Nina kituo kinacholea na kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu, nilikuwa naomba kujua njia za kupata wafadhili ili kusapoti kituo changu

Nina kituo kinacholea na kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu, nilikuwa naomba kujua njia za kupata wafadhili ili kusapoti kituo changu

1 . Hapo unahitaji grants and fund mobilization experts kwa ajili ya kukufundisha jinsi ya kupata pesa za wahisani ikiwemo kuandika propasals

2. promo promo promo. Kuwa na social media page na website maana wafadhili lazma waone uthibitisho wa umefikia wapi. Usione watu wapo busy kupiga picha na videos za watu walio katika mazingira hatarishi ukadhani wanapenda. Mkakati tu mkuu

3. I assume pesa unayo kwa setting ya hicho kituo. Tengeneza connections zaidi na jamaa wa NGOs maana wana group zao kama secret societies.. Taarifa yoyote hata kama ni grants announcement wanapeana wao kwa wao kirahisi. So ingia kwenye mfumo mkuu.
Fuata huu ushauri mkuu, tafuta expert wa grants and funds ambae ni mzuri kuorganiae, atakufundisha na kukusaisia yote hayo hata kupitia balozi mbalimbali, lakini kikubwa social adverts pia is very important katika kufikia watu wengi nchi tofauti.

Tafuta mtu huyo haraka.
 
Fuata huu ushauri mkuu, tafuta expert wa grants and funds ambae ni mzuri kuorganiae, atakufundisha na kukusaisia yote hayo hata kupitia balozi mbalimbali, lakini kikubwa social adverts pia is very important katika kufikia watu wengi nchi tofauti.

Tafuta mtu huyo haraka.
🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Asante mkuu kwa kuwatag, kumbukumbu iliniishia kidogo.

Sidhani kama ni watu wa shari, watalipokea hili jambo kwa moyo mweupe kabisa.
Ni watoaji hawawezi kuzingua, km wakizingua basi hawakumaanisha katika kujitolea..!! 😹😹
Usiogope dogo tulia hebu 🤣
 
Kituo kipo vizuri Ila nimefikiria kuwafikia watoto wengi zaidi hasa. Wenye mahitaji maalumu.


Dah! Pamoja na nia yako njema ya kutaka kusaidia watoto wenye uhitaji maalumu, lakini pana walakini kidogo. Unasema kimeanzishwa majuzi tu, na leo umeshafloat, je ulikianzisha kwa mhemuko? Toka kukianzisha mpaka sasa ni akina nani walokupa support? Wakati unakianzisha uliwaza picha ya kituo chako miaka 5, 10, 20 kuanzia sasa?
 
Mimi naelewa vizuri hayo mambo wengi mnaazisha vituo ili mpate faida kupitia hao watoto na sio watoto kupata faida kupitia wewe iyo ipo wazi

Hapo tukisema tuje kukagua kituo kina makosa chungu nzima
mkuu, i think ni vema tuache hizi nergativity. Ni kweli wengine wanaanzisha kwa maslahi yao, lakini wengine ni kitu wanatamani kufanya ili kweli kusaidia hao watu wenye mahitaji maalum kwa sababu either washawahi kuona wanavopata shida na kunyanyapaliwa na kuishia kua kamacwametelekezwa.

Tuwatie moyo wanaoanzisha vituo hivi, lakini tu tuwasisirize wafuate sheria, Wizara ya mama gwajima, dada angu @gwajimad ikutambue ili apate miongozo sahihi.

tuwatie moyo lakini wawe wanachunguzwa na kufatilowa na wizara ya maendeleo ya jamii.
 
Kupata wafadhili kwa sasa unaweza kupitia wakati mgumu kidogo kwakua huko Amerika Trump amesha tibua mfumo.
Wafadhili na wadau hawana ile hamasa kama hapo kabla, ikizingatiwa pia asilimia kubwa na lengo na madhumuni ya kuanzishwa vitio vya hivi ni kwa masilahi ya kibinafsi kwa waanzilishi.

Wao wafadhili kwa sasa wanafahamu fika na ndio maana kuna kuwa na kauzito kidogo.

Unacho paswa kufanya pamaja na lengo au kusudio lako la kuanzisha kituo hiki ulipaswa kuwa na mtaji mkubwa kidogo uweze kunda kwa muda mrefu na kuwa na wahitaji wachache unao weza kuwamudu.


Hizi issue zina uzika ila si kama juzi na jana.
Kwa hio tembelea wewe na wahitaji wako kwa wafadhili wa ndani, wape sababu za kutosha kwanini kuwepo na kituo hiko, dhumuni na lengo na makusidio.

Tengeneza mradi ambao utakuwa mali ya kitio ambao utautegemeza kituo na si kituo kitegemee wafadhili.

Tembelea makanisi, ongea na viongozi wao, tasisi kubwa kubwa , ongea na viongozi wao, serika na misikiti na wote wanao jihusisha na imani.
Tembelea vituo vingine na kupata connection wao wanafanyaje .


Yote ya yote mleta mada usiweke tarajio la kupata faida ya wewe kupitia hiko kituo , we fanya kama sadaka , muachie Mungu akipiganie hakika hata wahitaji 500 wakiwa hapo hakuna hata mmoja atalala njaa.


Shukurani kwa huduma yako hio jaliwa uwezesho nasi tukijaliwa tupe anwani rahisi ya kufika hata tukija na sukari kilo moja itakidhi haja japo kiasi.
 
Kuna njia nyingi za kupata ufadhili ila njia nzuri na rahisi ni Kuandaa Project proposal kumshawishi mfadhili akupe kupitia walengwa wako..

Hizi grants huwa zipo za aina mbili solicited na unsolicited, solicited ni hizi ambazo huwa zina tangazwa.. hizi huenda Kwa trend/misimu kuanzia January-march mara nyingi huwa wanatoa kwa upande kilimo/ardhi / misitu/ Nyuki mfano mfuko wa Misitu Tanzania limeanza kutoa ruzuku kwa vikundi, NGOs, CBOs tokea December march.. Pia Climate action window 2025

Stay up to date soon wataanza kutoa kwa upande wa jamii na hapo ndo unatakiwa uwe fisi kufanya Lobbying and advocacy (ukisikia mtu anatumia pesa kupata pesa ndo hapo).

Ni jambo jema sana kusaidia asiye na uwezo pia ni amri ya Mungu.. All the Best 🙏
 
Wakuu noamba Muongozo wa kupata wafadhili katika kituo changu Ambacho kinahudumia watoto wenye mahitaji maalumu.

Kituo hiki kipo Mikocheni, ndo kimeanzishwa hivi karibuni.

Je, naomba kuuliza nitapataje wafadhili wakukisapoti kituo changu ili kikue na kuwafikiwa watoto wengi zaidi

Wapo walemavu wa viungo
Wapo wenye Usonji
Wapo vipofu
Wapo viziwi

Wapo wenye mtindio wa ubongo.

Kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu ningependa kupata sapoti na back up kutoka Kwa wafdhili mbali mbali ili kuhakisha tunahudumia watoto wengi zaidi.

Kituo hiki kina Nyumba za kulala watoto zipo .

Miundombinu ipo vizuri

Kipo mikocheni

Karibu Kwa mawazo na ushauri .

Kuhusu idadi ya watoto inafika 50 Ila kituo kinategemea kuweza kua-Accommodate watoto 150

Facilities zote na recreation pamoja na madarasa zipo .
Wewe si ndo mfadhili mwenyewe, unatafuta mfadhili mwingine nani?! Au unataka kupiga pesa kupitia migongo ya walemavu? Hebu kuwa siliazi bwana!
 
Back
Top Bottom