At Calvary
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 4,533
- 3,595
Kiukweli pana ugumu.M
Milioni 29 haiwezekani
Hivyo vya 2015 ulienda kuhakiki? Kama haujaenda Kuhakiki usitegemea kupiga kura.Pole.
Lakini wengine si wanavyo vya 2015.
Kwa hiyo Lissu hataenda kupiga kura?Hivyo vya 2015 ulienda kuhakiki? Kama haujaenda Kuhakiki usitegemea kupiga kura.
Mwaka 2015 wapiga kura walikuwa wangapi?Kweli inatia Shaka milioni 29 mmmmh siamini hata Mimi.
Acha tusibiri tuone
Cdm munahofu kubwa sana ya kushindwa. Mwisho wa siku mutajikuta hata nyinyi wenyewe hapo ufipa hamuaminiani.
Kama unaona tume imekosea, lete wewe idadi yako iliyo sahihi.
Kwa hiyo Lissu hataenda kupiga kura?
Mwaka 2015 wapiga kura walikuwa wangapi?
Mpango mzima wa wizi wa matokeo huanzia kwenye;
1. Kuandaa idadi ya wapiga kura - lazima hapa data ziwe coocked ili kuja kuhalalisha uongezaji wa kura upande wa CCM bila kuzidi idadi ya waliojiandikisha.
2. Uwepo wa vituo hewa - hii hitumika zaidi katika maeneo CCM ilipo na nguvu. Lengo ni kuongeza kura zaidi za urais kupitia kisingizio cha kushinda ubunge. Mbinu hii hutumika sana kwenye maeneo wapinzani wasiopo na nguvu.
3. Utumaji wa matokeo NEC badala ya kutangaza matokeo ya Urais kila kitu - hii husaidia ku monitor mwenenndo mzima wa idadi ya kura wanazoachwa nyuma CCM ili kuona jinsi ya kutwist vitu na kuongeza kura kwa CCM kufidia na kuzidi zile za wapinzani.
4. Kuamua tu kutangaza kisichokuwepo - inaootoke kila njia ni ngumu, maandalizi ya kiulinzi na usalama huandaliwa ili kutangaza kwa nguvu kwa kutumia Sheria dhaifu ya matokeo ya urais kutohojiwa popote.
Sina hakika kama upindishaji wa matokeo utatoa matokeo Salama mwaka huu.
Huenda historia ikawekwa na mwiko ukavunjwa. Stay tune.
NEC iweke majina ,ya wapiga Kura walionao ambao ni 29+ kwenye tovuti Yao watanzania wayaone online. Idadi iliyowekwa sio sawa ni kubwa zaidi . NI sawa na kusema zaidi ya nusu ya watanzania wamejiandikisha Jambo ambalo sio kweli.Pia sio kweli kuwa watanzania wapo 50 m, watanzania ni pungufu ya 50m.Makadirio ya Idadi ya watu Tanzania 2020 ni Milioni 59.7.
Idadi hii imegawanyika kama ifuatavyo:
1. Walioko chini ya miaka 15 ni zaidi ya 44.8%
2. Katikati ya miaka 15 hadi 64 ni 52%
3. Walozidi miaka 64 ni 3%
Miaka inayoruhusiwa kupiga kura ni zaidi ya miaka 18 ambayo tukiangalia katika huo mgawanyo inaleta picha kuwa nusu au karibu na nusu ya Watanzania wako chini ya miaka 18.
Hivyo kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi tayari tuna idadi ambayo inakaribi milioni 29[(44.8%(chini ya miaka 15)+ a waliokuwa na miaka 15-17)] ikiwa hawaruhusiwi kupiga kura.
Point yangu:
Idadi ya ambao wamejiandikisha ni milioni 29(kama nimekosea nirekebishwe) Idadi hii inaenda sambamba au kukaribiana na idadi ya watanzania halali wanao ruhusiwa kupiga kura(bila kujiandikisha).
Kwa elimu ya watanzania na majukumu yao naeza kusema, waliojitokeza kwenye kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura haikuwa kubwa kutokana na sababu kama zifuatazo
1. Kununuliwa kwa wapinzani(hivyo watu wengi kupuuzia hata swala la kuja kupiga kura)
2. Kupatikana kitambulisho ambacho kina nguvu kuliko cha kura (Kitambulisho cha Taifa kimeonekana kina nguvu sana katika maswala mengi hivyo watu wengi walokuwa wakijiandikisha kwa ajili ya kupata kitambulisho cha kura kwajili ya kazi zao, kupuuzia baada ya kupata mbadala.)
3. Mchezo mchafu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka jana(2019) huu ulipunguza kasi sana na morali kwa watu wengi.
Kwa hayo machache: Je, tunakubali kuwa idadi tulopewa ya walojiandikisha ni sawa?
Kama sio sawa basi kutakuwepo watu hewa ambao kazi yake wahusika wanaijua ni ipi.
Na kama ni kweli, basi niwapongeze sana NEC kuhamasisha watu kujiandikisha Kwenye Daftari la uchaguzi.