Njoo nayo kitambaa cheupe bar, nitakuelekeza namna ya kutumia,Kuna pisi zitakupa ushauri[emoji23]au ngoja nimalize hapahapa
Laki sita ni nyingi mbona,
Kama unaweza kutembea achana na masomo
1.Chukua toroli, jaza matunda kama ndizi, nanasi, maembe, matango, n k, kabla hujafanya hivyo tafuta mtu ambaye anafanya kazi hiyo, akupe utaratibu, utanunua shilling ngapi unauza shiling ngapi.
2.Nenda karume au ulizia machimbo ya viatu kariakoo, chukua pairs kadhaa ingia nazo mtaani, kumbuka kuwa makini.
3.Nunua begi kubwa, jaza makava ya simu na protectors ,chaja za simu ingia nazo mtaani, huku nyingine ukishikilia mkononi.
4.Ingia machimbo, ya spana na baadhi ya vifaa vidogo vidogo, kama stickers, Stering covers, mchawi foleni au kwenye yards za magari makubwa.
5.Urembo,Boxers za kiume, saa za mkononi , cheni,bangili , n. K Cha muhimu kufanya utafiti kidogo kabla hujanunua.
Zipo biashara nyingi sana kwa mtaji wako kama kianzio, ila kikubwa biashara haikosi changamoto.
Zingatia kuwa na lugha nzuri kwa wateja, maana mwingine anajua kiatu hiki akienda chimbo ni 10,000 tu iweje umuuzie 15000?
Zingatia usafi wa mwili na mavazi, kuwa smart na unukie .
Omba MUNGU kwa kila hatua.
Kila la kheri.