Nina leseni ya driving gari ndogo (sio class C) na nime-renew tangu 1990, leo hii nakataliwa ku-renew eti sina cheti!

Niliwahi kusema humu JF, katika taasisi za serikali ninazozichukia kuliko zote, ni Polisi na TRA - kwa sababu hawa ndio wana mambo ya kijinga kupita kiasi.
Kama unawachukia TRA na Polisi unakosea hawana kosa lolote wao ni watendaji tu na watekelezaji wa kile wanachoagizwa na serekali,chuki yako ungeielekeza kwenye serekali hapo ungekuwa umelenga penyewe.
 
Kama unawachukia TRA na Polisi unakosea hawana kosa lolote wao ni watendaji tu na watekelezaji wa kile wanachoagizwa na serekali,chuki yako ungeielekeza kwenye serekali hapo ungekuwa umelenga penyewe.
Ukipewa amri isiyo halali usiisimamie kama mbwa anavyoitikia amri ya bwana wake
 
Acha kutetea ujinga ina maana huyo hajuwahi kusoma chuo udereva alijifunzia nyumbani hamna dereva hapo
Udereva unasomewa apeleke cheti
Na ukaruhusiwa kuendesha gari na ku-renew license kwa miaka 34 na leo ndio unakuwa tatizo?
 
Pole mkuu,kwani huna cheti kweli au umepoteza au ndio yale mambo ya juu kwa juu ukapata leseni...?
 
Mkuu fungua pochi Tu hakuna namna
Hatuwezi kuwa watumwa wa kuwafungulia pochi kwa kila kitu ndani ya nchi yetu wenyewe. Kwa nini wanaweka utaratibu ambao wanajua utawaumiza watu kwa kufungua pochi? In fact, kujua kwamba ukifungua pochi uta renew leseni ina maana hiyo sheria waliyoweka ni useless, haisaidii
 
Wana vidriving school vyao uchwara mitaani wanavipigia chapuo ili waingize pesa, kichekesho wanaofundisha hawana hivyo vyeti
Na hilo ni tatizo sana. Hawa watu ili kujinufaisha wanahujumu kila kitu

  • wanahujumu SGR mabasi yao yapate abiria
  • wana complicate sheria kuuwapa askari ulaji kwa sababu wanawalipa mishahara kidogo
  • wanahujumu Mwendo kasi daladala zao na bajaji wapate abiria
  • wanahujumu Tanesco ili wauze majenerator
  • wanahujumu barabara kwa kuacha zijae mashimo ili watoe tenda za kuziba viraka kwa watu wao
  • wanahujumu kilakitu kama kuna namna watavuta pesa!
 
Ndiyo mambo ya kikao cha juzi cha Bashungwa,Police,LATRA kudhibiti ajali itakuwa!

Madereva wa serikali wana vyeti safi kutoka NIT ila fujo zao kila mtu anazijua.

Hawajui zebra crossing wala vibao vya 50 na 80.
Umeongea point sana Mkuu. Hivi hawa wajinga wanafikiri cheti ndio kinazuia uendeshaji wa kizembe? Cheti ndio kinazuia mtu ku-overtake bila kuchukua tahadhari - kwani wanafikiri mtu anaefanya hivyo hajui kuwa anafanya kosa? Cheti ndio kinazuia madereva wa mabasi kushindana huko barabarani?

Wanaacha kujikita kutengeneza miundo mbinu ambayo kwa asilimia 80% ndio inasababisha ajali wanakimbilia kusema madereva wawe na vyeti kupunguza ajali. Hebu wawapeleke boda boda wote shule wapewe vyeti waone kama Muhimbili kutapungua wagonjwa wa ajali za boda boda.

Hawa watu sijui wanatumia nini kufikiria!

Huu uzi nilifungua kwa kuwa najitambua katika udereva wangu wa zaidi ya miaka 30, na najua watu walioendesha gari kwa zaidi ya miaka 5 ni ujinga leo kuwaambia lete cheti.

Kwa wote mnaotarajia kusafiri kwa magari yenu kipindi cha December/January ningependa kuwakumbusha jambo la msingi sana hapa, kwa faida na uhai wenu


Cheti sio suluhisho la ajali, warekebishe barabara, zisiwe na mashimo na sehemu hatarishi ziwekewe climbing lanes

Angalia barabara ya Dar-Moro ilikuwa na ajali za kugongana karibu kila wiki. Tukashauri sana waweke climbing lanes. Walipoweka leo tumesahau ajali za barabara ya Dar-Moro. Kwa nini hawajifunzi? Ajali ngapi zinatokea kwa sababu ya mashimo au sehemu ndefu kutokua rafiki kwa overtake kwa sababu hakuna climbing lanes? Pale Mbeya Mbalizi, kuna mwinuko na hakuna climbing lane, kila siku ajali zinatokea pale, wanafikiri ni kwa sababu madereva hawana veti? Vyeti vitaondoa mashimo ambayo Tanroads wanazembea kuyaondoa?

Wamekaa wakafanya tathmini ya "cause and effect" ya ajali barabarani ndio wakagundua ni kwa sababu madereva hawana vyeti, really? Huyu Samia anitafute nimsaidie kumwekea mambo sawa nchini. Kuna ujinga mwingi sana unafanyika.

Hawa watu wanastahili kunyongwa au kupigwa risasi hadharani kwa ujinga wa kuongoza nchi kama huu.
 
Maisha hapa Tanganyika yanachekesha sana hapo wanataka ununue cheti tu na sio kwenda shule ya udereva. Hata zile stika nenda kwa usalama zilikuwa zinauzwa unampa mtu namba ya gari anakuletea.
 
Jibu limenyooka sana yani halina porojo.
 
Nenda driving school utaratibu ulishswekwa wazi....refresher course ni muhimu sana
 
Ukipewa amri isiyo halali usiisimamie kama mbwa anavyoitikia amri ya bwana wake
Ukiwa chini ya serekali au chini ya yeyote mwenye mamlaka juu yako amri zote atakazo zitoa kwako ni halali kama una swali kuhusu amri uliopewa nenda katekeleze kwanza swali utauliza baada ya kutekeleza amri yake.
 
Ni Sahihi kabisaa
 
Kwa sasa ukienda ku renew utaachiwa Daraja D. Daraja E na C huwezi kupewa bila cheti. Kwenye Daraja C wapo very sensitive huwezi pewa kirafiki kwa sasa watu wasikuambie habari ya penyeza rupia
 
Acha mboyoyo mbona kupata cheti ni chap zaidi ya muda uliotumia kulia lia apa JF.
Tafuta kachuo kokote uchwara Mpe msimamizi 20k uondoke na cheti swafi
 
punguza makasiriko, nyie wenye leseni za zamani ndio mmesababisha yote haya, mlikuwa mnasababisha maajari kila siku, sasa hivi unaambiwa ukasome unakaza fuvu, nenda kasome huwezi tupa leseni Pambaav
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…