku mwema.
 
wala usijali wewe mbona genius? div 4 hapo umefaulu kabisa, apply cbe
hata VETA kuna corse za usafi unachukua deploma yako then unapangiwa barabarani kusafisha au manispaa ya jiji
 
Kwanza tafakari kwa makini kwanini umepata point 30 ni si 21 au zaidi ya hapo yaani matokeo ya ujumla ya shule yenu yalikuaje ukilinganisha na matokeo yako, pia je ulipata hizo point kwa kuwa ulikuwa husomi kwa bidii, au ulipata point hizo kwa kuwa ulikuwa mtoro darasani (kiujumla angalia sababu zilizokufanya upate hizo point yaani kama wewe mwenyewe ndio ulisababisha kwa kutotumia fursa vizuri au shule uliyosoma haikuwa nzuri n.k). Baada ya hapo sasa angalia hizo sababu kama mojawapo imechangia kisha chukua hatua ya kutafuta sehemu kwa ajili ya kurudia mtihani huku moyoni ukijiwekea ahadi ya ushindi. Lakini kama ulikuwa mtoro nakushauri jaribu kujipanga kwa kufanya mtihani mwakani ila mwaka huu tumia kwa kujiandaa na kurekebisha makosa yako.

Kimsingi elimu ya O-level ni muhimu kuliko elimu zote kama mambo yalikuwa hayapandi vizuri hapa hata huko uendako ngazi za juu utaishia kutumia nguvu kubwa ili ufaulu kumbe mambo mengine uliyapuuzia huku O-level.

Waone waliokutangulia madarasa watakusaidia maana hata kama ukitafuta shule nzuri kama hujapikwa vizuri tangu form one bado utakuwa hujatatua tatizo, wewe waone walimu wazoefu watatumia uzoefu wao kwa kutengeza program za muda mfupi na utaweza kikubwa utambue sababu zilizokufanya upate hizo point na kuzifanyia kazi

kaka nimekuelewa, kiujumla matokeo ya shule yetu haya kuwa mazuri , pia sababu iliyochangia mimi kufeli ni kupuuzia masomo kidato cha tatu na kuzidisha michezo baasi. Asante
 
bora umetambua kosa lako kuliko ungalisingizia walimu hawafundishi. Kama una nia jipange kijana utafanikiwa.
 
Back
Top Bottom