Nina mbuzi zaidi ya 900 dar, nauza bei nafuu sana!!!ofa ya 2014

Joined
Aug 15, 2013
Posts
5
Reaction score
5
Wadau
katika kupambana na maisha ili kupunguza msongo wa mawazo wa kutegemea mshahara mwisho wa mwezi, nilianza ufugaji wa mbuzi na sasa nina zaidi ya mbuzi 900 katika mabanda yangu hapa dar es salaam na wengine zaidi ya 1500 kwenye mabanda yangu mkoani morogoro.
Ili kuboresha huduma na kumpunguzia mteja gharama, ninaweza kukuletea mbuzi mpaka mlangoni kwako kwa gharama zangu. Bei zangu ni za chini ukilinganisha na masoko ya mbuzi yote yaliyopo hapa dar es salaam. Nina mbuzi wa kuanzia 75,000 mpaka 100,000 kutegemea na ukubwa wake.
Kwa anayehitaji mbuzi wazuri kwa bei nafuu asisite kunitafuta kwa simu no.0786 294545
karibuni
 
Mkuu
Soko la mbuzi halijawahi kuwa tatizo hata kidogo

kwanza mbuzi ulio nao ni wengi saana..unaweza uza mpaka uarabuni kama utataka na ni rahisi saana..

zunguka kwenye mabaa maarufu wanayochoma mbona ni wanunuzi tena kwa bei nzuri tu.....
 
Mbuzo wako aina gani, kienyeji pure? Wanazaa pacha au? Nitakutafuta nipate wa kufuga
 
hongera sana mkuu tupe siri umewezaje kufuga mbuzi wote hao hapa dar
 
Daah!mkuu mbuzi 900 dar?!?!unawalisha vitumbua nini?(joking muzee)...ila yataka moyo maanake hivi vijamaa raha yake uvikute vimebanikwa jikoni kwa mangi,ila vikiwa hai visumbufu balaa!unatoa huduma ya kuwachinja pia?nitakutafuta....
 
hahaaaa usije uliza kama ana mkarinanga na machalali pia? nimecheka sana
 
Daah!mkuu mbuzi 900 dar?!?!unawalisha vitumbua nini?(joking muzee)...ila yataka moyo maanake hivi vijamaa raha yake uvikute vimebanikwa jikoni kwa mangi,ila vikiwa hai visumbufu balaa!unatoa huduma ya kuwachinja pia?nitakutafuta....

Kweli kaka, Mbuzi mia tisa Dar siyo mchezo!!! MUUNGWANA MKUU unafugia wapi tuje kujifunza, hilo ni shamba darasa tosha mkuu, HONGERA SANA. Ongea na mkuu Prodigal Son akuunganishe na waarabu mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana....ukitaka mradi aw ufugaji usio umiza kichwa fuga mbuzi....hawana pressure km ng'ombe na kuku...
 
Mkuu, MBUZI?!!!!...navyowajua hawapendi kufungiwa ndani, halafu wanakula balaa, unafuu unaanzia wapi mkuu?
 
Jamani mbuzi 900 sio mchezo, labda typing error,
Mi ninao kama 50 hivi, shughuli yake sio mchezo, na nina wafuga huria sababu mashamba ya majirani zangu hayajaendelezwa. Sasa wewe 900 !!!!!!. namjua mmoja pale pande za Kibada, anao wengi sana, lakini yy ni tajiri hasa. Kama ndio wewe, basi itakuwa kweli.
 
malila mbuzi wako unawafugia eneo gani huko morogoro,napenda kuja kuona hayo maeneo
 
Nina mpango wa kuwafuga,nshapata eneo la ekari 20 kisarawe,nahitaji shamba darasa,unafugia wapi nije kujifunza?
 
Jamani mbuzi 900 sio mchezo, labda typing error,
Mi ninao kama 50 hivi, shughuli yake sio mchezo, na nina wafuga huria sababu mashamba ya majirani zangu hayajaendelezwa. Sasa wewe 900 !!!!!!. namjua mmoja pale pande za Kibada, anao wengi sana, lakini yy ni tajiri hasa. Kama ndio wewe, basi itakuwa kweli.

Kweli Mkuu, kama mtu anamiliki mbuzi mia tisa basi huyo kwa hapa nchini tunaweza kumweka kwenye kundi la "mfugaji mkubwa", Mkuu malila huyo jamaa ungetupigia hata picha za mabanda yake ya mbuzi tukahamasika nayo mkuu, au ukiomba utembelee kujifunza si anaweza kukubali? Huenda sisi tunakosea kuwafuga kienyeji, mbuzi wengi niliowahi kufuga ni mbuzi 120, lakini wachungaji walikuwa wanalala hoi kila siku, nadhani ukiwafuga kisasa zaidi inawezekana, tatizo sijajua chakula bora cha mbuzi ukiwafuga kisasa uwalishe nini, na gharama zake zikoje!
 
Wadau
katika kupambana na maisha ili kupunguza msongo wa mawazo wa kutegemea mshahara mwisho wa mwezi, nilianza ufugaji wa mbuzi na sasa nina zaidi ya mbuzi 900 katika mabanda yangu hapa dar es salaam na wengine zaidi ya 1500 kwenye mabanda yangu mkoani morogoro.
Ili kuboresha huduma na kumpunguzia mteja gharama, ninaweza kukuletea mbuzi mpaka mlangoni kwako kwa gharama zangu. Bei zangu ni za chini ukilinganisha na masoko ya mbuzi yote yaliyopo hapa dar es salaam. Nina mbuzi wa kuanzia 75,000 mpaka 100,000 kutegemea na ukubwa wake.

Kwa anayehitaji mbuzi wazuri kwa bei nafuu asisite kunitafuta kwa simu no.0786 294545
karibuni

Mbona sasa simu haipatikani? Biashara gani hii? Simu inatakiwa kuwa on muda wote.
 
Back
Top Bottom