Wakuu Wasalaam
Leo nimekuja tupeane uzoefu na ushauri.Nina bwana mdogo naishi naye.Ana miaka 18 kwenda 19 ni wa kiume.Huyu alikuwa mtoto wa jirani yangu kijijini nilipokulia.Ule ujirani wa kijijini ni kama ndugu tu,sbb huyu bwana mdogo toka anazaliwa mpaka anakua namuona,kila nikienda likizo basi namuona.Maana kwao na kwetu ni uzio wa minyaa tu ndio uliotutenganisha.
Huyu dogo wazazi wake wote walifariki kwa UKIMWI.Bahati mbaya na huyu dogo alizaliwa na maambukizi.Amekuwa hivyo huku akipatiwa dawa kuanzia umri fulani mpaka leo.Kilichonifanya nimchukue na kukaa nae,kuna wakati nirirudi likizo nikakuta dogo amedhoofu sana,sbb ilikuwa ameanza kugoma kutumia vidonge,hii ni baada ya kukua na kupata akili kuwa anatumia vidonge vile sbb ameathirika.
Ilihitaji ushawishi sana kumfanya dogo aendelee kutumia hizi dawa.Maana alikuwa mkubwa na akiwa shule akawa amepata akili kuwa vile vidonge anavyopewa kunywa ni kwa sbb ameathirika.Hakupenda kunywa akisema bora atangulie tu.
Sasa kwa sbb mimi kidogo ananiheshimu jumlisha kuniogopa,wakati wote wa likizo nikamsimamia aendelee kutumia dawa,hatimaye maamuzi ya kuja kuishi naye nilipo.Ameendelea kuwa na afya njema na tulimtafutia VETA baada ya kidato cha nne kutokufanya vizuri,na hii ni kwa sbb ni kama amekata tamaa.Kabla ya hapo darasani alikuwa anafanya vizuri sana kule sekondari.
Sasa bwana mdogo nilianza kustukia kuwa kaanza mahusiano ya kimapenzi.Na hii ni baada ya siku moja kumsikia akiongea kwenye simu asijue kama mimi na wife tupo ndani.Nikajipa zoezi la kutaka kuujua ukweli kupitia simu yake.Nikakuta kweli msg kadhaa toka na kwenda kwa mpenzi wake.
Kifupi dogo kaanza kugegeda,na alivyo HB na afya kuimalika huwezi kujua kuwa ameathirika.Sasa naona hata hapa mtaani kama vibinti vinamshobokea na havijui background yake.Hii inanipa wasiwasi juu ya afya yake na hao anaowagegeda.
Nilijipa siku nikakaa nae,nikampa somo kuwa hayo mambo anatakiwa kuyapa kisogo,atazame kwanza afya yake,lkn pia akumbuke bila kinga atwaangamiza vijana wenzake.Yaani ilikuwa kama nimeharibu.
Dogo akawa anaona kama namnyanyapaa!Anasema yeye pia ana haki ya kuwa na mtu maana umri wa kuwa na mpenzi eti umefika.Mimi kumwambia hivyo eti ni kama namnyanyapaa.Basi akaongea na mambo mengi yaliyonitia uchungu,sbb sikuwa na nia mbaya,bali kumsaidia yeye na hao watakaogegedwa nae.
Mimi bado nataka huyu dogo aachane na mwenendo wa kugegeda,japo nilionana na mshauri mmoja akasema sehemu nyingi huwa wanawatafutia vijana/wenza walioathirika ili wawe pamoja na kujijua kuliko kupeleka kwa wengine.Ila mimi naona umri wa huyu bado kwanza,atulie na kujenga afya.
Toka nimwambie alizila kula siku nzima,siwezi kumkaripia sana sbb ya hali yake.Sipendi aendelee sbb anaweza kuathiri afya yake na wale anaoshirikiana nao.
JF hakiharibiki kitu,kwa mazingira kama hayo,nyie wananzengo wenzangu mngefanyaje?Nifanyaje ili nimsaidie huyu dogo na huyo aliyeanzisha nae mahusiano?Tupeane mawazo.