KERO Nina masikitiko makubwa: Pamoja Waziri kuchukua hatua na kutoa maelekezo, bado Kinyerezi maji yanatoka kwa manati

KERO Nina masikitiko makubwa: Pamoja Waziri kuchukua hatua na kutoa maelekezo, bado Kinyerezi maji yanatoka kwa manati

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Annie X6

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2023
Posts
704
Reaction score
1,331
Mh waziri una watendaji viburi sijawahi kuona. Au wamegoma? Kuna shida gani ndani ya wizara yako?

Tumekaa miezi na miezi maji hayatoki na leo hakuna maji pamoja na ujio wako. Hawa watendaji wametoa wapi. Ni Watanzania kweli hawa?

Wana roho mbaya sana. Kama tank halikuwa na maji na wamejaza kwanini maji yanatoka dakik 5 na kukatika?

Leo ni siku ya 3 tangu matone matone yalipopita kwenye bomba langu. Kwanini kuna hali kama hii?

Naweka location hapa.

Pia soma Dar: Waziri Aweso amemsimamisha Meneja wa DAWASA, Kinyerezi Burton Mwalupaso Kwa kushindwa kutekeleza vyema majukumu yake

Location
Screenshot_20240707_181143_Maps.jpg

Hapa hakuna maji
 
Wanatutesa sana hawa watu
Poleni sana, kama huko kinyerezi sio ur permanent residence ,fanya mpango uhamie sehemu nyingine. Si unajua serikali yetu hii
 
Nimepanga lkn. Kwanini wafanye hivi. Nikijenga siwez kukaa huko maeneo
 
Mh waziri unaeatendaji viburi sijawahi kuona. Au wamegoma? Kuna shida gani ndani ya wizard yako?

Tumekaa miezi na miez maji hayatoki na leo hakuna maji pamoja na ujio wako. Hawa watendaji wametoa wapi. Ni Watanzania kweli hawa?

Wana roho mbaya sana. Kama tank halikuwa na maji na wamejaza kwa nini maji yanatoka dakik 5 na kukatika?

Leo ni siku ya 3 tangu matone matone yalipopita kwenye bomba langu. Kwa nini kuna hali kama hii??
Naweka location hapa.

Location
View attachment 3035918

Hapa hakuna maji
Kubadili mtu pekee siyo solution ya baadhi y matatizo
 
kazi yao ni kujazana maofisini kupiga umbea tu, halafu uta wasikia tuna taka ongezeko la mshahara..
 
Si rahisi kuona uzembe ule

Mtoni maji yapo
Umeme upo
Njia pipe zipo
Mtandao wa maji upo
Hela zipo
Pump zipo
Kama hazifanyi kazi
mafundi wapo
Watu wapo
Matank yapo

Ila
Hayana maji
Wateja wanalipa
Tatizo ni nini??
 
  • Thanks
Reactions: I M
Aweso kamuondoa kwa mbwembwe Kaimu Mkurugenzi wa Dawasa,utadhani akiondoka yeye,ataondoka na matatizo yote ya Maji.
Mbona Maji bado hayatoki na matenki yamejaa!?
 
Jumaa aweso ajitafakari. Hata Paul makonda ana afadhari anatatua migogoro kwa usikivu. Jumaa anatabia kama za wake zake. Nibkama petrol ⛽️ anawaka tu. Yule dc nae anawakawaka flan
 
Jumaa aweso ajitafakari. Hata Paul makonda ana afadhari anatatua migogoro kwa usikivu. Jumaa anatabia kama za wake zake
Jamaa anafikiri kutoa hukumu papo kwa papo ndio ataonekana anafanya kazi.Dawasa ni Idara kubwa ya Maji hapa Nchini,wanahudumia almost mikoa yote miwili ya Dar es Salaam na Pwani.
Kwenye Clip zake zote hajampa nafasi yoyote Kaimu Mkurugenzi wa Dawasa kusema chochote!.zaidi ya kumpa taarifa tu kuwa amemsimamisha kazi!.na lawama za uzembe!
Leo hayupo mbona pako vilevile tu?..
Mawaziri kama kina aweso wasikilize maelezo ya watendaji wao,waangalie kwa jicho la 3 ndani ya Idara hii kubwa Ili kubaini chanzo Cha tatizo ni nini?
Kama kweli Kuna mgomo,miundombinu mibovu au Uzembe ijulikane na hii changamoto itatuliwe.
Sio mtu anavamia tu matenki usiku anakuta hayana Maji,anavamia ofisi Moja ya Wilaya anaomba faili analikosa,uamuzi anaouchukua ni kumfuta kazi Kaimu Mkurugenzi!
Aweso apunguze siasa kwenye Maji,hili ni jambo nyeti sana kwenye Maisha ya watu.
Kama kweli anayo nia ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo la Maji ndani Dawasa,asifanye maamuzi ya kukurupuka kwa nia ya kuwafurahisha watu "flani".
Huyo Kaimu Mkurugenzi umemtumia kama scapegoat tu,"bangusilo".
Hamkumtaka toka mwanzo,mtu anakaimu Mwaka mzima!.anapata wapi authority huyu ya kuimplement mipango yake na ubunifu wake?
Mtu unamfunga kamba mikono,akishindwa kuperform mzembe!!
 
Kuna mgomo wa nini hapo Idara ya maji ya Mkuu
 
Jamaa yangu yuko Segerea anasema toka huu mwaka uanze maji alipata kwake mara 1 tu Januari baada ya hapo hayajawahi kutoka na amehudhuria Dawasa kulalamika lakini wapi.

Hapa Dar maji ni tatizo, miaka 60+ ya uhuru chini ya ccm.
 
Back
Top Bottom