Hii nchi sasa imefikia kuwa na watawala wa kipumbavu sana. Nimekuwa na leseni ya kuendesha gari kwa miaka 34, na siku zote nimekuwa niki-renew bila tatizo.
Leo hii nataka ku-renew TRA wananiambia mambo ya cheti cha udereva, shule sijui, nenda polisi na utumbo mwingi wa kuku kibudu.
Hivi hawa watu wanaokaa huko juu na kutunga hizi taratibu wana akili sawa kweli? Kama wameleta sheria mpya kwa nini zisitumike kwa wakataji wapya wa leseni za udereva? Niliwahi kusema humu JF, katika taasisi za serikali ninazozichukia kuliko zote, ni Polisi na TRA - kwa sababu hawa ndio wana mambo ya kijinga kupita kiasi.
Kawaida, unapotunga sheria mpya, huwa inaanza kutumika pale ilipotungwa na kwenda mbele. Huwezi kutumia sheria mpya "retroactively". Kwa mfano, huwezi kutunga sheria mpya mwaka 2025 kwamba wabakaji mbuzi wanyongwe, halafu useme hata wale waliobaka mbuzi miaka ya 1980 huko nao watafutwe tuwanyonge. Hakuna kitu cha namna hiyo.
Sasa hawa watu wanaokuja na taratibu za kijinga namna hii wana ubongo huko ndani ya vichwa vyao kweli?
Na nyie kina Mwabukusi, kwa nini mnakaa kimya utopoo kama huu unapofanyika nchini? TLS ipo kwa ajili ya nini na nani, vyama vya upinzani peke yake?
Nchi hii inahitaji mapinduzi - na hapa simaanishi CCM!