Nina kijana mdogo ameathirika naishi nae, anagegeda sana vibinti vya watu, nimsaidiaje?

Nina kijana mdogo ameathirika naishi nae, anagegeda sana vibinti vya watu, nimsaidiaje?

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,880
Wakuu Wasalaam,

Leo nimekuja tupeane uzoefu na ushauri.

Nina bwana mdogo naishi naye. Ana miaka 18 kwenda 19 ni wa kiume. Huyu alikuwa mtoto wa jirani yangu kijijini nilipokulia. Ule ujirani wa kijijini ni kama ndugu tu, sababu huyu bwana mdogo toka anazaliwa mpaka anakua namuona, kila nikienda likizo basi namuona. Maana kwao na kwetu ni uzio wa minyaa tu ndio uliotutenganisha.

Huyu dogo wazazi wake wote walifariki kwa UKIMWI. Bahati mbaya na huyu dogo alizaliwa na maambukizi. Amekua hivyo huku akipatiwa dawa kuanzia umri fulani mpaka leo. Kilichonifanya nimchukue na kukaa nae, kuna wakati nilirudi likizo nikakuta dogo amedhoofu sana, sababu ilikuwa ameanza kugoma kutumia vidonge, hii ni baada ya kukua na kupata akili kuwa anatumia vidonge vile sababu ameathirika.

Ilihitaji ushawishi sana kumfanya dogo aendelee kutumia hizi dawa. Maana alikuwa mkubwa na akiwa shule akawa amepata akili kuwa vile vidonge anavyopewa kunywa ni kwa sababu ameathirika. Hakupenda kunywa akisema bora atangulie tu.

Sasa kwa sababu mimi kidogo ananiheshimu jumlisha kuniogopa, wakati wote wa likizo nikamsimamia aendelee kutumia dawa, hatimaye maamuzi ya kuja kuishi naye nilipo. Ameendelea kuwa na afya njema na tulimtafutia VETA baada ya kidato cha nne kutokufanya vizuri, na hii ni kwa sababu ni kama amekata tamaa. Kabla ya hapo darasani alikuwa anafanya vizuri sana kule sekondari.

Sasa bwana mdogo nilianza kustukia kuwa kaanza mahusiano ya kimapenzi. Na hii ni baada ya siku moja kumsikia akiongea kwenye simu asijue kama mimi na wife tupo ndani. Nikajipa zoezi la kutaka kuujua ukweli kupitia simu yake. Nikakuta kweli SMS kadhaa toka na kwenda kwa mpenzi wake.

Kifupi dogo kaanza kugegeda na alivyo HB na afya kuimarika huwezi kujua kuwa ameathirika. Sasa naona hata hapa mtaani kama vibinti vinamshobokea na havijui (background) yake. Hii inanipa wasiwasi juu ya afya yake na hao anaowagegeda.

Nilijipa siku nikakaa nae, nikampa somo kuwa hayo mambo anatakiwa kuyapa kisogo, atazame kwanza afya yake, lakini pia akumbuke bila kinga atwaangamiza vijana wenzake. Yaani ilikuwa kama nimeharibu.

Dogo akawa anaona kama namnyanyapaa! Anasema yeye pia ana haki ya kuwa na mtu maana umri wa kuwa na mpenzi eti umefika. Mimi kumwambia hivyo eti ni kama namnyanyapaa. Basi akaongea na mambo mengi yaliyonitia uchungu, sababu sikuwa na nia mbaya, bali kumsaidia yeye na hao watakaogegedwa nae.

Mimi bado nataka huyu dogo aachane na mwenendo wa kugegeda, japo nilionana na mshauri mmoja akasema sehemu nyingi huwa wanawatafutia vijana/wenza walioathirika ili wawe pamoja na kujijua kuliko kupeleka kwa wengine. Ila mimi naona umri wa huyu bado kwanza, atulie na kujenga afya.

Toka nimwambie alizira kula siku nzima, siwezi kumkaripia sana sababu ya hali yake. Sipendi aendelee sababu anaweza kuathiri afya yake na wale anaoshirikiana nao.

JF hakiharibiki kitu, kwa mazingira kama hayo, nyie wananzengo wenzangu mngefanyaje? Nifanyaje ili nimsaidie huyu dogo na huyo aliyeanzisha nae mahusiano? Tupeane mawazo.
 
Una watoto?,usalama wao upo vipi?.kwa kitu cha msingi Kama hicho ulichomwambia kwa huo umri wake alipaswa kukuelewa,kuwa mwangalifu wema wako unaweza kuujutia...
Mkuu nina watoto,wangu nilishawaelekeza na wanajua kinachoendelea juu ya huyu kijana wangu mpendwa!!Pale nyumbani sidhani,maana wa kike nilienae bado ni mdogo
 
Umeckia mkuu...

Usipende kusema *sbb... Sema sababu...
Usipende kusema *lkn... Sema lakini...

Kwann unaharibu Lugha yetu maridadi...

[HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng
Nimekuelewa Eng.
Ni kufupisha tu,kama wewe badala ya hapo chini kuandika Chief Engineer umeandika [HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng
Tujirekebishe wote mkuu
 
mwenyewe kunadada mmoja huku mtaa najuwa ana gwegwe anagwa tu kama kifulushi cha tigo hapo mzee mwache awape dozi kwa ha vitabu vya mungu vinasema mshahara wa zambi nimauti kwa acha awagawie mauti
 
Ila cha kufanya hapo ni kumtafutia mshauri tu wa kumshauri jinsi ya kuwakinga wenzake maana kisheria
Kuathirika na vvu hakukunyimi haki ya kuwa na mahusiano na pia hakukupi uhuru wa kufanya ngono zembe ila ni umakini tu unatakiwa ili
Hao wengine nao wawe salama mtafutie mshauri na saa na hata hospitali akutane na wataalamu wa afya wamfundishe
 
Back
Top Bottom