Nina kijana mdogo ameathirika naishi nae, anagegeda sana vibinti vya watu, nimsaidiaje?

Nina kijana mdogo ameathirika naishi nae, anagegeda sana vibinti vya watu, nimsaidiaje?

Ha ha ha hio simple sana, Huyo dogo mrudishe Bush kisha muwezeshe maisha kama kumfungulia mradi kama duka ama kilimo na ufugaji au mpe boda boda kisha mueleze ukweli kuwa kadri anavyojiingiza kwenye mapenzi ndivyo anavyo fupisha maisha yake. Kwakuwa ni mtu mzima ushauri haulazimishwi na ukiendelea kumfuga hapo kwako yatakayokukuta usimlaumu yeyote. Muwezeshe akaishi maisha yake mbali na hapo
Kwahiyo huko vijijini hakuna wasichana bali kuna wanaume watupu au wasichana wa vijijini siyo muhimu sana kuliko wa mjini,unahalalisha wasichana vijijini waangamie mjomba ,bado sijaona suluhisho
 
Waache waangamie tu hao kina Dada ,werevu ndio watakaosalimika
 
ati wenye ngoma wana genye mara saba saidi ya walioathirika.....!!!!
mkuu dogo anahitaji psychological twisting
 
Wakuu Wasalaam,

Leo nimekuja tupeane uzoefu na ushauri.

Nina bwana mdogo naishi naye. Ana miaka 18 kwenda 19 ni wa kiume. Huyu alikuwa mtoto wa jirani yangu kijijini nilipokulia. Ule ujirani wa kijijini ni kama ndugu tu, sababu huyu bwana mdogo toka anazaliwa mpaka anakua namuona, kila nikienda likizo basi namuona. Maana kwao na kwetu ni uzio wa minyaa tu ndio uliotutenganisha.

Huyu dogo wazazi wake wote walifariki kwa UKIMWI. Bahati mbaya na huyu dogo alizaliwa na maambukizi. Amekua hivyo huku akipatiwa dawa kuanzia umri fulani mpaka leo. Kilichonifanya nimchukue na kukaa nae, kuna wakati nilirudi likizo nikakuta dogo amedhoofu sana, sababu ilikuwa ameanza kugoma kutumia vidonge, hii ni baada ya kukua na kupata akili kuwa anatumia vidonge vile sababu ameathirika.

Ilihitaji ushawishi sana kumfanya dogo aendelee kutumia hizi dawa. Maana alikuwa mkubwa na akiwa shule akawa amepata akili kuwa vile vidonge anavyopewa kunywa ni kwa sababu ameathirika. Hakupenda kunywa akisema bora atangulie tu.

Sasa kwa sababu mimi kidogo ananiheshimu jumlisha kuniogopa, wakati wote wa likizo nikamsimamia aendelee kutumia dawa, hatimaye maamuzi ya kuja kuishi naye nilipo. Ameendelea kuwa na afya njema na tulimtafutia VETA baada ya kidato cha nne kutokufanya vizuri, na hii ni kwa sababu ni kama amekata tamaa. Kabla ya hapo darasani alikuwa anafanya vizuri sana kule sekondari.

Sasa bwana mdogo nilianza kustukia kuwa kaanza mahusiano ya kimapenzi. Na hii ni baada ya siku moja kumsikia akiongea kwenye simu asijue kama mimi na wife tupo ndani. Nikajipa zoezi la kutaka kuujua ukweli kupitia simu yake. Nikakuta kweli SMS kadhaa toka na kwenda kwa mpenzi wake.

Kifupi dogo kaanza kugegeda na alivyo HB na afya kuimarika huwezi kujua kuwa ameathirika. Sasa naona hata hapa mtaani kama vibinti vinamshobokea na havijui (background) yake. Hii inanipa wasiwasi juu ya afya yake na hao anaowagegeda.

Nilijipa siku nikakaa nae, nikampa somo kuwa hayo mambo anatakiwa kuyapa kisogo, atazame kwanza afya yake, lakini pia akumbuke bila kinga atwaangamiza vijana wenzake. Yaani ilikuwa kama nimeharibu.

Dogo akawa anaona kama namnyanyapaa! Anasema yeye pia ana haki ya kuwa na mtu maana umri wa kuwa na mpenzi eti umefika. Mimi kumwambia hivyo eti ni kama namnyanyapaa. Basi akaongea na mambo mengi yaliyonitia uchungu, sababu sikuwa na nia mbaya, bali kumsaidia yeye na hao watakaogegedwa nae.

Mimi bado nataka huyu dogo aachane na mwenendo wa kugegeda, japo nilionana na mshauri mmoja akasema sehemu nyingi huwa wanawatafutia vijana/wenza walioathirika ili wawe pamoja na kujijua kuliko kupeleka kwa wengine. Ila mimi naona umri wa huyu bado kwanza, atulie na kujenga afya.

Toka nimwambie alizira kula siku nzima, siwezi kumkaripia sana sababu ya hali yake. Sipendi aendelee sababu anaweza kuathiri afya yake na wale anaoshirikiana nao.

JF hakiharibiki kitu, kwa mazingira kama hayo, nyie wananzengo wenzangu mngefanyaje? Nifanyaje ili nimsaidie huyu dogo na huyo aliyeanzisha nae mahusiano? Tupeane mawazo.
Ni kumpa ushauri tuuu unamtosha na jinsi ya kujikinga mapenzi yakija ni vigumu kuzuiaaa
 
Kwahiyo huko vijijini hakuna wasichana bali kuna wanaume watupu au wasichana wa vijijini siyo muhimu sana kuliko wa mjini,unahalalisha wasichana vijijini waangamie mjomba ,bado sijaona suluhisho
Si kazaliwa hapo hivyo wanamjua watajilinda nae
 
bro pole sana....hili suala usilichukulie simple kabisa,, huyo kijana anatumia huo ugonjwa kama defensive yake na hasa unapokuwa unamshauri.. unaongea nae ktk mazingira gani? elewa hata wewe na familia yako mko hatarini, kama ameamua kuambukiza ili asife peke yake, je wewe na familia yako yeye anaichukuliaje? usije kujuta kwa wema wako, najua ktk hali kaa hiyo lazima atasema unamnyanyapaa but huna jinsi. Kumbuka wewe pia ni mhusika ktk kueneza maambukizi,, ulimleta kutoka kijijini, ili uje kumuendeleza, na unajua fika ni HIV +,,,kuwasaidia ni wajibu wetu...but umakini zaidi watakiwa.....kwa kifupi unashiriki kueneza maambukizi.
 
Nafahamu hawezi kufika huku,lakini naelezea kwa undani kwa sababu sio wote wanaojua kisa hiki. Zamani tulitumia Ukurasa wa "MAONI/MASWALI" wa gazeti la Uhuru,sasa mitandao imeturahisishia
Hujafanya jambo baya. Ni vizuri kuwa muwazi ili upate ushauri kama unavyoomba. Msamehe bure nadhani kaguswa na amezoea kuficha ficha mambo. Ushauri wangu ni kuwa huyo kijana hajielewi na kama ulimwambia ukweli akaja juu na kuzira chakula basi amekuzidi kimo. Kukaa naye humsaidii bali unamharibu tu.

Aidha Nakuona unajisahau hususan pale unaposema mtoto wako wa kike ni mdogo!!!! Na wengine ni wavulana!!!!!! Siku hizi watoto wa kuchungwa ni wavulana hasa majumbani maana vijana kama huyo wa kwako anaweza kuwanajisi.

Onyo acha kuishi na mtu nyumbani kwako umlishe na umpe kitanda bila kukutiiiiiii kama hataki kukutii akapange au ajenge yake.
 
Nimezingatia ulichokisema,umeongea kwa hekima
 
bro pole sana....hili suala usilichukulie simple kabisa,, huyo kijana anatumia huo ugonjwa kama defensive yake na hasa unapokuwa unamshauri.. unaongea nae ktk mazingira gani? elewa hata wewe na familia yako mko hatarini, kama ameamua kuambukiza ili asife peke yake, je wewe na familia yako yeye anaichukuliaje? usije kujuta kwa wema wako, najua ktk hali kaa hiyo lazima atasema unamnyanyapaa but huna jinsi. Kumbuka wewe pia ni mhusika ktk kueneza maambukizi,, ulimleta kutoka kijijini, ili uje kumuendeleza, na unajua fika ni HIV +,,,kuwasaidia ni wajibu wetu...but umakini zaidi watakiwa.....kwa kifupi unashiriki kueneza maambukizi.
Mkuu naona hekima ndani yako,nitazingatia ulichowasilisha
 
Duh kumbe ni wewe barafu, wkt nacomment siku hizo nilicomment kiutani. Hakika wewe ni mjuvi wa vitu vingi na hii post huenda ni kweli. Tupe update za huyo dogo
 
Duh kumbe ni wewe barafu, wkt nacomment siku hizo nilicomment kiutani. Hakika wewe ni mjuvi wa vitu vingi na hii post huenda ni kweli. Tupe update za huyo dogo
Sasa leo ndio ukomenti serious sasa.
Ha ha ha ha eti wakati huoo...Kwani huo wakati una tofauti na sasa?
 
Back
Top Bottom