Jumaa aweso ajitafakari. Hata Paul makonda ana afadhari anatatua migogoro kwa usikivu. Jumaa anatabia kama za wake zake
Jamaa anafikiri kutoa hukumu papo kwa papo ndio ataonekana anafanya kazi.Dawasa ni Idara kubwa ya Maji hapa Nchini,wanahudumia almost mikoa yote miwili ya Dar es Salaam na Pwani.
Kwenye Clip zake zote hajampa nafasi yoyote Kaimu Mkurugenzi wa Dawasa kusema chochote!.zaidi ya kumpa taarifa tu kuwa amemsimamisha kazi!.na lawama za uzembe!
Leo hayupo mbona pako vilevile tu?..
Mawaziri kama kina aweso wasikilize maelezo ya watendaji wao,waangalie kwa jicho la 3 ndani ya Idara hii kubwa Ili kubaini chanzo Cha tatizo ni nini?
Kama kweli Kuna mgomo,miundombinu mibovu au Uzembe ijulikane na hii changamoto itatuliwe.
Sio mtu anavamia tu matenki usiku anakuta hayana Maji,anavamia ofisi Moja ya Wilaya anaomba faili analikosa,uamuzi anaouchukua ni kumfuta kazi Kaimu Mkurugenzi!
Aweso apunguze siasa kwenye Maji,hili ni jambo nyeti sana kwenye Maisha ya watu.
Kama kweli anayo nia ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo la Maji ndani Dawasa,asifanye maamuzi ya kukurupuka kwa nia ya kuwafurahisha watu "flani".
Huyo Kaimu Mkurugenzi umemtumia kama scapegoat tu,"bangusilo".
Hamkumtaka toka mwanzo,mtu anakaimu Mwaka mzima!.anapata wapi authority huyu ya kuimplement mipango yake na ubunifu wake?
Mtu unamfunga kamba mikono,akishindwa kuperform mzembe!!