Nina kituo kinacholea na kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu, nilikuwa naomba kujua njia za kupata wafadhili ili kusapoti kituo changu

Nina kituo kinacholea na kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu, nilikuwa naomba kujua njia za kupata wafadhili ili kusapoti kituo changu

Joined
Dec 11, 2024
Posts
94
Reaction score
240
Wakuu noamba Muongozo wa kupata wafadhili katika kituo changu Ambacho kinahudumia watoto wenye mahitaji maalumu.

Kituo hiki kipo Mikocheni, ndo kimeanzishwa hivi karibuni.

Je, naomba kuuliza nitapataje wafadhili wakukisapoti kituo changu ili kikue na kuwafikiwa watoto wengi zaidi

Wapo walemavu wa viungo
Wapo wenye Usonji
Wapo vipofu
Wapo viziwi

Wapo wenye mtindio wa ubongo.

Kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu ningependa kupata sapoti na back up kutoka Kwa wafdhili mbali mbali ili kuhakisha tunahudumia watoto wengi zaidi.

Kituo hiki kina Nyumba za kulala watoto zipo .

Miundombinu ipo vizuri

Kipo mikocheni

Karibu Kwa mawazo na ushauri .

Kuhusu idadi ya watoto inafika 50 Ila kituo kinategemea kuweza kua-Accommodate watoto 150

Facilities zote na recreation pamoja na madarasa zipo .
 
Uliazishaa kwa madhumuni gan??... Kama kusaidia Mungu akubaliki ilaa kama kupigaa helaa za misaaada the rest is history... maaana nmeona sehem nying watu wanaazisha center hizo kwa ajili ya MAOKOTO tuu...... Anyway make affiliation with churches..
 
Asante Kwa ushauri mkuu .
 
1 . Hapo unahitaji grants and fund mobilization experts kwa ajili ya kukufundisha jinsi ya kupata pesa za wahisani ikiwemo kuandika propasals

2. promo promo promo. Kuwa na social media page na website maana wafadhili lazma waone uthibitisho wa umefikia wapi. Usione watu wapo busy kupiga picha na videos za watu walio katika mazingira hatarishi ukadhani wanapenda. Mkakati tu mkuu

3. I assume pesa unayo kwa setting ya hicho kituo. Tengeneza connections zaidi na jamaa wa NGOs maana wana group zao kama secret societies.. Taarifa yoyote hata kama ni grants announcement wanapeana wao kwa wao kirahisi. So ingia kwenye mfumo mkuu.
 
Barikiwa Sana.
 
Mimi naelewa vizuri hayo mambo wengi mnaazisha vituo ili mpate faida kupitia hao watoto na sio watoto kupata faida kupitia wewe iyo ipo wazi

Hapo tukisema tuje kukagua kituo kina makosa chungu nzima
Hiki kitu kiliniumiza sana maana unaingia kwenye NGO kwa ajili ya kuvolunteer. Ila wenzio wapo busy kujua tunafanya nini kupata funds.

Yani kwao ni kama chanzo cha pesa au career halafu wahitaji wanakuja mwishoni
 
Back
Top Bottom