Nina mashaka na elimu walizonazo Madaktari pamoja na Wataalamu wa lishe!

Nina mashaka na elimu walizonazo Madaktari pamoja na Wataalamu wa lishe!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
2,753
Reaction score
12,932
Nsikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane!

Nimekuwa nikiwasikia watu wanaojiita "Madaktari" pamoja na watu wanaojiita "Wataalamu wa lishe" wakizungumza au wakitoa ushauri wa namna ambavyo mtanzania anapaswa kula ili kuyakimbia magonjwa ya FIGO,INI pamoja na KANSA!.

Wataalamu " Uchwara " hao wamekuwa hadi wakiwapangia watanzania nini chakutumia na kipi si chakutumia!.

Miongoni mwa Vitu ambavyo wamekuwa wakivipigia kelele ni vyakula vya wanga na kabohaidreti,ikiwemo

1. Mahindi na bidhaa zake
2. Viazi vitamu na bidhaa zake
3. Mhogo na bidhaa zake
4. Mchele na bidhaa zake
5. Nyama na bidhaa zake

Wameenda mbali sana hadi Hivi sasa wanadiliki kusema tusitumie matunda kwa wingi!

Mimi binafsi nimekuwa napata mashaka na wataalamu "Uchwara" hawa.

Jamii nyingi za Afrika espeshali Tanzania,tunajua kabisa kuna umasikini wa kutisha,na vyakula vikuu vya nchi zetu hizi ni NAFAKA na Bidhaa zake!

Hebu fikiria Tuache kula Wali tule nini?

Hebu fikiria watu waache kula ugali wale nini?

Hebu fikiria watu waache kula Viazi vitamu wale nini?

Hebu fikiria watu waache kula Viazi mbatata wale nini?

Hebu fikiria watu waache kula matunda wale nini?

Mi nilidhani watawashauri walimaji na wafanyabiashara waache kutumia kemikali mbaya za kuhifadhia mazao ambazo mwisho wa siku zinaleta madhara kwa walaji,lakini wao wamekuja na kelele nyingi za kuwazuia watu kula hivyo vyakula tajwa hapo juu!.

Zamani mazao yalikuwa yakihifadhiwa kwenye maghala ya kiasili yaliyotengenezwa kwa fito na kusilibwa kwa kinyesi cha ng'ombe na bado mazao yalidumu miaka guarani,Je hawaoni wafanyabisha walafi wa pesa ndiyo Tatizo la matatizo ya kiafya kwa jamii?,Nilidhani nguvu na kelele zielekezwe kwa wanadamu waishio Tanzania ya kwamba wasitumie nafaka zozote zilizohifadhiwa kwa kemikali lakini wao kutwa kutupigia kelele eti watu wasile Wanga kwasababu unaleta shida!

Sasa hamtaki tule hivyo vyakula mnataka tule nini kama mbadala?
 
Capture.PNG
 
Maisha hayana formula wapo watu gym muda huu wanapunguza Mwili umejaa mafuta wengine kutwa kuhangaika barabarani wanafanya mazoezi wapunguze Mwili
 
Hao dawa yao ni kuwasikiliza na kuwapuuza, kila mtu ana maamuzi yake binafsi juu ya maisha yake.

Za kuambiwa, changanya na zako 🤒 😎 😊
 
Umenena vyema. Niliwahi kwenda kwa wasabato kuingia kanisani nikakuta Moja ya vipindi vilivyokuwepo pale ni AFYA.

Dr akasema imefika Wakati Sasa wakuacha kula nyama nyekundu
Akasema wanyama wote wenye miguu minne hawafai Tena yeye akasema ana miaka13 Sasa hatumii.

Nikajiuliza tangu zamani najua wasabato hawali nguruwe na Bata Leo hii wamefikia Hadi kwenye ng'ombe,kondoo,mbuzi,swala,nyumbu nk?

Badae muda wa maswali ukafika
Sikusta kuuliza Wana shida Gani hawa wanyama?

Yule Dr wa mchongo akasema kama Kuna mtu anaweza nijibu ajibu

Bila kupoteza muda jamaa mmoja na tai yake ndefu Pana kama bapa la katani. Akasema saivi ng'ombe ana dungwa sindano sijui anapewa madawa Ili anenepe yaani nyama ya ng'ombe Kwa Sasa imejaa Sumu tupu. Aliendelea sana kuongea. Mwisho nikamwambia mwenye shida ni huyo ng'ombe au anayempa hizo dawa ndo mwenye tatizo?
Je kama Mimi nimefuga bila kutumia hizo Sumu Bado ni hatari kwangu?
Hapa umejumuisha wanyama wote wenye miguu 4 Hadi swala nk..

Mjadala ukawa Mpana Hadi kipindi kinaisha hatukupata chakula salama Kwa afya

Maana iwe nyanya,mchicha, matikiti yote Wanaitia madawa Ili yakuwe na kunenepa haraka. Shida sio mazao shida ipo Kwa watu.

Narudia Tena umenene vyema mkuu
 
Tukisema tumejifunza kutoka kwa Wazungu tutakua tumekosea?

Nafikiri itakuwa sahihi nikisema 'Una mashaka na Elimu ya Mzungu' Walakin tatizo lako mleta mada, unapenda kulalamikia-Unalalama lalama kuhusu Waafrika na Utamaduni wao. Tufanyeje sasa?
 
Mkuu sidhani kama nitasimulia tena hapa JF simulizi,nisamehe sana ndugu yangu!
Pole sana mkuu kwa walivyokutenda watu wale, wamekuacha na jeraha kubwa moyoni.

Ikikupendeza huko mbeleni, samehe urudi kwenye nafasi yako ya kuelimisha umma kupitia simlizi halisia za maisha ya kila siku.
 
UMUGHAKA Una hoja ya msingi sema tunyapuuzia sana mambo ya msingi na kuyapa kipaumbele mambo ya kipuuzi.
Kwanini zamani ilikuwa safe kutumia nafaka na baadhi ya vyakula vinavyoitwa hatarishi kwa afya ila leo imekuwa tofauti? Anatokea profesa au dokta katika kujenga hoja zake haina tofauti na anavyojua mtu wa darasa la saba. Tunasoma research za wazungu bila kujua wanafanya kwa lengo gani! Wataalamu wetu kupitia reseach tunazoletewa hawana muda ila kukariri tu na kutulisha matango pori.
 
Mi nadhani tatizo linaweza kuwa namna wanavyotafsiri theories wanazopitia. Maana kiingereza nacho wasipokuwa makini wanaweza kuelewa tofauti na dhana iliyokusudiwa.
Ipo siku wanaweza kutuambia hatukakiwi hata kulala, wanaweza kusema kulala ni nusu ya kufa hivyo jitahidi uwe macho, ufanye mazoezi ya kutopata usingizi
 
Back
Top Bottom