Nina kilo 86 lakini kila ninayekutana naye anasema nimekonda sana! Nifanyeje ili ninenepe kwa haraka?

Nina kilo 86 lakini kila ninayekutana naye anasema nimekonda sana! Nifanyeje ili ninenepe kwa haraka?

Na yeye pia alisema nimekonda Cha ajabu nguo zangu zinanitosha vizuri tuu lakini tangu watu waniambie nimekonda nikitmbea naona napepeseuka
Basi haujiamini😁,,,mie inakuwaga hivo minyama ikianza kujaa wakianza kaniambia nanenepa aisee nakuwa najichukia,,sipendi ubonge,,,,

Nilishakuwaga bonge yaani bonge,nilikuwa nikitembea kidogo nahema kama nimebeba mzigo.
 
Mimi ni ke

Daa kwa huo urefu na hizo kilo inatakiwa uwe bonge nyanya. Nakuzidi urefu mbali sana na nina kilo 83 lakini kila mtu ananambia nimenenepa sana . Maana nimeongezeka kilo 7 ndani ya mwaka mmoja.
Kumbe wewe ni Ke basi ngoja wengine waje watoe muongozo maana maumbo yenu mnayajua wenyewe
 
Nina urefu wa 165cm lakini Cha ajabu mwakaa juzi nilikua Nina kilo 83 Sasa shida ni nini mpaka na Mimi nimeanza kujiona nimekon
Una uhakika ulitumia mizani nzima? Inaweza kuwa mbovu. Nasema hivi kwa sababu kilo 80+ ni nyingi na haiwezi kuwa ni kukonda. Jambo jingine... unaishi kwa kufuata matakwa ya watu au unaishi maisha yako? Na pia, vijijini kuna ule ushamba wa kutaka kuona ''mijitu minene'' kama ndiyo afya na mafanikio katika maisha hivyo kama ulikuwa na kitambi na kimeisha wanaona kama umepata shida.
 
Jamani nahitaji msaada wenu hivi karibuni nimepima kilo zangu nikawa Nina kilo 86 nikasafiri kwenda mkoani kwaajili ya sikukuu kila ninae kutana nae ananiambia kua nimekonda jamani nifanyaje je ni ugonjwa au ni shida gani maana Mimi najiona Niko kawaida ila watu wanasema nimekonda sana naogopa hata kukutana na watu wangu wa zamani nifanyaje ninenepe Kwa haraka
Mkuu lee jack pole kwa kadhia hiyo ya pressure ya jamii kuhusu muonekano wa afya yako; hata hvy pressure ya jamii isikufanye ukawa namna ambayo itakupa majuto baadae, afya hupimwa kwa vipimo si kwa macho ya mwanadamu kama ilivyo kwako.

Hapa nakupa Key Factors (Afya vs Mtazamo wa watu kuhusu afya;

1. Kununepa huonekana kama afya njema, kukonda huchukuliwa kama ugonjwa — mtazamo wa zamani usioendana na hali ya sasa.

2. Uhalisia wa afya ya sasa: Magonjwa yasiyoambukiza (presha, kisukari, moyo) yanaonekana zaidi kwa watu wanene; mwili wa wastani mara nyingi ni afya bora.

3. Uzito pekee si kipimo cha ugonjwa: Kilo 86 hazimaanishi ugonjwa bila kuangalia urefu, mtindo wa maisha na vipimo vya afya.

4. Sababu za kuonekana umekonda: Mabadiliko ya maisha, chakula bora, shughuli nyingi, au kupungua mafuta mwilini.

5. Dalili za kuhofiwa: Kupungua uzito ghafla, kukosa hamu ya kula, uchovu mkubwa, homa/jasho la usiku — bila hizi, uwezekano wa ugonjwa ni mdogo.

6. Kunenepa haraka si suluhisho: Kunenepa kwa kulazimisha huongeza hatari ya magonjwa; lengo ni unene wa afya, si mafuta mengi.

7. Ushauri wa kiafya: Fuata mlo kamili, ongeza protini, pumzika vizuri, pima presha na sukari kwa uhakika.

8. Kwa uhakika ni vema ukapima magonjwa kama sukari, shinikizo la damu, IBM yako ili kujua usahihi wa uwiaano wa urefu na uzito unaokutia hofu.

Hitimisho: Afya hupimwa kwa vipimo na mwenendo wa mwili, si maoni ya watu. Mwili wa wastani ni kinga ya magonjwa ya baadaye.
 
Bila picha ni porojo tu😂😂
Cc: secretarybird
Kwanza bibie lee jack tambua kuwa hao wanaokuambia umekonda wanakuonea wivu kwa kudhani kuwa kwa kupungua huko sasa utakuwa mnyumbulifu katika sita kwa sita ukijamiiana vikali na mwenza wako.

Watu huwa hawafurahi wakiona unaumbo linalokuwezesha kungonoka kwa styles anuwai (tofauti tofauti).

Vincenzo Jr.
 
Back
Top Bottom