Mkuu,
Hofu yako ni yetu tulio wengi.
Ni hivi:
1) Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza idadi ya wapiga kura waliojiandikisha (2020) kuwa ni 29,188,347 (Ref: Taarifa ya NEC, August 19, 2020)
2) Makadirio ya Idadi ya watu Tanzania hadi sasa (2020) ni milioni 59,700,000 na idadi hii imegawanyika kama ifuatavyo:-
a) Watu (wananchi) wenye umri chini ya miaka 15 ni zaidi ya 44.8%
b) Watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 64 ni 52%
c) Watu wenye umri zaidi ya miaka 64 ni 3%
Tufanye uchambuzi:
i) Wapiga kura (kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi) ni miaka 18+
ii) Idadi ya wapiga kura (2020) waliotangazwa na NEC ni takriban 48.9%
iii) Kwa makadirio, idadi ya watu wasioruhusiwa kupiga kura kwa mujibu wa sheria (umri chini ya miaka 18 kutoka kundi 2(b) hapo juu) kuwa ni 1.1% ya wapiga kura wote
iv) Kwa hiyo, idadi ya wapiga kura kwenye uchaguzi wa 2020 ni 50% ya Watanzania wote. Hii ni sawa na watu 29,850,000
Uchambuzi huu hapo juu unamaanisha:
MOJA: Kwamba wakati wa kujiandikisha Watanzania WOTE walikuwepo hapa nchini na walijiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu 2020;
MBILI: Kwamba kila Mtanzania mwenye umri wa kupiga kura kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi amejiandikisha kwenda kupiga kura
Nikiri, tangu Uchaguzi Mkuu wa kwanza katika Tanzania huru, Uchaguzi wa mwaka 2020 ndio utakuwa na maajabu kuwa asilimia mia moja (100%) ya Watanzania wenye umri wa kupiga kura walijiandikisha kupiga kura!
Serikali ya awamu ya 5 inatuona wapumbavu kiasi hiki?