Nina kijana mdogo ameathirika naishi nae, anagegeda sana vibinti vya watu, nimsaidiaje?

Nina kijana mdogo ameathirika naishi nae, anagegeda sana vibinti vya watu, nimsaidiaje?

huo siyo ushauri mkuu kwani kule kijijini hamana mabinti?cha msingi dogo apelekwe apewe ushauri nasaha msiangalie tuu kua anaambukiza maana uwezo huo hana kwa kua anatumia dawa sema kumshauri kua anapofanya ngono zembe pia anachukua maambukizi mapya kwa hiyo wale virus watakua wengi na watajenga usugu wa dawa muwe mnasoma kabla ya kutoa ushauri unapoathirika ukawa unatumia arvs huwezi muambukiza mtu maana wale wadudu wamelewa wamelala ila sasa ukifanya na ambaye hatumii dawa na ni muathirika apo unachukua maambukizi mapya na pia unapofanya sana kinga inashuka maana kwa umri wa huyo dogo utakuta anapiga bao zaidi ya tatu ...cha msingi apewe elimu ale vizuri aache mawazo ,afanye zoezi,apate mwathirika mwenzie anaetumia dawa afanye ngono kama kawaida bila madhara ataishi miaka mingi sana ....ukimwi siyo ugojwa...........


Kwa hiyo nikigegedana na mtu aliyeathirika na anatumia ARV na mimi ni mzima cjaambukizwa sipati virusi..??? Ukiachana na kinga(ndomu). Ni swali kutoka kwenye maelezo yako hapo juu..!!
 
Yaani huyo anakusumbua kwa kuwa unamdekeza! hebu kaza msuli mpe ukweli wake anavyopaswa kuishi! kama anazira kula azire!!! una mbeba mtu ambaye habebeki. Kuwa mkali atanyooka, anakuringia na kukuonesha vituko kwa kuwa yaelekea wewe ni mpole.
Kwa kuwa umemwambia kistaarabu hasikii sasa unapaswa uwe mkali, akira kula hakuna kumbembeleza, kila mtu atakufa siku zake zikitimia.

Waafrika wengi hasa watanzania, tunafikiri ukali ndo suluhisho... Ukali haumzuii kugegeda bado na kuwasambazia wengine.. Kazi kubwa anayotakiwa kufanya ni kutreat psychology ya huyo dogo...!! Mara ngapi wazazi wenu walikuwaga wakali lkn bado mlikua watukutu..??
 
zamani watu wazima walikuwa nakimbilia vibinti vidogo wakiza viko salama..kwa sasa ndio hatari zaidi..vijana wengi waliozaliwa miaka ya elfu2 wamezaliwa nao..kuna binti hapa mtaani pia alizaliwa nao cha kushangaza ana mpenzi tena kijana mwenzake...nihatari sana sana..niwakati wa serikali kutoa elimu mashuleni ili kunusuru vijana hawa
 
Wakuu Wasalaam,

Leo nimekuja tupeane uzoefu na ushauri.

Nina bwana mdogo naishi naye. Ana miaka 18 kwenda 19 ni wa kiume. Huyu alikuwa mtoto wa jirani yangu kijijini nilipokulia. Ule ujirani wa kijijini ni kama ndugu tu, sababu huyu bwana mdogo toka anazaliwa mpaka anakua namuona, kila nikienda likizo basi namuona. Maana kwao na kwetu ni uzio wa minyaa tu ndio uliotutenganisha.

Huyu dogo wazazi wake wote walifariki kwa UKIMWI. Bahati mbaya na huyu dogo alizaliwa na maambukizi. Amekua hivyo huku akipatiwa dawa kuanzia umri fulani mpaka leo. Kilichonifanya nimchukue na kukaa nae, kuna wakati nilirudi likizo nikakuta dogo amedhoofu sana, sababu ilikuwa ameanza kugoma kutumia vidonge, hii ni baada ya kukua na kupata akili kuwa anatumia vidonge vile sababu ameathirika.

Ilihitaji ushawishi sana kumfanya dogo aendelee kutumia hizi dawa. Maana alikuwa mkubwa na akiwa shule akawa amepata akili kuwa vile vidonge anavyopewa kunywa ni kwa sababu ameathirika. Hakupenda kunywa akisema bora atangulie tu.

Sasa kwa sababu mimi kidogo ananiheshimu jumlisha kuniogopa, wakati wote wa likizo nikamsimamia aendelee kutumia dawa, hatimaye maamuzi ya kuja kuishi naye nilipo. Ameendelea kuwa na afya njema na tulimtafutia VETA baada ya kidato cha nne kutokufanya vizuri, na hii ni kwa sababu ni kama amekata tamaa. Kabla ya hapo darasani alikuwa anafanya vizuri sana kule sekondari.

Sasa bwana mdogo nilianza kustukia kuwa kaanza mahusiano ya kimapenzi. Na hii ni baada ya siku moja kumsikia akiongea kwenye simu asijue kama mimi na wife tupo ndani. Nikajipa zoezi la kutaka kuujua ukweli kupitia simu yake. Nikakuta kweli SMS kadhaa toka na kwenda kwa mpenzi wake.

Kifupi dogo kaanza kugegeda na alivyo HB na afya kuimarika huwezi kujua kuwa ameathirika. Sasa naona hata hapa mtaani kama vibinti vinamshobokea na havijui (background) yake. Hii inanipa wasiwasi juu ya afya yake na hao anaowagegeda.

Nilijipa siku nikakaa nae, nikampa somo kuwa hayo mambo anatakiwa kuyapa kisogo, atazame kwanza afya yake, lakini pia akumbuke bila kinga atwaangamiza vijana wenzake. Yaani ilikuwa kama nimeharibu.

Dogo akawa anaona kama namnyanyapaa! Anasema yeye pia ana haki ya kuwa na mtu maana umri wa kuwa na mpenzi eti umefika. Mimi kumwambia hivyo eti ni kama namnyanyapaa. Basi akaongea na mambo mengi yaliyonitia uchungu, sababu sikuwa na nia mbaya, bali kumsaidia yeye na hao watakaogegedwa nae.

Mimi bado nataka huyu dogo aachane na mwenendo wa kugegeda, japo nilionana na mshauri mmoja akasema sehemu nyingi huwa wanawatafutia vijana/wenza walioathirika ili wawe pamoja na kujijua kuliko kupeleka kwa wengine. Ila mimi naona umri wa huyu bado kwanza, atulie na kujenga afya.

Toka nimwambie alizira kula siku nzima, siwezi kumkaripia sana sababu ya hali yake. Sipendi aendelee sababu anaweza kuathiri afya yake na wale anaoshirikiana nao.

JF hakiharibiki kitu, kwa mazingira kama hayo, nyie wananzengo wenzangu mngefanyaje? Nifanyaje ili nimsaidie huyu dogo na huyo aliyeanzisha nae mahusiano? Tupeane mawazo.
Huyo kijana kwa sasa yuko wapi?
 
Ko unataka agegedwee yeye? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huyo nimuuwaji....piga sindano ya sumu kuokoa kundi kubwa la vijana,mfanye mbuzi wakafara ili kundi kubwa la.mbuzi liweze kuokokaa.hana maana
 
Back
Top Bottom