Nina Miaka 27 lakini watu wananiona kama mzee

Nina Miaka 27 lakini watu wananiona kama mzee

Mtindo wangu wa maisha na kuvaa kwangu navaa kama kijana na mambo yangu ni ya vijana lakini watu wananiona kama mzee.

Kuna wazee wamenizidi umri lakini wananiamkia na kunipigia magoti na Mimi nabaki kuwashangaa.Nikijiangalia kwenye kioo naona uumbaji wa Mungu upo sahivi Wala sio mimi sio Mzee kama wao wanavyoniona.

Wengine wananiita Babu.Wengine wanasema nitafute wazee wenzangu niwaoe.Cha ajabu wanashindwa kutambua wao wananiona Mzee ila napiga kazi kama kijana .

Huu ni ugonjwa gani na dawa gani naweza kutumia wataalam maana nimechoka kuitwa na kudhaniwa Mimi ni Mzee wakati Bado Mimi ni Kijana.
Tafuta pesa, kula vizuri vaa smart, jipende kama una kipara tafuta style ya nywele itakakayokupendeza, vaa miwani, jiweke kimazoezi punguza kuvaa mabwanga na story za kizee achana nazo....
 
Kibali umri umekutupa mkono jomba
Miaka 27, ndio umri umemtupa mkono? Sio kweli. Huyo bado ni kijana mbichi kabisa. Kuwa na mwonekano wa uzee ilhali mtu ni kijana kunachangiwa na mbalimbali yakiwemo ya kiafya na ULOZI. Umri wa ujana unaisha mtu anapofikisha miaka 35. Baada ya hapo unafuata umri wa utu uzima. Uzee unaanzia miaka 60. Ndiyo maana hata serikali imeweka umri wa kustaafu kwa lazima kuwa ni miaka 60.
 
Jitahidi kuna vitu natural kama mchicha sana na matunda, Acha mavyakula ya kukaanga.

Kunywa maji mengi kwa siku(kama hufanyi kazi ngumu basi angalau lita mbili nusu kwenda mbele) kama ni kazi ngumu zaidi ya lita tatu na nusu kwa siku.

Acha na soda tumia juice sio za viwandani ila za kutengeza ila mara moja moja

Punguza sana matumizi ya vyakula vyenye sukari hasa za kutengeneza labda zikizoko kwenye matunda.

Fanya mazoez kiasi asubuh na jioni.

Usifunge nywele ndefu, nywele ziwe za brashi na usifuge midevu nyoa bakiza kidogo za kuonesha uwakiume.

Usivae manguo makubwa . Vaa nguo za size na za kwenda na muda na jitahidi kuzipasi

Usitumie chumvi nyingi na ya kuongeza mfano kwenye nyama choma.. Ila achana na nyama tumia zaidi mboga za majani kwa vyakula vyako. Yaaan hata wali piga na mboga za majani.

Punguza kabisa stress hiili ndo kubwa ambalo ni gumu ila jifunze kuacha stress
 
A
Mtindo wangu wa maisha na kuvaa kwangu navaa kama kijana na mambo yangu ni ya vijana lakini watu wananiona kama mzee.

Kuna wazee wamenizidi umri lakini wananiamkia na kunipigia magoti na Mimi nabaki kuwashangaa.Nikijiangalia kwenye kioo naona uumbaji wa Mungu upo sahivi Wala sio mimi sio Mzee kama wao wanavyoniona.

Wengine wananiita Babu.Wengine wanasema nitafute wazee wenzangu niwaoe.Cha ajabu wanashindwa kutambua wao wananiona Mzee ila napiga kazi kama kijana .

Huu ni ugonjwa gani na dawa gani naweza kutumia wataalam maana nimechoka kuitwa na kudhaniwa Mimi ni Mzee wakati Bado Mimi ni Kijana.
Au unakunywa sana visungura
 
Shikamoo mzee ,punguza unoko kuwakodolea watu macho, kuvaa mikoti na muhimu wewe ni kijana wa zamani
 
Kuna mambo Mengi katika hilo yakiwapo.
1.Suala la Kiafya.
Huenda ngozi yako imesinyaa na imekosa nuru.Hapa angalia sana lishe yako. Na inahitajika sana ushauri wa kitaalamu.

2.Uvaaji.
Kama unavaa nguo za watu waliokuzidi umri lazima uonekane kama mzeee.
 
Mtindo wangu wa maisha na kuvaa kwangu navaa kama kijana na mambo yangu ni ya vijana lakini watu wananiona kama mzee.

Kuna wazee wamenizidi umri lakini wananiamkia na kunipigia magoti na Mimi nabaki kuwashangaa.Nikijiangalia kwenye kioo naona uumbaji wa Mungu upo sahivi Wala sio mimi sio Mzee kama wao wanavyoniona.

Wengine wananiita Babu.Wengine wanasema nitafute wazee wenzangu niwaoe.Cha ajabu wanashindwa kutambua wao wananiona Mzee ila napiga kazi kama kijana .

Huu ni ugonjwa gani na dawa gani naweza kutumia wataalam maana nimechoka kuitwa na kudhaniwa Mimi ni Mzee wakati Bado Mimi ni Kijana.
Huo si ugonjwa ndugu,hata mi nakaribua fifty, lkn wanaonizidi hata miaka 20,wananiamkia,wengine wa mama wakubwa,hadi sometime natamani niwatokee!!!,,lkn mhimu we hakikisha hauchakai hasa kimavazi,ngozi isipauke,zaidi ya hapo waache waongee wala usiwe na wasi.
 
Ila u mzee kweli hali hii ujana utoke wapi wewe shkamoo

1000321020.jpg
 
Back
Top Bottom