Nina mashaka na ujauzito wa mpenzi wangu

Nina mashaka na ujauzito wa mpenzi wangu

nyakandula

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
1,250
Reaction score
1,727
Habari, nipo kwenye mahusiano na binti fulani hivi kwa muda wa mwaka, sasa mara ya mwisho kukutana nae kimapenzi ni wiki tatu zilizopita na kabla ya hapo sijakutana nae kimapenz zaid ya miez mi3.. sasa juzi kaniambia anahisi ana mimba maana hajazion siku zake.

Nikamtumia pesa aende hosptal kupima.. baada ya kupima akanitumia ultrasound inasoma mimba ipo na ina week 5 na sku 2. Nimepiga hesabu zangu naona zinagoma nilitegemea angalau iwe na wiki 3 au zisizid 4.
Ila yeye sijamueleza hiki nachohisi kama mimba sio yang.

SWali langu je hizi ultrasound zinaonesha uhalisia au ni makadirio?

Na kama ni makadirio, je mimba ya wiki 3 inaweza kweny ultrasound ikasoma 5weeks?
 
Siku hizi ukifanya sex na Binti hasa single maza weka kumbukumbu sahihi. Siku akijichanganya tu kusema ana mimba mwambie tukapime ultra sound then tukae chini tuhesabu siku.
Mambizi, hawa mabinti mimba hugeuza mtaji .
Wengine hawana mimba wanataka pesa tu
Sasa hzo hesabu hapo ndio zinagoma, au ultrasound ni uhalisia au makadirio
 
Ikiwa mlifanya tendo la ndoa na mpenzi wako wiki tatu zilizopita na kipimo cha ultrasound kinaonyesha kuwa ana ujauzito wa wiki 5 na siku 2, inawezekana kwamba mtoto ni wako. Kipimo cha ultrasound kawaida hupima muda wa ujauzito kuanzia siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho ya mwanamke (LMP), ambayo ni takriban wiki mbili kabla ya yai kuachiliwa (ovulation) na mimba kutungwa. Hii inamaanisha kuwa ujauzito wa wiki 5 na siku 2 ungehusishwa na kutungwa kwa mimba takriban wiki 3 zilizopita.
 
Back
Top Bottom